Kila Ijumaa wazazi tunadaiwa shs 1,500 kama ada ya mtihani. Je walimu wanafanya haya kwa ruhusa ya Wizara kama examination policy?
Mtoto asipoleta hela anapigwa. Tupelekane mahakamani na walimu wako kwa kuwapiga watoto bila sababu? Kama mtoto hakupewa hela, unampiga ili hela aitoe wapi?
Au Ni miradi ya waalimu kujiongezea kipato?
Wazazi watashindwa
Nitakupa ushahidi kama ukihitaji uthibitisho
Soma :
Ndugu mtoa mada hebu amka katika huo usingizi mzito na pumbazo ulilo nalo.
Hakuna kitu kinaitwa elimu bure hata iwaje.
Ni nyinyi ndio wa kwanza kuhoji matokeo iwapo watoto hawafanyi vema matokeo yanapoachiliwa.
Hivyo ili kuwajengea uwezo watoto: walimu waliona mitihani ya mara kwa mara inaweza ikawajengea uwezo.
Je hapo gharama za hiyo mitihani ambayo ni kwa manufaa ya watoto wenu nani anabeba? Hao walimu wapate TB ya chaki kwa sababu ya kuandika mitihani ubaoni?
Ukiangalia hiyo mitihani inafanyika weekend (nje ya ratiba ya muajiri) hivyo hao walimu wanaacha familia zao hata weekend kuwajengea uwezo watoto wenu na bado hamna shukurani hata kwa muda wao wanaowekeza kwa watoto wenu.
Mnahoji 1500/= ya mitihani ya watoto ila hamuhoji 5000/= sijui 10,000/= ya kumuona tu daktari nje ya vipimo.
Ifikie hatua mthamini na jitihada za za walimu na taaluma yao kama mnavyowathamini na kuwaheshimu madaktari au wanasheria na mihuri yao. Hii ni kwa matokeo ya watoto wenu.
Ila upande mwingine kwa wale walimu wanaoadhibu watoto kwa kukosa pesa ya kulipia mtihani wanakosea kwa kuwa mtoto hana chanzo cha mapato ni mtegemezi. Hivyo watumie busara katika hilo.
Mzazi pia kama hauridhii hii mitihani hiyo onana na uongozi wa shule liweke bayana ili mwanao akae kando na hata akifanya vibaya usihoji na pia ujicommit kimaandishi kwa uongozi wa shule ili hapo baadae wanapohojiwa ionekane kabisa kuwa nini sehemu ya chanzo ya hayo matokeo.
Kumbuka pindi hayo matokeo yanapotoka wanakumbana na kashkash nyingi sana za mamlaka juu ya matokeo.