Waziri wa Elimu na TAMISEMI, ni sawa Wanafunzi Shule za Serikali kuambiwa waende na dissecting kit na vitabu vya tahasusi?

Waziri wa Elimu na TAMISEMI, ni sawa Wanafunzi Shule za Serikali kuambiwa waende na dissecting kit na vitabu vya tahasusi?

Labda cha kukushauri, vitabu muhimu sana hata kama havijaandikwa kwenye joining instructions isipokuwa kama huna hela angalia kwanza mahitaji ya umuhimu kisha vitu vingine vitafuata kidogokidogo

#A level inabidi uache ubahiri, hapo bado kuna tuition likizo zina gharama, pamphlets zinahitajika na ikiwezekana pesa ya matumizi ya kutosha maana Kula maharage -ugali siku zote za wiki haijakaa vizur

Shule hazina hela, kuna shule inabidi ziingiziwe mil 38 kwa mwez ila inaingia mil chini ya 25 so zina madeni hatar
I totally understand...

Lakini hivi ndivyo mambo haya yanavyopaswa kwenda..?

Tatizo liko wapi?

Je unadhani tatizo ni vipaumbele (priorities) huko serikalini? Au siyo...?

Nimeibua mjadala huu kwa staili hii si kwa sababu yoyote isipokuwa kwa kuwafikiria na kuwasaidia ndugu zetu wengine kutoka familia fukara wasio na uwezo wa kujikakamua kupeleka watoto wao shule binafsi kama tunavyojikakamua sisi wengine...

Huyu kwangu amesoma private school. Kuchaguliwa kwenda shule za serikali kumekuja kwa sbb tunajua hata waliosoma private schools, huchaguliwa shule za serikali kwa masomo ya A'Level Secondary Education...

Ni decision ya mzazi aende huko au aendelee na mkondo wa private. Mimi niliona acha nipumzike kidogo, asome tu ya serikali kwa level hivi kwa sbb ni boarding...

Ile kuona maelekezo haya, ikanitia shaka sana. Kwamba mtoto aende na boksi la vitabu. Ndipo nikaibua mjadala huu kwa staili hii ili wadau wa elimu tujadiliane. Tujue tatizo ni nini? Kama nchi tumejwama wapi? Tufanyeje ili twende kuzuri...?

Kwa hiyo ishu ya gharama kwangu wala siyo tatizo. But why these things in public schools...?.

Asante
 
Tunaelewana kweli? Mjadala hapa ni shule kukosa vitabu kabisa na kuwataka wanafunzi waende na maboksi ya vitabu shuleni...!

Hata hiivyo, vya Tanzania Institute of Education (T.I.E) navyo ni vitabu. Viwepo hivyo hivyo mashuleni kwa wingi. Tatizo hata hivyo pengine havipo kabisa...!

Mapungufu atayaona mwanafunzi (mwanangu) mwenyewe akishafika huko. Yeye ndiye atasema baba/mama nahitaji kitabu cha ziada (reference books) hiki ama kile ili kinisadie na nitanunua (kama uwezo upo)...

Kuna wenye watoto wengine hawana uwezo kabisa wa kutoa hata photocopy achilia mbali kununua vitabu. Wakikuta hivyo shuleni, watatumia hivyo hivyo na watafaulu...
Apa nimekuelewa mzazi
 
Hadi nakuhurumia unavyojitahidi kuwaelewesha hawa viumbe[emoji23] tulia tu kunywa maji ulale it's too complicated! Bongo wajinga wengi mno.

Hapana, tuendelee kujadiliana...

Tunatofautiana upeo, ufahamu na uelewa...

Kila wazo na mchango wa mtu tuuheshimu maana that's how they see things...

Huu ndiyo uhuru wa majadiliano alioukataa Mwendazake John Pombe Magufuli...

Angekuwepo, JF management ingeshaamuriwa kusitisha mjadala kwa sababu unajadili mapungufu ya serikali...!!!
 
Hivi ni nani aliwambia huko. A-Level elimu inatolewa bure?!

Kwanza Elimu Bure siyo sela ya taifa.
Ndiye maana tunauliza kwa sababu hatujawahi kusikia neno kulipa ada zaidi ya elimu bure. Na Kama kuna kulipia ada ni kwa shule zote kwa kutumia mwongozo au ni kila shule ina gharama zake na mwongozo wake.

Embu tufafanulie vizuri.
 
1. Mwanangu amechaguliwa kuendelea na masomo ya kidato cha tano na sita (F. V & VI) mwaka huu 2021 Shule ya Sekondari Nyantakara katika tahususi (Combination) ya Chemistry, Biology & Geography (CBG) iliyoko wilaya ya Biharamulo mkoa wa Kagera. Hii ni shule ya serikali ya Tanzania.

