Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo avikumbusha vyombo vya habari kuwa kutumia uvumi kama habari rasmi ni kukiuka sheria

Baraza zima la mawaziri limegeuzwa kuwa madispline masters wa zile shule za boarding za miaka ya 90

Wao kila kukicha wanakuja kutuonya kana kwamba sisi ni watoto wao
 
I cement that kabisaaaa maana watu wamekalia umbea tuuu , oo flani anaumwa ooh flani kafa , turudi kwenye misingi yetu ya zamani ya utu ifike mahali usifurahie mwenzio akipata matatizo hata kama ni kweli. Enzi za mwalimu haikuwa hivi tubadilike
Waliokuwa wanaona Lissu kuuawa ni Sawa tu, leo wanawafundisha wenzao kuwa na utu!?

Aisee!!
 
Ni upuuzi.

Tuna viongozi wa ajabu awamu hii, wanaoamini kuwa wamepewa haki ya kufikiri kwa niaba ya wote, kutafiti,, na kunena kwa niaba ya wengine.

They think they know everything better than others, what they are missing is to admit to the fact that the intelligent citizens are outside their ignorance circle.

Vyombo vya habari vina haki ya kutafuta habari, kuchunguza na kutangaza. Anaposema watangaze habari zinazotolewa na vyombo rasmi, anamaanisha nini? Hivi kama kuna jambo linanihusu mimi, chombo cha habari kikanihoji mimi, nami nikathibitisha, kutangaza mpaka akapate ruhusa ya serikali? Huo ni ujinga wa hali ya juu.

Msiingilie uhuru wa vyombo vya habari wala uhuru wa maoni wa raia.

Zile semina elekezi zilikuwa muhimu sana kwa wateule ili waweze kujua mipaka ya mamlaka yao, siyo kupayuka dhidi ya kila jambo.
 
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Innocent Bashungwa ametoa wito kwa vyombo vya habari kuendelea kutoa taarifa zinazotolewa kwenye vyanzo rasmi na kuepuka kutumia uvumi/rumours...
Kama wanataka kuepusha habari za uvumi, basi wawe wanatoa taarifa sahihi kwa wakati. Tumezoea kila jumapili tunaambiwa rais kasali kigango fulani, na tumezoea kila siku rais yuko font fend ya magazeti, lakini hii ni wiki ya pili hatujui rais yuko wapi sasa kwanini kusiwe na rumours?
 
Hivi Uvumi sio habari? (Kuhabarisha watu kwamba kuna Uvumi fulani). Yaani ukisema kuna uvumi unasema ABCD, ila kwa tulivyofuatilia hatukupewa majibu au tumegundua kwamba ni EFGH...

Sababu kukaa kimya kuhusu uvumi ni mbaya zaidi na pia kama vyombo vya habari vikienda kuhakiki uvumi kwa wahusika vikalishwa matango pori, vifanye nini? viwalishe pia wananchi matango pori eti tu sababu hayo matango yametoka kwenye vyanzo vinavyohusika?

Mfano suala la kuwepo au kutokuwepo kwa Changamoto za Upumuaji hivi vyombo vingeendelea kusema hakuna changamoto kumbe huenda ata mdau mwenyewe anayetoa hizo habari amepona tu changamoto juzi kati...
 
I cement that kabisaaaa maana watu wamekalia umbea tuuu , oo flani anaumwa ooh flani kafa, turudi kwenye misingi yetu ya zamani ya utu ifike mahali usifurahie mwenzio akipata matatizo hata kama ni kweli. Enzi za mwalimu haikuwa hivi tubadilike.
Mtenda hutendwa...

Akutendae mtende Mche aso kutenda..
 
Ni habari gani hiyo imetolewa kwa mtindo wa uvumi?

Kama ni ile inayovuma sasa mtandaoni tangu jana hivi, waje tu waseme ni kweli au si kweli yaishe.
 
I cement that kabisaaaa maana watu wamekalia umbea tuuu , oo flani anaumwa ooh flani kafa , turudi kwenye misingi yetu ya zamani ya utu ifike mahali usifurahie mwenzio akipata matatizo hata kama ni kweli. Enzi za mwalimu haikuwa hivi tubadilike
Utu huzaa utu. Na kinyume chake ni kweli pia.
 
Wazungu wana kama kamsemo kao 'Silence means consent'.
Wanapokaa kimya bila kutoa kauli yeyote kuhusiana na 'uvumi' huu basi kunaamaanisha wameridhia habari hiyo hivyo itachukuliwa kuwa ni kweli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…