Waziri wa Elimu na TAMISEMI, ni sawa Wanafunzi Shule za Serikali kuambiwa waende na dissecting kit na vitabu vya tahasusi?

Waziri wa Elimu na TAMISEMI, ni sawa Wanafunzi Shule za Serikali kuambiwa waende na dissecting kit na vitabu vya tahasusi?

Kuna vitu ukiambiwa kununua vinaleta mantiki na vingine havileti. Tatizo la shule za Tanzania wanajaribu ku-complicate mambo bila sababu. Kwa mfano hili la shuka. Kwani ni lazima yawe na rangi moja? Vitu kama vitabu inaweza kueleweka lakini vitu kama dawa ya chooni, mafyekeo etc ni vitu vinatakiwa kutolewa na shule.
Yeah vyote ulivotaja navyo vina umuhimu wake mfano shuleni lazima kuwepo na uniformity na usafi ni muhimu pia
 
Zamani ni lini?na shule gani hiyo?
Mimi nilisoma Bihawana Secondary Dodoma Combination ya CBA niligraduate 2010 form six. Mbaya zaidi hata hukukuepo na waalimu wa masomo yote kwahiyo vitabu vilitusaidia Sana tena Sana . Kumbuka Bihawana secondary ni miongoni mwa shule kongwe kabisa nchini

Sent from my CPH1937 using JamiiForums mobile app
 
3. Nikajiuliza ina maana shule hii anayokwenda kusoma mwanangu haina vitabu? Imekuwaje inaanza kidato cha tano huku ikiwa haina vitabu? Kipi kilipaswa kuanza, majengo au vitabu na walimu kwanza? Hivi mzazi kama nanunua vitabu vyangu kwa ajili ya mwanangu, si bora asomee nyumbani sasa na siku ya mtihani aende kufanya tu...?

Hili wazo lako zuri pia, asomee nyumbani ataenda tu kufanya mitihani, na hao panya chura atawapasua hapo hapo nyumbani na wembe wa topaz.
Muwaeleze na wazazi wao huko majukwaani basi. Sio muwaache watoto wanakwenda kupata shida huko shuleni.
 
Tena shukuru sasa Hiv mnaandikiwa sis ilikuwa unaripot ndo Unajua kumbe kuna dissection kit, kumbe kuna chandi, kumbe kuna scientific calculator, kumbe kuna vitin pamflect
Yeah hata sisi ilikuwa hivo dissection kiti niliuziwa tsh 30 enzi hizo na calculator mbona nilinunua bila kulazimishwa?nina uhakika huyu mzee akisoma comments atajiona bonge la mbwiga,ataukimbia uzi
 
Hayo ndo matatizo ya kuwa LY. Sasa Kama umeona Elimu ni gharama, jaribu Ujinga. Otherwise mnunulie BS ya Biology, Chand za masomo yote matatu, Nelkon book of Physics kwa kuanzia. Kama huwezi, lala mbele.
 
Ndugu mzazi acha kulalamika shule za advance siku zote zipo hvo mnunulie mtoto mahitaji hayo
Hujui uandikacho wewe. Ni wazi umezaliwa juzi, umekuta matatizo haya na unadhani ndivyo ilivyo....

Mimi nimesoma O' Level, Shule ya Sekondari Kibaha [boarding]....

Nikasoma A'Level Tabora Boys' Sec. School [boarding]....

Hizi zote ni shule za serikali. Kote huko sikuwahi kuagizwa kwenda na kitabu chochote. Kila kitu tulikikuta hapo hapo shuleni...

Na zipo shule za kata [A'Level Sec. Schools] haziagizi mpaka vitabu kwa sbb shule haiwezi kuitwa shule isipokuwa ina mambo matatu muhimu na ya msingi...

[A.] Majengo (madarasa)

[B.] Walimu

[C.]. Vifaa vya kufundishia na kujifunzia

Sasa jibu swali hili; Kwanini hii shule ya serikali iitwe shule wakati haina vifaa vya kujifunzia na kufundishia i.e vitabu, vifaa vya maabara, chaki nk nk...???
 
Wazazi wa siku hizi hovyo sana, mnazaa tu ila hamna mpango na watoto wenu, mimi nimewahi kumsomesha mdogo wangu nilimnunulia kila kitu vikiwemo hivyo uliyotaja ila sikulalamika.
Shule ya serikali? Na ukadhani ni kawaida? Wewe ndiye wa hovyo....

Kumbuka kuna Text books & Reference books...

Kila shule ni lazima iwe na vitabu vya kiada [Text books] lakini vitabu vya ziada (reference books), mzazi kwa reference zaidi ya mtoto na kwa manufaa ya mtoto wake, anaweza kumnunulia...

Lakini kamwe isiwe kama hitaji sharti la msingi na la lazima ili Mtoto apokelewe shuleni kuanza masomo...!!!

