Waziri wa Kilimo Hussein Bashe zuieni uuzwaji wa chakula nje ya nchi, mfumuko wa bei unatisha!

Waziri wa Kilimo Hussein Bashe zuieni uuzwaji wa chakula nje ya nchi, mfumuko wa bei unatisha!

Bashe aache kupeleka Chakula kwa ndugu zake Ethiopia na Somalia aanze kuangaika na Waswahili,kweli!!
Kwanza Mama alipokuwa Kagera alisema chakula kipo chakutosha!
Kwaiyo Watanganyika tupambane na hali yetu!
Kwani alikuja kukupora kwako? Kalime acha porojo na blaa blaa za kijinga
 
Mleta mada akili huna

Kama mfumuko wa bei za vyakula unaona mkubwa rudi kijijini ukalime chakula chako

Wacha wakulima tupate faida ya jasho letu
Ni kweli mnanufaika kwa bei hiyo ila mngepambana muwezeshwe muuze unga badala ya mahindi yan hapo ndio mngepiga pesa kinyama tena ingewezekana hata mkiuzia hapa hapa TZ
 
Naona hapa kuna ndezi zinashangilia vyakula kupanda bei, eti wakulima nao wanufaike. Hawa nguruwe [emoji200] hawajui kuwa mkulima huwa hacheleweshi kuuza mazao, na sasa kashauza kila kitu. Na ikitokea taifa au shehemu wanakumbwa na njaa wanaokufa njaa siku zote ni haohao wakulima. Acheni huo upuuzi
 
Mkuu

Bei ya debe la mahindi huko Tabora vijijini ni 25000/= hadi sasa, watu wameshaanza kula kwa kununua unga kwa kilo sh.1700 hadi sasa na hii ni Oktoba hatujui January hali itakuwaje!

Fungeni mipaka hali sio nzuri kabisa, watu wasije kufa njaa, mfuko wa sembe ushafika sh.37000/= tena vijijini kabisa hali sio nzuri!

Naamini utasoma na hatua zitachukuliwa!
Naimani waziri amesoma na amekuelewa
 
Kwani alikuja kukupora kwako? Kalime acha porojo na blaa blaa za kijinga
Acheni utapeli,hizo Bei mnazotaja ndizo ambazo Bashe na watu wake anaowapa vibali wanauza,hakuna mkulima anauza mazao kwa Bei hizo kwa wafanyabiashara.Kama yupo nitajie Kijiji ambacho Mkulima anafaidika na Kilimo zaidi ya Madalali na Wafanyabiashara uchwara.
 
Ni kweli mnanufaika kwa bei hiyo ila mngepambana muwezeshwe muuze unga badala ya mahindi yan hapo ndio mngepiga pesa kinyama tena ingewezekana hata mkiuzia hapa hapa TZ
Kwani unga ndio ungeuzwa Bei ya chini? Wako wajasiliamali kibao wanauza unga..

Kama ni kuwawezesha Serikali ya Awamu ya 6 kama ikivyosema haifungi mipaka pia inawawezesha wajasiliamali kwa mikopo ya viwanda vya kuiobgeza thamani Mazao..

Ilishusha riba na Sasa sekta ya kilimo pesa za mikopo zinamiminika 👇
 
Attachments

  • Screenshot_20221020-105106.png
    Screenshot_20221020-105106.png
    108.3 KB · Views: 5
Acheni utapeli,hizo Bei mnazotaja ndizo ambazo Bashe na watu wake anaowapa vibali wanauza,hakuna mkulima anauza mazao kwa Bei hizo kwa wafanyabiashara.Kama yupo nitajie Kijiji ambacho Mkulima anafaidika na Kilimo zaidi ya Madalali na Wafanyabiashara uchwara.
Na wewe Sasa utakuwa mburula,hakuna sehemu ambayo haifiki na Wala Haina mawasiliano kwa sasa hapa Tanzania kiasi kwamba eti mjini Bei iwe kubwa na kijijini iwe ndogo Sana,utakuwa hujawahi fanya biashara Wala huelewi biashara..

Kwa taarifa yako biashara yaazo inafanywa na Wachuuzi wadogo wadogo na sio wafanyabiashara wakubwa..

Mfano Kijijini ndani huko gunia ni sh.65,000 na hapa Mjini niliko ni 80,000 sasa unasemaje mkulima hapati hii Bei?

Akitaka Bei nzuri zaidi asafirishe mwenyewe alete mjini,alipie ushuru ndio apate hiyo 80,000.
 
