Waziri wa Katiba na Sheria Mwigulu Nchemba awajibu TLS kuhusu Rais Samia Suluhu kuteua Baraza jipya la Mawaziri

Angeongezea pale tuzingatie mabarakoa kwenye kuomboleza yeye kama Daktari wa binadamu angekuwa kakomelea zaidi.

Ni muhimu sana kelele zipigwe kuhusiana na ugonjwa huu unaoouwa watu.

Vinginevyo baada ya msiba huu kuna mingine.

Eeh mola wetu utupe hekima ya kusoma nyakati.
Unasubiri tangazo la nyungu?
 
Hili jambo linatakiwa lijadiliwe na watu wenye upeo na akili. Siyo size ya Mwingulu. Yeye abaki na vitu vya kiwango cha chini.
 
Majinga mengi hayatamwelewa mwigulu! Yapo mengi yanavizia vyeo sahivi hata hayajui sahivi kuna tukio gani
 
Mwenzake ametoa vifungu vya katiba,Mwiguli ni kama ametumia busara zake zaidi na siyo sheria.busara ni nzuri lakini kufuata matakwa ya katiba ndiyo jambo la mhimu zaidi
Ni wapi katiba imesema raisi akifariki dunia,makamu wa Raisi atakayeapishwa kuwa Raisi inabidi aunde baraza lake la mawaziri?
 
Mwigulu yuko sahihi katika hili,tuache ubabaishaji
Yuko sawa kivipi? hao mawaziri walikula kiapo kwa rais wa zamani,hapo lazima baraza liundwe upya kulingana na katiba mwigulu analinda ugali tu.hata waziri akibadilishiwa wizara anarudi kula kiapo kwa rais yuleyule itakuwa kwenye mabadiliko ya rais,kama baraza lipo Ni mwendelezo wa kuvunja katiba.
 
Yuko sawa kivipi? hao mawaziri walikula kiapo kwa rais wa zamani,hapo lazima baraza liundwe upya kulingana na katiba mwigulu analinda ugali tu.hata waziri akibadilishiwa wizara anarudi kula kiapo kwa rais yuleyule itakuwa kwenye mabadiliko ya rais,kama baraza lipo Ni mwendelezo wa kuvunja katiba.
Ni wapi katiba imesema raisi akifariki dunia,makamu wa Raisi atakayeapishwa kuwa Raisi inabidi aunde baraza lake la mawaziri?
 
Huyu ni Kati ya Watu Mamafia chama inawalea! Ana Rangi nyeupe ila Roho nyeusi imejaa imejaa Unyama!!Rejea alivokua minister wa Enterior affairs!! Huyu Mama Samia amtupe mbali akachunge ng,ombe !!
 
Nimesoma andiko la TLS, kwa heshima zote kwa chombo chetu hiki kilichopewa mamlaka kisheria, Nimeshtuka sana, I wish to say,

Kwanza KATIBA HAIJAVUNJWA KWA MHE RAIS SAMIA SULUHU kuapa, na wala hakuna Mkanganyiko wowote wa Kikatiba, kwa yeye kutoteua PM na Baraza jipya. Mmekaa wote kweli mkaona hivyo.

Kwa mujibu wa Katiba Ibara ya 42(5) kuna watu wa aina mbili wanaweza kuwa Rais. Moja, Rais Mteule ambaye anatokana na Ibara ya 42(1). Mbili, Mtu anayeshika kiti cha Rais ambaye anatokana na ibara ya 37(5) na 50(2)(d) ambaye ni Makamu wa Rais. Kwa Mazingira haya, Makamu wa Rais, baada ya kifo cha Rais, anakuwa Kaimu Rais baadae ndio ameapa na kuwa RAIS wa Nchi. Rais Mteule anapatikana kutokana na uchaguzi. Hivyo basi ibara ya 57(2)(f) ya Katiba haitumiki katika mazingira haya. Kwa mjibu wa Sheria, Mhe Rais alitakiwa kutoa taarifa hii kwenye Baraza la Mawaziri baada ya kuapa na alifanya hivyo, maana yake Baraza lipo.

Hata hivyo kwa tamaduni za Kiafrika, kitanzania na Misingi ya UTU, SIONI KAMA NI JAMBO JEMA SANA KUANZA KUJADILI MGAWANYO WA MADARAKA TUNGALI HATA HATUJAMZIKA ALIYEKUWA KIONGOZI WETU. HUU SIO MSIBA MDOGO, JAMBO HILI ZITO LIKO MIKONONI MWA RAIS WETU MAMA SAMIA SULUHU, HALAFU SISI TUANZE KUMPATIA MAMBO YA MARA TEUA PM, MARA VUNJA BARAZA, KATIBA INAELEKEZA RAIS KUAPA NA NAMNA YA KUMPATA MAKAMU WA RAIS.

KWA MJIBU WA KATIBA RAIS ANARUHUSIWA KUVUNJA BARAZA MUDA WOWOTE NA KUPANGA ATAKAVYO HATA SIO KWA MAZINGIRA KUAPA KWAKE,

KWANINI HATUIONI HEKIMA YAKE YA KUSHUGHULIKIA MSIBA KUMSITIRI KWANZA ALIYEKUWA KIONGOZI WETU? TUNAANZA NA MAZISHI AU MIRATHI? 😭😭😭😭

Pia soma > TLS: Kwa Mujibu wa Katiba, sasa Tanzania haina baraza la Mawaziri, Rais Samia atakiwa kuteua Waziri Mkuu ndani ya siku 14
Umesahau Kama uliteuliwa wakati Mh.Mahiga hajazikwa? Mbona hukukaa huo uteuzi Kama wewe ni mtu kweli?
 
