Unaweka msimamo wako tu watauelewa.Hivi hizi shule za serikali na private unajua jinsi wanavyotuchukilia wazazi. Yani ukimchukuwa mwanao Mfano private unaweza kuambiwa umuhamishe moja kwa moja au akirudi atasakwamwa haswa.
Hakuna shule inayo fundisho wakati wa likizo masaa 12 .Uliona wapi mtoto wa miaka kumi anasoma masaa kumi na mbili kwa siku kwa muda wa mwaka mzima?
Ushahidi upo nenda pale Anzazak au Right way ,watoto wanapigishwa kwata hadi saa tatu usiku na bado wanapewa homework .Hivi huyu mtoto anapumzika saa ngapi?Hakuna shule inayo fundisho wakati wa likizo masaa 12 .
wakati wa likizo mwisho saa 6 au 9 tu .
Ndio wakati wa mavuno,wanapolazimisha watoto kulala shuleni wanaongeza na ada piaWalimu wenyewe wanasemaje
Hapa ameshauri hakutoa amri .....kama una shida mtoe mwanao kimyaHii tabia ya watendaji wa Elimu kutotii maagizo ya boss wao either ni ishara ya dharau au ni kushindwa kutii maagizo kwa makusudi. Sisi wazazi tunasubiri watoto wetu kurejea nyumbani alafu wanatokea maafisa Elimu na wakuu wa dhule wasio na nidhamu kwa maboss wao kwa makusudi wanaamua kuwakatalia watoto wetu shuleni.
Hizi shule za binafsi Wana sababu Mfu kuwa watoto wakirudi nyumbani et huwa wanazurura tu. Hii ni dhana ya hovyo kabisa maana wazaz wengine husubiri watoto warudi likizo ili wafundishwe maadili ya kifamilia na kijamii kulingana na ukuaji wao wa akili na mwili.
Wanadai kuwa wazazi huwa wanaridhia. Sio kweli bali wazazi hupewa tu taarifa ya mipango Yao na pale wazazi tunapoitwa huwa km ni kupokea tu agizo kutoka kwa uongozi wa shule. Na km wanaona wakija likizo watazurura basi wawe wanawapatia assignments ili wafanye wawapo makwao. Kinyume na hapo si tu kuwa wanawafanyia watoto ukatili wa kiakili bali wanatunyanyasa wazazi kwa kukosa fursa ya kukaa na kuongea na watoto wetu kadri ya mabadiliko ya miili yao.
Hivi Wizara wakati wanaweka mihula hawa wanaokaidi wanadhani wao walikuwa wajinga. Hakuna elimu Wala kazi isiyo na mapumziko. Hata hao Walimu wanahitaji kupumzika, siyo maroboti. Inafikia wakati watoto wengine wanaenda shule kabla ya kuvunja ungo, wanakaa huko hadi wanavunja ungo na hatimae kukosa taulo za kike.
Hii hali inakera sn, ebu Waziri wa Elimu tumia kipaza sauti ili tuone wapi panavuja.
Kabisa ndugu ,mimi ninae wa darasa la sita nimemwamisha baada ya kuona mateso aliyopata dada yake,Mi hilo swala nitalipinga daima, nitapeleka mtoto shule ambayo hawafanyi huo upumbavu
Mtoto anahitaji malezi yako pia. Unapoishi naye unamjua mtoto wako, changamoto anazopitia na kuona jinsi ya kumsaidiaKamchue mwanao hawatakuzuia. Mimi wangu atabaki shule!
Mimi ni mwalimu....sipendi kubaki kazini wakati wa likizo ila basi tu ni vile kuna kulazimishwa. Shule ya sekondari ninayofundisha watoto wanarudi shule tarehe 19/7 ....sitaenda. Nitaomba ruhusa ya aina yoyoye hata kwa kusingizia chochote.Walimu wenyewe wanasemaje
Ni kweli kabisa mkuu!Mtoto anahitaji malezi yako pia. Unapoishi naye unamjua mtoto wako, changamoto anazopitia na kuona jinsi ya kumsaidia
Watoto wanakabili mambo mengi sana wakiwa shuleni tenga muda wa kujua nini anakabil uone jinsi ya kumsaidia
Tumia kipindi cha likizo kuwajenga na kufurahia na watoto wako. Usikimbie majukumu yako
Wazazi tunafeli sana hapa
Ni kweli kabisa mkuu uyasemayo. Mimi nina mtoto wangu kidato cha nne ni bora zaidi abaki shule kuliko nyumbani. Mimi kama mzazi nikitoka asubuhi kwenda kazini narudi jioni, itakuwa kuwa ngumu kujua nini anafanya ndani ya masaa hayo 12.(mimi na mama yake tunatoka asubuhi na kurudia jioni).Mtoto anahitaji malezi yako pia. Unapoishi naye unamjua mtoto wako, changamoto anazopitia na kuona jinsi ya kumsaidia
Watoto wanakabili mambo mengi sana wakiwa shuleni tenga muda wa kujua nini anakabil uone jinsi ya kumsaidia
Tumia kipindi cha likizo kuwajenga na kufurahia na watoto wako. Usikimbie majukumu yako
Wazazi tunafeli sana hapa
Itakuwa wazazi wamegoma kuchangia na wakati huo huo wana wapeleka watoto tuition.Huku kwetu sek zote za gv zmefngwa
Ujue ni kwa vile siyo wazazi wote ni Walimu au wana wanafunzi huko. Ila ukweli hali ni tete sn, hasa shule za serikali. Yani unakuta kidato cha nne wanabakizwa ilihali shule siyo za bweni. Watoto wanarundikwa madarasani eti wanaita kambi. Humo madarasani wanarundikana km nzige huku wakilala chini kwenye mikeka wengine wenye uwezo wazazi wanawanunulia vigodoro vidogo. Hapo sasa unadhani ushoga utaisha vipi. Kuna watu humu sababu ya ukosefu wa taarifa ya yanayoendelea huko wao wanaona kubakiza watoto shule sawa tu.Itakuwa wazazi wamegoma kuchangia na wakati huo huo wana wapeleka watoto tuition.