Wewe sijui hata kama unajua hata bei ya vitabu halafu ulinganishe hali ya kiuchumi za wazazi wengi...

Si ndiyo maana mlifuta ada na michango shule za msingi na sekondari O'level...?

Nini mantiki yake kama watoto hawahawa kutoka shule hizi ambako ada na michango iliondolewa ndiyo wanaofaulu kuendelea na masomo kidato cha V & VI katika nyingi ya shule hizohizo...?

Inawezekana hutaweza kujieleza na utasema, oooh wa kwangu alisoma private school na nilimnunulia na kitabu...!!!
 
• Duh! Niseme tu pamoja na kwamba elimu yetu inachangamoto kadha wa kadha ila kusoma sayansi haijawahi kuwa rahisi; ni gharama , kuanzia: muda, pesa, kusoma kwenyewe n.k

• Mwanafunzi kuwa na vitabu vyake ni suala la muhimu, kama uwezo upo. Hii inaleta uwiano mzuri shuleni kati ya idadi ya wanafunzi na vitabu.

• Kuwa na "disection kit" binafsi ni muhimu, mwanafunzi anaweza kuwa anafanya mazoezi peke ake; ukisubiri vya shule atazishika wakati wa mitihani tu au inapokaribia. Kama unauwezo nunua.

• Anaweza kusoma nyumbani kama unaona hivyo ni vyema, atafanya mtihani kama 'private candidate', inawezekana pia.
 
Yeah hata sisi ilikuwa hivo dissection kiti niliuziwa tsh 30 enzi hizo na calculator mbona nilinunua bila kulazimishwa?nina uhakika huyu mzee akisoma comments atajiona bonge la mbwiga,ataukimbia uzi
Never ever, mambwiga ni nyie ambao mnasoma na kumalizia shule hizi ambazo ni zao la siasa uchwara na maji taka na mnadhani mambo yako hivyo.

Nyinyi [mambwiga wengi] hata hamjui kwanini mnalipa kodi serikalini na pengine hamjui hata jukumu la msingi la serikali yoyote duniani, kwamba ni kukusanya kodi na kutoa huduma bora na za kiwango kwa wananchi ikiwemo elimu.

Wewe kweli ni Mbwiga has a maana kama hujui haya, utaweza vipi kudai haki zako? Viongozi watakuwekea makalio yao usoni mwako na utasema sawa tu ni kawaida maana hata baba na mama yangu walikuwa wanawekewa makalio kwenye nyuso zao na DC au Katibu kata!

Kweli hiki ndicho kizazi za shule za kata.
 
• Duh! Niseme tu pamoja na kwamba elimu yetu inachangamoto kadha wa kadha ila kusoma sayansi haijawahi kuwa rahisi; ni gharama , kuanzia: muda, pesa, kusoma kwenyewe n.k

• Mwanafunzi kuwa na vitabu vyake ni suala la muhimu, kama uwezo upo. Hii inaleta uwiano mzuri shuleni kati ya idadi ya wanafunzi na vitabu.

• Kuwa na "disection kit" binafsi ni muhimu, mwanafunzi anaweza kuwa anafanya mazoezi peke ake; ukisubiri vya shule atazishika wakati wa mitihani tu au inapokaribia. Kama unauwezo nunua.

• Anaweza kusoma nyumbani kama unaona hivyo ni vyema, atafanya mtihani kama 'private candidate', inawezekana pia.
Absolutely, YES. Hilo ni muhimu sana pia...

Lakini iwe vya ziada (reference books) na serikali lazima ihakikishe ime - equip shule zake zote na vitabu (Text books) vyote vinavyoendana na syllabus/mitaala yake. Hili wala siyo hisani au option bali ni LAZIMA lifanywe na serikali....!!

Kama mwanafunzi atahitaji cha ziada for her/his extra reference, hapo ni hiari yake anunue...

Kuna watu wengine humu wanajiandikia tu wakiwa hata hawajui jukumu la msingi la serikali, kuwa ni kutoa huduma za kijamii bora na kamilifu kwa watu wake na ndiyo maana inatulazimisha kulipa kodi na sasa tunakwenda kulipa kodi za LUKU na LINE za simu. Tunadhani hizi fedha zinatakiwa kufanya ñini kama si kuhudumia watu...?

Tunapojadili haya mambo ni lazima tuwafikirie na watu wengine wa jamii masikini kabisa ambayo kwao hawana hata uwezo kuinua Abbott - Physics inayouzwa almost 100,000 achilia mbali kulipa ada ya 70,000...!!
 
Hayo ndo matatizo ya kuwa LY. Sasa Kama umeona Elimu ni gharama, jaribu Ujinga. Otherwise mnunulie BS ya Biology, Chand za masomo yote matatu, Nelkon book of Physics kwa kuanzia. Kama huwezi, lala mbele.
Wewe nashindwa hata kukujibu kwa sababu ni wazi hujelewa mantiki ya andiko langu lote. Na hiki unachosema "Elimu ni gharama" na kuwa kama sitaki gharama, nijaribu UJINGA, it's completely irrelevant na mantiki ya hoja yangu...

