Waziri wa Elimu tunaomba utusaidie walimu DIT hatujalipwa tangu Juni

Waziri wa Elimu tunaomba utusaidie walimu DIT hatujalipwa tangu Juni

Uchumikati

Member
Joined
Dec 8, 2020
Posts
82
Reaction score
97
Sisi walimu wa Chuo cha Serikali cha DIT tunaofanya part time tunaomba utusaidie tulipwe mishahara yetu tunayodai tangu mwezi June na sasa ni December na hatuoni dalili za kulipwa.

Kwakweli ni tatizo la muda mrefu ambalo hakuna anaeonekana kujali sio mkuu wa chuo wala nani maana semester inaisha bila kulipwa hata mia na wanafunzi wanaenda likizo hadi miezi mitatu bado hawaprocess malipo hadi semester nyingine inaanza bado hawalipi na masomo yanatakiwa yafundishwe.

Hapo kuna kutoa elimu bora kweli mtu kila siku unatumia nauli yako miezi 6 usilipwe ni uungwana kweli? Tunakuomba utusaidie mheshimiwa waziri tunateseka na watu tunafamilia na madeni lukuki yenye riba umiza zinazotokana na kucheleweshewa malipo bila sababu za msingi.

Vyuo vimeshafungua wanafunzi wameshalipa ada lakini bado hatulipwi kama walivyoahidi kwamba hadi wakusanye ada. Hatupendi kuingia mitandaoni kuandika ila tunalazimika kutokana na uzembe wa watu wachache.

UPDATES
Mwezi December ndio unaisha hivyo tunaelekea mwaka mwingine na hatujalipwa toka June, waziri Ndalichako unataka mpaka walimu tuanze kuuza mitihani ili kujikimu na familia zetu haLafu ndio muanze kutafuta mchawi?
 
Mungu alinipa moyo wa ajabu sana, na ninavyo ona mimi watu wengi wanakosa haki zao za msingi kwasababu ya hofu na mashaka, na pia kutokujiamini

Mimi sijawai kuhofia kudai haki yangu popote hata kwa yeyote. Kumbuka hiyo ni haki yenu na mnatakiwa kumuandikia barua mkuu wa chuo na copy kwa mtu wa juu yake (yaani msiruke ngazi)

Tena mnapaswa kujieleza kwa ufasaha pamoja na kuahinisha Jambo lenu, na hakikisheni mnaandika majina yenu/lako ili usionekane kama mnaweka majungu tena kwa kujificha.
 
Eti na DIT kinazalisha ma engineer.

Wamepewa mradi wa kuweka mfumo wa kutumia gesi kwenye magari wanakenua tu. Magari tz yako mengi sana Ila wazee wa DIT wameshindwa kabisa kujiongeza.

Fungueni gereji mpaka mikoani.
Tangu awamu ya JK ni Ubungo Ubungo Ubungo. Kama mmezeeka waachieni vijana ofisi.
 
Eti na DIT kinazalisha ma engineer.
Wamepewa mradi wa kuweka mfumo wa kutumia gesi kwenye magari wanakenua tu. Magari tz yako mengi sana Ila wazee wa DIT wameshindwa kabisa kujiongeza.
Fungueni gereji mpaka mikoani.
Tangu awamu ya JK Ni Ubungo Ubungo Ubungo. Kama mmezeheka waachieni vijana ofisi.
Dokta NYARI yupo anakusikia
 
Mkuu, katika vitu ambazo sitakagi mchezo ni kwayeyote anae chezea ama kudharau kazi yangu.
Hii hali ukiizidisha sana inapelekea kufanya mambo ndivyo sivyo, wakati mwingine unaweza kuwa na matatizo yakisaikolojia, kwamba kila jambo wewe unaona hutendewi haki, punguza panick uwe na kiasi ili uruhusu uhuru akili yako ndio aimue na si jazba ama kutaka watu wakuone kwamba wewe ni mtata.

Yote kwa yote DIT wajirekebishe kwenye hili.
 
Sisi walimu wa Chuo cha Serikali cha DIT tunaofanya part time tunaomba utusaidie tulipwe mishahara yetu tunayodai tangu mwezi June na sasa ni December na hatuoni dalili za kulipwa

Kwakweli ni tatizo la muda mrefu ambalo hakuna anaeonekana kujali sio mkuu wa chuo wala nani maana semester inaisha bila kulipwa hata mia na wanafunzi wanaenda likizo hadi miezi mitatu bado hawaprocess malipo hadi semester nyingine inaanza bado hawalipi na masomo yanatakiwa yafundishwe

Hapo kuna kutoa elimu bora kweli mtu kila siku unatumia nauli yako miezi 6 usilipwe ni uungwana kweli? Tunakuomba utusaidie mheshimiwa waziri tunateseka na watu tunafamilia na madeni lukuki yenye riba umiza zinazotokana na kucheleweshewa malipo bila sababu za msingi

Vyuo vimeshafungua wanafunzi wameshalipa ada lakini bado hatulipwi kama walivyoahidi kwamba hadi wakusanye ada. Hatupendi kuingia mitandaoni kuandika ila tunalazimika kutokana na uzembe wa watu wachache
Kumbe ndo maana hamfundishi vizuri? Na ndugu yangu kahama chuo kisa anasema walimu hawaeleweki...

Sasa ndugu yangu nakushauri acha hiyo kazi toka kwenye comfort zone yako nenda katafute namna ya kujiajiri.. usiulize utapata wapi mtaji mbona umeweza kuishi miez sita bila mshahara na kila siku unafika kazini na kurudi?

Huwezi kujua wewe ni jasiri kiasi gan kama utaendelea kulalamika hapo

Wengi tuliojiajiri ni kwasabu tulilazimika na hatukuanza na mtaji ila tulianza na wazo
Toka nje ukakomae achana na ajira ya mkataba utatoboa tu!

Mkiamua kuungana hapo mnapata kabisa kampuni na mnaanza kazi..
 
Back
Top Bottom