Mkuu

Faida itapatikana kwa kukuza sarafu yetu kwenye soko la Dunia na kudhibiti mfumuko wa Bei!SIO kwa kupaisha mfumuko wa bei kama HIVI!!
Sarafu za noti ni vikaratasi tu wana print internet cafe kubwa

Unaprint bila jasho unabonyeza tu ki button cha command ya Print

Huwezi linganisha na kulima na hivyo vikaratasi vyenu ambavyo mna print kwenye printer na kuviita noti za dola au noti za hela ya Tanzania vyote vikwa mazao ya printer sio shambani

Wakulima lazima tufike mahali watu wa mjini mtuheshimu na vikaratasi vyenu vinaitwa noti mnavyolipwa huko mjini bila kulima chochote
 
Mkuu

Bei ya debe la mahindi huko Tabora vijijini ni 25000/= hadi sasa, watu wameshaanza kula kwa kununua unga kwa kilo sh.1700 hadi sasa na hii ni Oktoba hatujui January hali itakuwaje!

Fungeni mipaka hali sio nzuri kabisa, watu wasije kufa njaa, mfuko wa sembe ushafika sh.37000/= tena vijijini kabisa hali sio nzuri!

Naamini utasoma na hatua zitachukuliwa!
UVIVU wako wa kulima unataka wakulima tuteseke kwa bei zenu za kimasikini? Acha tukauzie wenye pesa zao wewe
 
Ukitaka kujua hasara ya kuuza mahindi jaribuni kuwauzia wakenya unga pekee na si mahindi kama watanunua
Kwani unga ndio ungeuzwa Bei ya chini? Wako wajasiliamali kibao wanauza unga..

Kama ni kuwawezesha Serikali ya Awamu ya 6 kama ikivyosema haifungi mipaka pia inawawezesha wajasiliamali kwa mikopo ya viwanda vya kuiobgeza thamani Mazao..

Ilishusha riba na Sasa sekta ya kilimo pesa za mikopo zinamiminika 👇
 
Bora uko 37000 niliko sembe kg 25 ni elfu 40
 
Mleta mada akili huna

Kama mfumuko wa bei za vyakula unaona mkubwa rudi kijijini ukalime chakula chako

Wacha wakulima tupate faida ya jasho letu
Si ajabu hizi bei hazimnufaishi Mkulima
 
Je kufunga mipaka kutashusha Bei kwa nafaka?

Je chakura Kiko mikononi mwa wakulima au kwa waranguzi?

Dagaa nao wamepanda Bei je nawenyewe tufunge mipaka?

Kwanini Kila anae amka nakukutana naongezeko la Bei kwenye mahindi, unga na mchere anaona jibu ni kufunga mipaka?

Nilitegemea kutolewa wito wakulima mazao ya mda mfupi kwa maeneo yenye mvua.
Kushawishi serikari iongeze bajeti ya Kununua mazao ya wakulima hasa nyakati za mavuno.
Na kutoa wito kwa serikali , ingize chakura sokoni Ili kupunguza uhaba wa nafaka , maana hata mipaka ikifingwa bila hatua nyingine Bei hazishuki.
 
Wakulima wameshauza mazao Yao mda Sana na wengine waliuzia shambani wafanyabiashara ndo wanufaikaji wakubwa kwa huu mfumuko WA bei
Sijui kwa nini hili hawalioni hawa watu.
Nipo Kusini huku ninanunua korosho zikiwa bado maua,na hili ni kwa kila mwaka na inafanyika kwa mazao mengi tu yakiwamo ya chakula.

Bei ya kununua kilo moja ya korosho kwa sasa ni 800 ambapo unapokuja msimu wa minada hufika 2300 kwa kilo,sasa hapo nimeshamlipa mkulima tsh 800 kwa kilo kwa korosho ambazo hazijavunwa,je akivuna na bei ya kilo ikawa 2500 mtasema mkulima ananufaika na bei hiyo?

Njooni huku mashambani muone wakulima wasivyofaidika kabisa na bei kubwa ya haya mazao kwa kuwa umasikini mkubwa umewazunguka kiasi kwamba hawezi kusubiria mpaka avune na kupeleka mnadani kesho na kulipwa baada ya mwezi wakati leo hana chumvi, sukari wala mafuta ya taa na "kangomba" nipo tayari kumpa hela ya kutatua changamoto zake za leo kwa kununua "maua" ya korosho!
 
Akiuza kwa bei ghali halafu akanunua mahitajit kwa bei kubwa atapata faida Gani!!?

UNAFIKIRI uchumi wetu utakuaje kwa style Hiyo!!?

Maoni yako ni economic oriented au ni politically perspective!?
Hapo ndipo unapoambiwa unahitaji kutumia Akili zaidi ya Ushabiki ok mkulima anauza mazao kwa soko la nje then njaa inaingia then huyo huyo na jamii yake wananunua bidhaa zitokanazo na mazao waliyouza kwa bei ya juu
 
Back
Top Bottom