Waziri wa Elimu anasimamia asichokiamini? Mwanae anasoma English Medium

Waziri wa Elimu anasimamia asichokiamini? Mwanae anasoma English Medium

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] amna namna nchi inatia hasira sana hii ila ndio home sasa tufanyaje!

Kila mtu anatamani aingie serikalini sikuhizi sio kwamba ni kuna maslahi sana ila tu jinsi waheshimiwa wanavyomenya ile inawapa hamasa wanahisi wakiingia tu watakuwa karibu na bata!

Sasa mtoto kama huyo akipewa wadhifa unafikiria kuna analojua! Tabu na shida anaziskia tu toka kazaliwa yeye amekula kwa ubua tu shule anafuatwa na VX V8 yenye bendera mpaka kwao sijui Mbezi au Masaki! Likizo anaenda Mbugani kushangaa wanyama
Jaman mwenye nacho huongezewa, asiye nacho hunyang'wanya chote [emoji24][emoji24][emoji24]
 
Hivi kumbe aliungaga UDOM yule hahaha na sijui atakuwa ofisi gani kumamae bongo raha sana ujue! Ukute amepachikwa wizarani huko na atahudumu kwa raha mustarehe na mama Ndalichako ndio kapewa ulezi awe mlezi wake asisumbuliwe!

Ila ingekuwa wewe system ingekutema kama anaconda alivyomtema yule mzungu baada ya kummeza 😂😂😂! Yani huna SIFA braza kaanze Certificate level huko!
Hahaha Yuko zake kule kwny ofisi ya kabudi ya zamani.

Hahah yaani sijui hata ungeanzia wapi kujisogeza mitaa Ile,Kwanza sijui hata ilikuaje akapewa div 4 wkt Necta iko chini ya dingi ake,au hapo yenyewe ukute ali differentiate constant(kapata zero) afu mabroo wakaona ngoja tuinuane tu., Hahah.
 
Hivi kumbe aliungaga UDOM yule hahaha na sijui atakuwa ofisi gani kumamae bongo raha sana ujue! Ukute amepachikwa wizarani huko na atahudumu kwa raha mustarehe na mama Ndalichako ndio kapewa ulezi awe mlezi wake asisumbuliwe!

Ila ingekuwa wewe system ingekutema kama anaconda alivyomtema yule mzungu baada ya kummeza [emoji23][emoji23][emoji23]! Yani huna SIFA braza kaanze Certificate level huko!
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hivi kumbe aliungaga UDOM yule hahaha na sijui atakuwa ofisi gani kumamae bongo raha sana ujue! Ukute amepachikwa wizarani huko na atahudumu kwa raha mustarehe na mama Ndalichako ndio kapewa ulezi awe mlezi wake asisumbuliwe!

Ila ingekuwa wewe system ingekutema kama anaconda alivyomtema yule mzungu baada ya kummeza 😂😂😂! Yani huna SIFA braza kaanze Certificate level huko!
Ukute yupo BOT au bandarini ndiyo sehemu zao hizo
 
😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂 amna namna nchi inatia hasira sana hii ila ndio home sasa tufanyaje!

Kila mtu anatamani aingie serikalini sikuhizi sio kwamba ni kuna maslahi sana ila tu jinsi waheshimiwa wanavyomenya ile inawapa hamasa wanahisi wakiingia tu watakuwa karibu na bata!

Sasa mtoto kama huyo akipewa wadhifa unafikiria kuna analojua! Tabu na shida anaziskia tu toka kazaliwa yeye amekula kwa ubua tu shule anafuatwa na VX V8 yenye bendera mpaka kwao sijui Mbezi au Masaki! Likizo anaenda Mbugani kushangaa wanyama
Niliwahi kumsikia Erick shigongo aakihojiwa akasema watoto wake walikua wanajua Mchele hua unatengenezwa kiwandani Kama pipi vile,sio Kwamba unalimwa.

Nikamcheki tu nikasema hiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii.
 