2. Licha ya orodha ya mahitaji mengi anayotakiwa aende nayo mfano; fagio wa kufagilia ndani, sabuni ya maji ya chooni, fagio wa kufagilia nje, ream ya kataratasi nk nk, lipo hili ambalo mimi limeniacha hoi hata kujiuliuza kulikoni hizi shule za serikali? Nimeambiwa nimnunulie mwanangu

[A.] Vitabu yote vya tahasusi (subject combinations) anayokwenda kusoma yaani CBG & Basic Applied Maths

[B.] Dissecting Kit ya somo la Bailojia

3. Nikajiuliza ina maana shule hii anayokwenda kusoma mwanangu haina vitabu? Imekuwaje inaanza kidato cha tano huku ikiwa haina vitabu? Kipi kilipaswa kuanza, majengo au vitabu na walimu kwanza? Hivi mzazi kama nanunua vitabu vyangu kwa ajili ya mwanangu, si bora asomee nyumbani sasa na siku ya mtihani aende kufanya tu...?

4. Nimelileta humu tujadiliane ili tujue majigambo ya serikali kuwa imeboresha elimu Tanzania, yana maana gani kama hali iko hivi ktk shule zake?

4. Naambatanisha na Joining instructions ya shule kwa ajili ya ushahidi na reference zaidi kwa atakayetaka kuthibitisha maelezo yangu.

5. Honestly, baada ya kuipata hii fomu ya maelekezo, nimeanza kusaka fedha tu na kufikiri kumpeleka shule ya binafsi.
View attachment 1829765View attachment 1829766View attachment 1829769
Serikali yetu haiko serious na elimu, shule hazina vitabu/vifaa hata zile shule kongwe zilizokua na vitabu/vifaa leo hazina. Nakushauri umnunulie mwanao vitabu na vitu vingine vitakavyoweza kumsaidia.
Hii serikali haiaminiki sababu haijali ubora wa utoaji wa elimu kwa wanafunzi.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nijuavyo mimi kwa advance inahitaji mtoto walau kuwa na vitabu vya kutosha tena kwa sayansi yahitaji kujiandaa.Lakini kama utaona private ni bora nayo sawa!

Sent from my Nokia 2.4 using JamiiForums mobile app
 
Unajua maana ya "SHULE...?"

Sasa mimi nakuambia leo kuwa huo sio wajibu wa mzazi, ni wajibu wa mwenye shule 100%..

Shule ni mali ya serikali, siyo mali ya mzazi.

In some very special circumstances tu, mzazi naweza kumnunlia mwanangu kitabu fulani for her/his extra reference...
Siasa zimetawala sana kwenye Elimu...
Serikali inatakia kununua vitabu ila hivyo vitabu kuna shule hakuna, kuna muda inabidi mwalimu aingie mfukoni kununua vitabu, ni changamoto sana.
 
Never ever, mambwiga ni nyie ambao mnasoma na kumalizia shule hizi ambazo ni zao la siasa uchwara na maji taka na mnadhani mambo yako hivyo.

Nyinyi [mambwiga wengi] hata hamjui kwanini mnalipa kodi serikalini na pengine hamjui hata jukumu la msingi la serikali yoyote duniani, kwamba ni kukusanya kodi na kutoa huduma bora na za kiwango kwa wananchi ikiwemo elimu.

Wewe kweli ni Mbwiga has a maana kama hujui haya, utaweza vipi kudai haki zako? Viongozi watakuwekea makalio yao usoni mwako na utasema sawa tu ni kawaida maana hata baba na mama yangu walikuwa wanawekewa makalio kwenye nyuso zao na DC au Katibu kata!

Kweli hiki ndicho kizazi za shule za kata.
Pitia comment zote ujione ulivo mbwiga umekuja kutafta kuungwa mkono kwa upuuzi wako?
 
1.Understanding biology yenye visual DVD inauzwa 350,000 ambayo haina DVD inauzwa 80,000
2. Biological science inauzwa 40,000
3. Martin Rowland inauzwa 150,000
CHEMISTRY
1. Ramsden for advanced level inauzwa 50,000
2. Rambert inauzwa 70,000
3. Organic chemistry TIE 15,000
4. In organic chemistry TIE 15,000
5. Chand XI inauzwa 35,000
6. Chand XII inauzwa 35,000
7. Kuna pamplets za akina ngaiza na issue boy