This are Tanzanians I know.
Aliko mdogo wangu halmashauri Y,shule anapofundisha huwa mara wanafunzi waingiapo kidato cha nne,pamoja na michango mingine ya kambi,ni lazima kuchangia 10K kwa ajili ya walimu watakao hiyari kuwafundisha kipindi cha likizo (June) na wakusanyaji ni wazazi wenyewe na kamati zao.
Sasa kabla ya kufunga dogo akaniambia hatokuja likizo kwani atabaki akifundisha kidato cha nne na cha pili (hawa huchangia 5000) kwa makubaliano ya wazazi. Akasema mwl wa Physics ni yy tu shule nzima hivyo walau awasogeze ukizingatia kuwa hivi vidato ratiba yao ya kusoma ni finyu sana kutokana na msululu wa mitihani inayo wakabili ya wilaya na mkoa.
Sasa juzi mara dogo huyu hapa,vp tena?
Akasema serikali imeagiza wanafunzi wakapumzike hivyo chapu nami nikatumia huo mwanya.
Jumatatu,jumanne,Mkuu wake akawatumia ujumbe kwenye kundi lao la WhatsApp la shule ujumbe unaonekana ni kutoka kwa Afisa elimu mkoa au wilaya ukiwataka waende wakafundishe eti wamepokea maelekezo kutoka ngazi za juu.
Kilicho nifanya nione ni kuna upuuzi mwingi kwenye elimu yetu,kwenye ujumbe huo kuna kipande kinasomeka hivi (tunawaomba radhi wazazi na wanafunzi kwa mkanganyiko uliojitokeza).
Sasa nikawaza,ni kwa nini mwl hakuombwa radhi?
Kwamba walimu ni wajibu wao kufundisha kipindi cha likizo au wanajitolea ili kuwasaidia hawa watoto?
Ni shule ya kata iko kijijini ambapo source of informations ni mwl, tuition ni msamiati mgumu sana. Lkn ndo hivyo,dogo ana ratiba zake wala hakujibu na sidhani km kuna mwl ataenda tena.
Hii ni battle kati ya wanaosomesha st Kayumba na wanaoenda kwa yellow buses shule,hawa wa kundi la kwanza wana danganywa na wa kundi la pili.
Kwakuwa wengi wao hazimo basi wana amini wako pamoja,kumbe wa kundi la pili wanachukua pointi 3.
Ni kweli aache kelele.ahamishe mtoto wake ampeleke kwingine hawatamkataliaKamchue mwanao hawatakuzuia. Mimi wangu atabaki shule!
Shida iko wapi kwani? Kazi ya mwalimu ni.kufunza mtoto kasomea ufunzaji watoto wazazi wengi hawajasomea jinzi ya kufunza mtoto walimu wana hadi digrii za kufunza watoto wazazi wengi hawana hsta certificate ya.kufunza watotoNa wewe ni miongoni mwa wazazi wenye watoto watukutu unaona kukaa naye nyumbani ni kero umeamua kuwasukimizia Walimu!!
Ni kweli aache kelele.ahamishe mtoto wake ampeleke kwingine hawatamkatalia
Ni kuhakikishie tu ndugu yangu, Walimu wa leo siyo Walimu wa jana na watoto wa leo siyo watoto wa jana. Kwa sasa Walimu % kubwa hawaangaiki na malezi ya watoto wanachojali ni ajira zao tu. Km hutaniamini basi utakuwa hutaki kuamini kwa makusudi huku ukijua. Unadhani wao wajinga Kila sku wananyooshewa vidole kuwa wanapiga wanafunzi hovyo, wazazi wamekuwa maadui na Walimu. Wewe ni shahidi hadi wengine huja humu kuwatukana. Sasa km una mtoto serikalini habari ndiyo hiyo, km yupo private angalau huko bado pazuri kiasi hasa shule za dini.Shida iko wapi kwani? Kaxi ya mwalimu ni.kufunnza mtoto kasomea ufunzaji watoto wazazi wengi hawajasomea jindi ya kugunzs mtoto walimu wana hadi digrii za kufunza watoto wazszi wengi hawana hsta certificate ya.kufunza watoto
Kisarawe Secondary na Msingi wamegoma kufunga.Huku kwetu sek zote za gv zmefngwa