Mwanamaji
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 2,905
- 4,518
Kwenye mfano wako hapo hapo.Sijui kwa nini hili hawalioni hawa watu.
Nipo Kusini huku ninanunua korosho zikiwa bado maua,na hili ni kwa kila mwaka na inafanyika kwa mazao mengi tu yakiwamo ya chakula.
Bei ya kununua kilo moja ya korosho kwa sasa ni 800 ambapo unapokuja msimu wa minada hufika 2300 kwa kilo,sasa hapo nimeshamlipa mkulima tsh 800 kwa kilo kwa korosho ambazo hazijavunwa,je akivuna na bei ya kilo ikawa 2500 mtasema mkulima ananufaika na bei hiyo?
Njooni huku mashambani muone wakulima wasivyofaidika kabisa na bei kubwa ya haya mazao kwa kuwa umasikini mkubwa umewazunguka kiasi kwamba hawezi kusubiria mpaka avune na kupeleka mnadani kesho na kulipwa baada ya mwezi wakati leo hana chumvi, sukari wala mafuta ya taa na "kangomba" nipo tayari kumpa hela ya kutatua changamoto zake za leo kwa kununua "maua" ya korosho!
Je, kufunga mipaka kunamsaidiaje huyo mkulima ambaye tayari ameuza mahindi au korosho kwa bei ndogo (bei ya shambani) ?