GEOGRAPHY - SIKUSOMA SO SIJUI


Lakini niwaambieni vitabu vya advance ili mwanao akamilike ktk field ya sayansi vinahitaji uwe na takribani 500k ama uwe navyo vichache uwe unagongea shule km wenzako so wabinafsi!
Kwa ufupi kuna haja ya serikali kupitia upya mitaala na kuchagua TEXT &REFERENCE BOOKS zinazohitajika na kuzipeleka kwenye shule zake zote. Maana mjue kuna familia huko vijijini hawana chochote cha kuweza kuwaingizia hata 100,000 kwa mkupuo na wana mtoto, mtoto mpaka adhaminiwe na diwani au kanisa!
WAO WALISOMA BURE NA KULIPIWA NAULI WKT WA NYERERE KWAHIYO WAFANYE HIVYO HIVYO KWA WENGINE
 
1. Mwanangu amechaguliwa kuendelea na masomo ya kidato cha tano na sita (F. V & VI) mwaka huu 2021 Shule ya Sekondari Nyantakara katika tahususi (Combination) ya Chemistry, Biology & Geography (CBG) iliyoko wilaya ya Biharamulo mkoa wa Kagera. Hii ni shule ya serikali ya Tanzania.

2. Licha ya orodha ya mahitaji mengi anayotakiwa aende nayo mfano; fagio wa kufagilia ndani, sabuni ya maji ya chooni, fagio wa kufagilia nje, ream ya kataratasi nk nk, lipo hili ambalo mimi limeniacha hoi hata kujiuliuza kulikoni hizi shule za serikali? Nimeambiwa nimnunulie mwanangu

[A.] Vitabu yote vya tahasusi (subject combinations) anayokwenda kusoma yaani CBG & Basic Applied Maths

[B.] Dissecting Kit ya somo la Bailojia

3. Nikajiuliza ina maana shule hii anayokwenda kusoma mwanangu haina vitabu? Imekuwaje inaanza kidato cha tano huku ikiwa haina vitabu? Kipi kilipaswa kuanza, majengo au vitabu na walimu kwanza? Hivi mzazi kama nanunua vitabu vyangu kwa ajili ya mwanangu, si bora asomee nyumbani sasa na siku ya mtihani aende kufanya tu?

4. Nimelileta humu tujadiliane ili tujue majigambo ya serikali kuwa imeboresha elimu Tanzania, yana maana gani kama hali iko hivi ktk shule zake?

4. Naambatanisha na Joining instructions ya shule kwa ajili ya ushahidi na reference zaidi kwa atakayetaka kuthibitisha maelezo yangu.

5. Honestly, baada ya kuipata hii fomu ya maelekezo, nimeanza kusaka fedha tu na kufikiri kumpeleka shule ya binafsi.
View attachment 1829765View attachment 1829766View attachment 1829769
wale tuliokuwa tuna lala chini mikono juu, incase elimu ya advance ni gharama sana mimi nilikuiwa siend shule miezi miwili, watatu natokea mwezi mmoja nautumia kibaha, mwingine minaki , na mwenge pre medic na mzumbe motto, gharama niliyotumia kwenye tution ni kama nimesoma private tu, kuhusu vifaa hata kwetu vilikuwepo
ingawa ni miaka zaid ya nane nyuma
, ila dawa ya chooni na mifagio hilo jipya
 
Vizuri sana. Hata hivyo...

1. Pamoja na yote haya, sina hakika kama umeelewa "logic" ya mjadala huu niliouanzisha...

2. Lengo langu la kuibua mjadala huu wa kielimu kwa staili hii ni ili kila mtu anayeelewa ajadili na kujibu maswali muhimu kadhaa;

å Kwanini mambo yako hivi?
å Tatizo liko wapi?
å Je, hivi ndivyo mambo yanavyopaswa kuwa?

3. Wewe umejitambulisha kuwa ni mwalimu. Na umejaribu kunielewesha sana, lakini bahati mbaya sijakuelewa kwa sehemu kubwa kwa SBB;.

å Katika maswali matatu hayo hapo juu, umejibu swali moja tu. Umekubali kuwa, haya mambo ndivyo yalivyo, ni kawaida kabisa..
å Umenipa onyo kuwa, mzazi NIKOMAE TU na mwanangu akizubaa ataruka na zero...!!?? Jibu la hili ni rahisi tu. That has never happened before and it will never happen to my children no matter what....!!
å Nisifikiri kuwa napigwa (NAIBIWA) kwa sababu ya kuibua hoja hii. Really? Serious?
å Na mwisho umenitaka niwe na POSITIVE THINKING to teachers and the government at large...

## Kwa hoja zako hizi, ni ushahidi kuwa wala hujaelewa mantiki (logic) ya mjadala huu...

4. Lakini, It's alright. Let me try to be positive about your school, you teachers and the government kama ulivyoshauri kwa sababu that's not a big deal at all...