Anyway, ngoja nikupe tip kidogo kufungua ufahamu wako...

Mada yangu kimantiki inahusu "SHULE ZA SERIKALI" na mapungufu yake...

Wewe umejibu kitu kilicho "out of context" na ni kana kwamba unahalalisha upungufu huu na kuona ni sawa tu...

For your information, mwenzio nimesoma shule bora sana zenye kila kitu na ni za serikali. Labda kwa kwa kuwa ni zile ilizorithi toka kwa wakoloni na zingine ilizotaifishwa toka mashirika ya kidini miaka ya 1970s...

Pia, watoto wangu wamesoma na bado wengine wanaendelea kusoma shule bora za mashirika ya dini zenye kila kitu...

Huo usemi wa "IF YOU THINK EDUCATION IS EXPENSIVE, THEN TRY IGNORANCE" naufahamu maana yake pengine kuliko wewe unavyoelewa. Na haunihusu mimi na wewe tu. Unamhusu kila mtu nchi hii yote na serikali kwa ujumla na maamuzi ktk mipango yake..

Seriously, ninaye mtoto mmoja. Amefaulu vizuri O'Level na kapata nafasi shule za serikali kidato cha 5&6....

Niliona nipunguze gharama kidogo asome shule hizi hizi za serikali...

Nilipotumiwa Joining Instructions, nilichokisoma kikanishangaza na nikaona napeleka mtoto Jehanamu tu. Hiki ndicho kilichonifanya nishee nanyi humu ili tujadili...

Sasa watu badala ya kujadili hoja, wengi ufahamu wao mdogo sana kumbe wa kuelewa mambo kwani badala tujadili hoja, wengi wanaleta mipasho na kujadili mtu....

Nakubali kuwa serikali haiwezi kukamilisha kila kitu kwenye shule zake Mara moja. Lakini mambo ya msingi kama vifaa vya kufundishia na kujifunzia kwa ajili ya ujifunzi wa watoto wetu mashuleni ni lazima iyape first priority....

Naomba tujadili hilo tukihusianisha na jukumu kuu la serikali ktk kutoa huduma kwa wananchi. Achana na hiki ulichokiandika hapa maana hakuna mwananchi ambaye halipi kodi ili kuboresha shule zetu...
 
Never ever, mambwiga ni nyie ambao mnasoma na kumalizia shule hizi ambazo ni zao la siasa uchwara na maji taka na mnadhani mambo yako hivyo...

Nyinyi [mambwiga wengi] hata hamjui kwanini mnalipa kodi serikalini na pengine hamjui hata jukumu la msingi la serikali yoyote duniani, kwamba ni kukusanya kodi na kutoa huduma bora na za kiwango kwa wananchi ikiwemo elimu...

Wewe kweli ni Mbwiga has a maana kama hujui haya, utaweza vipi kudai haki zako? Viongozi watakuwekea makalio yao usoni mwako na utasema sawa tu ni kawaida...!!
• Zamani za kale, miaka ya arobaini na kitu, na miaka ya tisini na kitu
Serikali iliweza kuwapa huduma zote za kijamii wananchi wanazotaka bure, watu walikuuwa wachache na serikali zilimudu.
IMG_20210625_224850_821.jpg


'Serikali itahakikisha itatoa huduma za hakika na bure' kwa zama hizi kauli hii haitekelezeki. Abiria chunga mzigo wako. Isitoshe vifaa husika ni vya mwanafunzi mwenyewe.

Kuna baadhi ya shule zimeelemewa, wanafunzi ni wengi kuliko rasilimali zilizopo. Nimesoma shule za kata; huenda Tabora boys na Kibaha hilo tatizo hakuna, ila mnunnulie kam huwezi mwache akapambane. Fikiria shule labda ina , ina Biology takers 180 alafu BS ziko 50 au 25! Acheni utani nyie, wenye pesa hawapelekagi watoto wao shule hizi zetu; wakiwapeleka hutimiza kisemwacho kwenye 'join instruction'

Anything cheap is expensive
 
Itakua kwa sababu ya korona walimu wanaogopa watoto wasiambukizane korona kila mtoto awe na vifaa vyake.
May be, but I don't think so.

Point na jibu nadhani ni kwa sababu, we have an irresponsible government under CCM.

Pesa nyingi zinaenda na kutumika kwenye mambo ya hovyo badala ya kuzielekeza kwenye huduma za jamii ili hata masikini wale matunda ya Uhuru.
 
Mkuu uzi wako umevamiwa na watoto ambao wanaamini kwenye ujinga na vichwa vyao wamevibeba kama mapambo. Labda tu niwaambie kuwa pesa za umma (serikali) zinapaswa zitumike sehemu kuu tatu pekee.
(1) ELIMU.
 
Back
Top Bottom