Nimememwelewa mwigulu, Raisi alitakiwa kutoa taarifa Kwa Baraza , ni Baraza lipi? Kwa mazingira yake hlo Baraza lilikuwepo , na hivyo busara aliyotumia Raisi ya kusitiri mwili Kwanza zen maswala ya kuvunja Baraza yaendelee ipo poa tuuu...anyway naweza kosolewa mana sio mtaalam wa Sheria Na katiba ....

Mahiga Alipokufa Magufuli alisubiri azikwe ndio ajaze nafasi yake? Wakati Magufuli akifanya hayo, mbona Mwigulu hakumshauri atumie busara sijui maadili?
 
Ni wapi katiba imesema raisi akifariki dunia,makamu wa Raisi atakayeapishwa kuwa Raisi inabidi aunde baraza lake la mawaziri?
samia anaunda baraza jipya hata litakuwa na watu walewale ktk wizara zilezile lzm wale kiapo cha utii mbele yake,na waziri mkuu anaweza kuwa siyo Majaliwa tena.
 
Namkumbuka kwenye issue ya Lwakatare akijiapiza kuwa anao ushahidi.
 
samia anaunda baraza jipya hata litakuwa na watu walewale ktk wizara zilezile lzm wale kiapo cha utii mbele yake,na waziri mkuu anaweza kuwa siyo Majaliwa tena.
Hujajibu swali langu,ni wapi katiba imesema hivyo
 
Nadhan unajipigia debe kiaina
Nimesoma andiko la TLS, kwa heshima zote kwa chombo chetu hiki kilichopewa mamlaka kisheria, Nimeshtuka sana, I wish to say,

Kwanza KATIBA HAIJAVUNJWA KWA MHE RAIS SAMIA SULUHU kuapa, na wala hakuna Mkanganyiko wowote wa Kikatiba, kwa yeye kutoteua PM na Baraza jipya. Mmekaa wote kweli mkaona hivyo.

Kwa mujibu wa Katiba Ibara ya 42(5) kuna watu wa aina mbili wanaweza kuwa Rais. Moja, Rais Mteule ambaye anatokana na Ibara ya 42(1). Mbili, Mtu anayeshika kiti cha Rais ambaye anatokana na ibara ya 37(5) na 50(2)(d) ambaye ni Makamu wa Rais. Kwa Mazingira haya, Makamu wa Rais, baada ya kifo cha Rais, anakuwa Kaimu Rais baadae ndio ameapa na kuwa RAIS wa Nchi. Rais Mteule anapatikana kutokana na uchaguzi. Hivyo basi ibara ya 57(2)(f) ya Katiba haitumiki katika mazingira haya. Kwa mjibu wa Sheria, Mhe Rais alitakiwa kutoa taarifa hii kwenye Baraza la Mawaziri baada ya kuapa na alifanya hivyo, maana yake Baraza lipo.

Hata hivyo kwa tamaduni za Kiafrika, kitanzania na Misingi ya UTU, SIONI KAMA NI JAMBO JEMA SANA KUANZA KUJADILI MGAWANYO WA MADARAKA TUNGALI HATA HATUJAMZIKA ALIYEKUWA KIONGOZI WETU. HUU SIO MSIBA MDOGO, JAMBO HILI ZITO LIKO MIKONONI MWA RAIS WETU MAMA SAMIA SULUHU, HALAFU SISI TUANZE KUMPATIA MAMBO YA MARA TEUA PM, MARA VUNJA BARAZA, KATIBA INAELEKEZA RAIS KUAPA NA NAMNA YA KUMPATA MAKAMU WA RAIS.

KWA MJIBU WA KATIBA RAIS ANARUHUSIWA KUVUNJA BARAZA MUDA WOWOTE NA KUPANGA ATAKAVYO HATA SIO KWA MAZINGIRA KUAPA KWAKE,

KWANINI HATUIONI HEKIMA YAKE YA KUSHUGHULIKIA MSIBA KUMSITIRI KWANZA ALIYEKUWA KIONGOZI WETU? TUNAANZA NA MAZISHI AU MIRATHI? [emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]

Pia soma > TLS: Kwa Mujibu wa Katiba, sasa Tanzania haina baraza la Mawaziri, Rais Samia atakiwa kuteua Waziri Mkuu ndani ya siku 14
 
Yaani wapinzani kulalamika ni jadi yao! Mnadhani kuna kupumua hapa? Magu spirit will prevail
Ungejua hiki kifo Magu alikitafuta kwa juhudi Sana ili kukimstiri na aibu ya kushindwa vibaya baada ya maneno yake ya shobo dhidi ya watangulizi wake,basi ungejiandaa tu kwa big U turn.hakuna mtu mwenye Akili anaweza kufuata ujinga wa Magu.mwache aende tu
 
Yaani wapinzani kulalamika ni jadi yao! Mnadhani kuna kupumua hapa? Magu spirit will prevail
Ni muhimu sana kusoma somo la historia.
Sijui kama China na Urusi fikra za waasisi wao bado zina prevail.
 
Back
Top Bottom