5. Na sasa baada ya maelezo yako yooote hayo, naomba nijibu kwa ufupi baadhi ya hoja yako na pia nikuachie wewe changamoto kadhaa;

MOSI; IDADI YA WALIMU KUWA NDOGO KULIKO IDADI YA WANAFUNZI:

Maswali kwako:

¶ Ni kosa la nani hili..?
¶ Ni jukumu la nani ku - balance mambo kwa maana ya kutafuta/kuajiri walimu ili kuleta uwiano kati ya walimu na idadi ya wanafunzi?
¶ Hakuna walimu mitaani wasio na ajira?
¶ Kwanini wako mitaani huku shule zikiwa hazina walimu? Unadhani tatizo ni nini?
¶ Unadhani suluhisho la hili ni nini?

PILI; UHABA WA VIFAA VYA KUFUNDISHIA NA KUJIFUNZIA = IKO HIVYO TOKA ZAMANI..

Maswali kwako:

¶ Nani ana wajibu kuhakikisha shule za umma ziko equipped na vifaa vya kufundishia na kujifunzia?
¶ Wewe unadhani kwanini hali iko hivi?
¶ Je wewe kama mwalimu unaijua na kuitambua Sera ya elimu Tanzania?
¶ Unafahamu kuwa katika serikali hata katika maisha ya mtu binafsi kuna kitu kinaitwa "sera na mipango?"
¶ Je, unadhani mambo ndivyo yanavyotakiwa kuwa? Kama jibu lako ni "NDIYO", tuishie hapo tusiendelee na mjadala huu. Lakini kama jibu lako ni " SIVYO" basi twende kazi tuendelee kujadiliana hadi tupate mwafaka...

HIVI NDIVYO ILIVYO TOKA ZAMANI..!!??

Kwanza, naomba nishangae kuwa, kauli hii imetoka kwa mwalimu kitaaluma..!!

å Je, hapa una maana ya kuwa, shule za umma kukosa vifaa vya kujifunzia na kufundishia ndivyo ilivyo toka zamani, ni kawaida hiyo? Au siyo mwalimu?

√• Je, hapa una maana pia kuwà, shule za umma kutokuwa na uwiano sawa kati ya idadi ya walimu na wanafunzi ndivyo ilivyo toka zamani, ni kawaida hiyo? Au siyo mwalimu?

Maswali kwako:

¶ Hii "ndivyo ilivyo toka zamani" ina maana gani?
¶ "Zamani" kwako ni lini kwani?
¶ Wewe ni mwalimu kweli? Una muda gani toka uanze kufundisha? Umesoma shule gani? Kama ni hizi zenye shida hii, basi kumbe NI KAWAIDA..!!

SASA mimi nakuambia hivi ndugu yangu, MAMBO HAYAKO HIVI TOKA ZAMANI...!!

Kuna tatizo la KISERA na KIMIPANGO katika nchi yetu na hii ndiyo imeharibu mambo haya. Hukupaswa ufundishe shule yenye mapungufu haya. Uwingi wa wanafunzi (students/pupils enrollment increment) siyo hoja na kamwe siyo utetezi wa kutetea mapungufu haya...

Nchi yetu kwa maana ya huko serikalini uliko kunakosekana mambo haya na kama yapo basi kuna tatizo la kutojali (negligence);

1. Mipango madhubuti

2. Vipaumbele vya matumizi ya rasrimali fedha

3. Commitment (utashi wa kisiasa)

4. Matumizi mabaya ya fedha za umma kunakotikana na namba 2 hapo juu...
@The Palm Tree ,mkuu umeongelea mengi mazuri sana !!!! Na lawama zote lazma SERIKALI iwajibike tu na lazma serikali iajiri walimu ili watoto wasome kwa usawa zaidi!!!


Na wakati mwingine serikali inakaa kimya ili watoto wengi wafeli zaidi halafu ifurahi yenyewe
 
Usimnunulie vitabu mtoto wako sawa Rafiki yangu mpendwa
Serekali itamnunulia mtoto wako mzuri sana

Kanywe bia tuu
 
We lalama hivo hivo wenzio sa hivi wamakaribia kumaliza topic zote,nikwambie tu kingine wamesahau calculator,Ile ni advanced level sio Olevel na ile ni kombi ya sayansi,sema siku hizi wamedilute sana paper zamani ulikuwa ukileta upuuzi sayansi unazungusha au unapata matokeo ya hovyo

Hata shule kongwe hazina kila kitu sembuse hizo za juzi?kingine kwa advance kombi za sayansi zina vitabu vingi mno huwezi tumia kitabu kimoja kwa maana shule inavitabu vyake lakini na wewe lazima uongeze vya kwako

Mzazi be positive hayo ni maisha ya mwanao otherwise useme hauna uwezo aende akaunge unge,au ukiona serikali wanazengua unaweza mpeleka private

Kama unaona elimu ni ghari,jaribu ujinga
Kodi anazolipa mzazi ikiwemo tozo za miamala zinaenda wapi ?
 
Back
Top Bottom