Waziri wa Elimu anasimamia asichokiamini? Mwanae anasoma English Medium

Ungefananishia na waziri mwenzake kipindi cha nyerere sasa ndo ingekuwa bora zaidi... hatahivyo, mtu yeyote (including wewe) hapangiwi wala halazimishwi shule ya kumpeleka mwanaye kusoma as long as anamudu masharti havunji sheria
 
Kwani private schools hazisimamiwi na Wizara ya Elimu?
 
Wanafiki tu hao. Kuwa Waziri na kumsomesha mtoto Ulaya hakumfanyi asijue kinachoendelea shule za hapa. Yeye no mdau wa elimu, na isitoshe ametokea huko huko Kayumba.
 
Reactions: RMC
Kusoma nje ndio kupata exposure ,au umeamua tu kumnanga JPM ,eti kakosa elimu ya nje ,wewe ulosoma wap? Elimu ya nje inasaidia ,kujua kingereza? Shame on u!
 
Naona una hallucination kijana. Unamtafutia visa tu waziri. Kwani amefanya kosa gani kupeleka watoto wake katika shule anayotaka kama uwezo upo. Achana na haya mawazo ya kijima dogo.

Nadhani umekurupuka soma bandiko vizuri.Waziri ndio msimamizi Mkuu wa sera ya Elimu na ndio mgawaji wa fedha za Elimu ambazo upelekwa mkoani hadi Wilayani.Fedha za Serekali hazipelekwi English Media .
 
almost mawaziri na wabunge wote watto wao wapo international , had watoto wa msukuma ila wanawalazimisha msomeshe kayumba KISWAHILI MEDIUM.
 
Mama Ndalichako, Ummy ikiwa watoto wenu hawasomi shule za serekali wakati nyinyi ni wasimamizi wakuu wa elimu Tanzania basi hakuna nafasi nyingine zaidi ya kujiuzulu.
Tutajieni mawaziri na viongozi wote ambao watoto wao wanasoma shule za private.
 
Naona una hallucination kijana. Unamtafutia visa tu waziri. Kwani amefanya kosa gani kupeleka watoto wake katika shule anayotaka kama uwezo upo. Achana na haya mawazo ya kijima dogo.
Its because of people like you tz will remain among the poorest countries in this world, if you dont understand what the topic is all abaut, just shut up pls, this is a discussion of another level, sio ya pale kwenu kijiweni
 
Kusoma nje ndio kupata exposure ,au umeamua tu kumnanga JPM ,eti kakosa elimu ya nje ,wewe ulosoma wap? Elimu ya nje inasaidia ,kujua kingereza? Shame on u!
Unaelewa nini kuhusu neno "exposure?"

Na ni wapi kwenye comment yangu nimezungumzia kuhusu kujua "Kiiingereza?"
 
Una kichaa wewe, kwanini wanasema wameboresha elimu kama wameboresha kwanini watoto wao wasiwe wa mfano?
 
Wazazi wapi? Hawa wa kibongo? Ambaye yupo radhi awashe gari hadi posta hata akichelewa foleni ili aonekane anazo ikiwa kuna UDART ambayo anaweza wahi bila tatizo.
Hii nayo inahitaji tafakuri. Lakini mimi nakumbuka miaka ile tusoma. Wanafunzi ambao hawakuchuguliwa kjiunga na kidato cha kwanza shule za umma,hao ndo wazazi wao waliwatafutia shule binafsi. Lakini sasa imekuwa kinyume chake. Aliyechaguliwa shule ya umma haendi badala yake anatafutiwa na mzazi shule binafsi kwa udi na uvumba.
 
Wabongo tunapenda show offs na ile trend ya kupeleka watoto shule za kata hata kwa wazazi wenye ilikuwa ina influence hata usimamizi na maboresho ya shule sababu hata michango walitoa panapohitajika.

Sasa sahizi wazazi wameamua kuzi abandon zile shule jumla jumla sababu ya stigmatization. Kwamba kila mzazi hasa wanawake eeh staki mwanangu asome kata ntajipiga piga tu asome shule ya maana. Stress zinahamishiwa kwa baba hapo lazma atafute million 4 za kulipia ada watoto wake wawili kila mwaka ili mama awadolishie wenzie 😅!

Kwahio imeonekana kama dhambi vile kwa watoto kusoma kata wanaopelekwa kata ni wale ambao wazazi wao wako hoi sana kiuchumi!
 
Kwa sababu ww ni public servant lazima watoto wako wasome shule za kata?this is such a dumb take....haya mawazo ni ya kidikteta.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…