Waziri wa Elimu tunaomba utusaidie walimu DIT hatujalipwa tangu Juni

Nadhani tatizo lililopo DIT ni la kimfumo zaidi maana vitu vingi vinafanyika kienyeji sana kama vile hamna uongozi. Hata hili la malipo uongozi unajua ndio ushangae ila nadhani wapo bize na mambo yao kwanza maslahi ya chuo wanaweka kando
 
Ukiwauliza wanasemaje??
Danadana tu, mara deparc hajasaini, mara ipo uhasibu, mara sijui nani kasafiri... na cha kusikitisha sio mara moja kila semester shida ni hiihii. Wanatudharau sana hadi vijana wadogo ofisi ya uhasibu wanakujibu mbovu, nakumbuka kuna siku niliambiwa nikaulize kwa mhasibu akanambia malipo ya kulipwa yapo mengi nikashangaa sana. Uache kulipa mshahara kwanza ufanye mambo mengine utegemee niingie darasani bila stress? Hata malaika hawezi, nilijiondokea zangu nikaacha wanafunzi wanasubiri darasani.
 
Mkuu, katika vitu ambazo sitakagi mchezo ni kwayeyote anae chezea ama kudharau kazi yangu.
Na bora muhindi ndio angekua anatufanyia hivi... Sasa chuo tena cha serikali kabisa na hadi mkuu wa chuo anafahamu vizuri haya malalamiko yetu maana si ya leo wala jana, ni vile kutoweka maslahi ya chuo mbele tu wao kila siku safari wanakula perdiem hawajui machungu ya kukosa mshahara hata wa mwez mmoja
 
Nakupa wiki mbili mkuu wa chuo anastaafishwa, muda mrefu alikua anatafutiwa angle ya kupigwa chini, anayemkingia kifua pale wizarani kashapigwa chini, next ni yeye.
 
Nakupa wiki mbili mkuu wa chuo anastaafishwa, muda mrefu alikua anatafutiwa angle ya kupigwa chini, anayemkingia kifua pale wizarani kashapigwa chini, next ni yeye.
Kwakweli huwa sifurahii anguko la mtu ila kwa huyu aisee binafsi nimeteseka sana kisaikolojia maana hakuna hata mara moja tumelipwa bila kusumbuliwa vibaya mno utafikiri machokoraa. Na iwe hivyo akapumzike waje wengine wanaoweza kujali maslahi ya chuo.
 
Nakupa wiki mbili mkuu wa chuo anastaafishwa, muda mrefu alikua anatafutiwa angle ya kupigwa chini, anayemkingia kifua pale wizarani kashapigwa chini, next ni yeye.
Kwa Hilo unasema kweli maana mkulu Yuko huku. Ila Dada joy Hana ujanja wa kujoin fb. Bado Yuko tuition ya kiarabu akimaliza ndio kiingereza
 
Mbona haki yako ya kulinda kura zisiibiwe ulishindwa kuitetea? Lisu aliibiwa Kura waziwazi na sasa una rais bogus kuwahi kutokea duniani asiyejua kingereza yeye anajua kudefine catalyst tu.
 
Kwa Hilo unasema kweli maana mkulu Yuko huku. Ila Dada joy Hana ujanja wa kujoin fb. Bado Yuko tuition ya kiarabu akimaliza ndio kiingereza
Dada joy afikishiwe tu ujumbe kuhusu huyu mtendaji wake maana alimteua yeye, vinginevyo yatamfika mwenyewe sababu huyu mtendaji wake mara nyingi tu analalamikiwa.
 
Dada joy afikishiwe tu ujumbe kuhusu huyu mtendaji wake maana alimteua yeye, vinginevyo yatamfika mwenyewe sababu huyu mtendaji wake mara nyingi tu analalamikiwa.
Dada joy huogopa kuchukua maamuzi ili kuficha udhaifu wake kwa mkulu na si vinginevyo, madudu yote yanayotendeka DIT anayaelewa kitambo.
 
Mbona haki yako ya kulinda kura zisiibiwe ulishindwa kuitetea? Lisu aliibiwa Kura waziwazi na sasa una rais bogus kuwahi kutokea duniani asiyejua kingereza yeye anajua kudefine catalyst tu.
Yaani wejamaa ndio kiazi kweli aiseeee, mimi sio mwanasiasa na sishabikii siasa and kwangu kupiga kura sio kitu cha lazima kabisa.
Kwaufupi naona kama unataka kunikazimisha ninye alafu nikurushie mavi, Jambo ambalo kwangu sioni Kama ni busara.
By the way, huyo lisu unaemzungunzia ndio nani?? Huyo lisu na john ndio watanilishia familia na kunisomeshea wanangu??
Ngoja nikupe tu pole kwa kudhani kwamba Lisu ama John watakuja wayabadikishe maisha yako.
Leo mifano haintumeiona:-
1. John yupo ikulu bara
2. Seif yupo ikulu nzanzibar.
3. Lisu yupo ulaya.
4. Lema yupo Canada.
5. Membe ametulia anakula pension.
6. Mdee na wenzake wapo bungeni.
Lakini wale wote walio wapigania wengi walipoteza maisha na familia zao zinahangaika, wengine walipata ulemavu na majeraha, na wengine wapo mahabusu na wanakesi na jamuhuri.
 
Yaani we ndo kiazi kweli. Hujui nguvu ya siasa kuwa ukibugi kiongozi unaweza kuwa na maisha mazuri au la? Siasa ndo maisha dogo. Hata shati Hilo ulilovaa ni matokeo ya siasa. Hata make uliyenaye ni matokeo ya siasa la sivyo usingemuoa angeshakuwa mkombozi wa kiuchumi. Hata kusali ni matokeo ya siasa. Hata baba yako au mama yako ni matokeo ya siasa. Hata ku.to.mba ni siasa na kuongea ni siasa pia. So siasa is inkwepable.
 
Usinilazimishe nimpende lisu mkuu, ebu kapambaneni na hali zenu maana mimi nipo busy kupambana na familia yangu aisee
 
Hivi yule jamaa bonge bado yupo?
Unalalamika huku wakati pesa wanazo wanafunzi, vujisha test hizo acha kulialia! Wakiume wakupe hela na mademu kula ..full batani! Lakini hivi si muache mukajiajili si mnafundisha ujasiliamali
Kwa huu upuuzi wanaotufanyia hakyanani unaweza fanya hayo maamuzi aisee toka june hadi leo wasilipe hata ya mwezi mmoja kweli? Labda hadi siku tuwaharibie afu serikali nzima itie kambi pale ndio wataanza kutuheshim.
 
Hapana nadhan ambao hawafundishi vizur sio wa part time , hata ukiuliza wanafunzi watakwambia part timers ndo tunaookoa jahazi pale japo kulipwa ndio mpaka wakose cha kufanyia na pesa zao....ila ipo siku tutawaadabisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…