Huku kwetu sek zote za gv zmefngwa
Itakuwa wazazi wamegoma kuchangia na wakati huo huo wana wapeleka watoto tuition.
This are Tanzanians I know.
Aliko mdogo wangu halmashauri Y,shule anapofundisha huwa mara wanafunzi waingiapo kidato cha nne,pamoja na michango mingine ya kambi,ni lazima kuchangia 10K kwa ajili ya walimu watakao hiyari kuwafundisha kipindi cha likizo (June) na wakusanyaji ni wazazi wenyewe na kamati zao.
Sasa kabla ya kufunga dogo akaniambia hatokuja likizo kwani atabaki akifundisha kidato cha nne na cha pili (hawa huchangia 5000) kwa makubaliano ya wazazi. Akasema mwl wa Physics ni yy tu shule nzima hivyo walau awasogeze ukizingatia kuwa hivi vidato ratiba yao ya kusoma ni finyu sana kutokana na msululu wa mitihani inayo wakabili ya wilaya na mkoa.
Sasa juzi mara dogo huyu hapa,vp tena?
Akasema serikali imeagiza wanafunzi wakapumzike hivyo chapu nami nikatumia huo mwanya.
Jumatatu,jumanne,Mkuu wake akawatumia ujumbe kwenye kundi lao la WhatsApp la shule ujumbe unaonekana ni kutoka kwa Afisa elimu mkoa au wilaya ukiwataka waende wakafundishe eti wamepokea maelekezo kutoka ngazi za juu.
Kilicho nifanya nione ni kuna upuuzi mwingi kwenye elimu yetu,kwenye ujumbe huo kuna kipande kinasomeka hivi (tunawaomba radhi wazazi na wanafunzi kwa mkanganyiko uliojitokeza).
Sasa nikawaza,ni kwa nini mwl hakuombwa radhi?
Kwamba walimu ni wajibu wao kufundisha kipindi cha likizo au wanajitolea ili kuwasaidia hawa watoto?
Ni shule ya kata iko kijijini ambapo source of informations ni mwl, tuition ni msamiati mgumu sana. Lkn ndo hivyo,dogo ana ratiba zake wala hakujibu na sidhani km kuna mwl ataenda tena.
Hii ni battle kati ya wanaosomesha st Kayumba na wanaoenda kwa yellow buses shule,hawa wa kundi la kwanza wana danganywa na wa kundi la pili.
Kwakuwa wengi wao hazimo basi wana amini wako pamoja,kumbe wa kundi la pili wanachukua pointi 3.