Mama Ndalichako, Ummy ikiwa watoto wenu hawasomi shule za serekali wakati nyinyi ni wasimamizi wakuu wa elimu Tanzania basi hakuna nafasi nyingine zaidi ya kujiuzulu.
kwani uliambiwa hizo shule za serikali ni za kwao binafsi?
Anochewza professor ni kusimamia kwa ukamilifu sera ya taifa ya elimu,na hii hajatunga yeye,kwa hiyo usimpangie wapi pa kusomesha wanawe
 
Hahahahhah na huko hamnaga kufuatiliana kabisa naskia dadake mwendazake alikuwa hazina nahisi atakuwa kawekwa jirani na shangazi yake kwa uangalizi [emoji23][emoji23][emoji23]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] mtoto wake yule bonge mdogo, naskia nae eti amepewa kitengo kikubwa, hata taaluma yake hajamaliza bado. Mweeeeh
 
Mazingira ukiyawaza sana hutafanya kitu mzee mwenzangu! Cha muhimu usiibe wala usikabe mtu yani! Ikiingia buku au laki kila siku zote pesa kaka tutengeneze mikondo tu! 10 years ahead tutahesabu achievements!
Sikatai mkuu tuna bambikwa kodi huku balaa mara unalazimishwa VAT huku mtaji wa kuunga unga
 
Hata mimi ningekua waziri ningemsomesha mwanangu shule nzuri kabisa, ada ni mamilioni ila wananchi nitawahubiria elimu bure na makofi wanipigie....
 
Wao ni wazalendo kutumikia wananchi miaka yote lakini huwakuti kwenye chaki wala utendaji mtaa wao uzalendo wao ni kuitwa waheshimiwa.
... hiyo ndio inaitwa the ruling class Chief! Kuiondoa ili kurudisha madaraka kwa wananchi sio lelemama! Shida zaidi ni mbumbumbu waliotengenezwa makusudi "kuiabudu" the ruling class.
 
Heshima sana wanajamvi,

Tanzania pengine ni nchi pekee duniani yenye maajabu yasiyoweza kulinganisha au kufananishwa na nchi nyingine.

Ni jambo la ajabu waziri wa elimu msimamizi wa elimu yenu na mustakabali wetu wa siku zijazo.Waziri wetu huyu watoto wake hawasomi katika shule za umma,wapo katika zile shule zetu "english medium" binafsi. Ikiwa Waziri hana imani na shule zetu za Kata au ukipenda St Kayumba na wakati huo huo yeye ni msimamizi na mwangalizi au ukipenda mlezi mkuu hapeleki watoto wake huko maana yake nini ?.

Mwl Nyerere watoto wake walisoma Tabora,Bunge,Tambaza. Waziri wake wa Elimu aliyajua matatizo yote ya elimu kwakuwa hata watoto wao walisoma shule hizo hizo.Watoto wake walikwenda JKT,walipigana vita vya Uganda hapakuwepo ubaguzi wa aina yoyote kama tunavyoona leo.

Ifike mahali uzalendo usisitizwe katika nyanja kama hizi,ukibahatika kupata nafasi ya kuongoza wizara ya Viwanda basi wewe kama Waziri lazima uonyeshe mfano wa kununua bidhaa za Tanzania mfano thamani za maofisini,nguo. Ukibahatika kuongoza Wizara ya Elimu lazima watoto wako wasome shule za kata wakutane na changamoto za ukosefu wa waalimu,vitabu madarasa,matundu ya choo na nk.Hii itasaidia Wizara kupanga mipango ambayo italenga kuondoa kero zote zinazozikumba shule za umma.

Ni aibu kwa jamii iliyostaharabika kuhubiri jambo ambalo kwa hakika wewe mwenyewe huliamini unalitilia shaka,unalionea aibu,hulipendi hauko tayari jamii yako ya karibu kwa maana ya watoto wako wasilishiriki.

Mama Ndalichako, Ummy ikiwa watoto wenu hawasomi shule za serekali wakati nyinyi ni wasimamizi wakuu wa elimu Tanzania basi hakuna nafasi nyingine zaidi ya kujiuzulu.
Watu mnafukunyua haswa hadi picha ya mwanae mmeipata! Du!
 
Back
Top Bottom