Angalau atapata ahueni kwenye chakula akapambana na mengine!
Vuta picha kama mfumuko wa bei ya chakula ukaungana na bidhaa nyingine Hali itakuaje!?
Kwa nn mkulima asiuze mazao yake kwa bei ya juu ili angalau apate hela ya kukidhi mahitaji yake mengine!!
Kwann uhisi kwamba mkulima yeye ndo anatakiwa auze mazao yake kwa bei ya chini wakati bidhaa nyingine zipo juu??
Usijiangalie wewe kwa sababu unapokea mshahara mwisho wa mwezi mwangalie yule anayepambana kulima kuingia gharama nyingi mwisho wa siku hata gharama aliyoingia hairudi miaka nenda rudi, yeye ni kupata hasara tu kwa kigezo kwamba mazao yasiuzwe nje!!
Kufanya export ya bidhaa za nchi ndo uchumi wenyewe wa nchi kuwa mkubwa!!
How?
1.Mazao yakiuzwa nje serikali inapata kodi kupitia hayo mazao!!
2.Nchi inapokea fedha za kigeni kwa hiyo sarafu yetu inazidi kuimarika kwa kufanya exportation
3. Demand ya mazao itakuwa juu kwa sababu ya uhakika wa soko, kwa hiyo watu wengi watajiingiza kwenye kilimo na kuanza kulima kwa wingi, na hivyo uchumi wa kilimo utaendelea kuwa juu!! Tofauti na hapo tulipotokea kwamba mtu unalima hujui uuze wapi? Ni upuuzi mtupu kuweka mtaji wako kwenye kilimo then mazao ya kuozee kwa kigezo cha kulinda watu na njaa!!
4. Kwa sababu population kubwa ya watu watajiingia kwenye kilimo pia viwanda vya mbolea pia vitauza kwa wingi na kuongeza pato kwa nchi!!
5. Hivi viwanda vitatengeneza ajira mbalimbali kwa watanzania!!
6. Kilimo pia kitatengeneza ajira nyingi sana kwa watanzania!!
Nakadhalika, nakadhalika, hata niandike mpaka kesho sitamaliza faida zake!!
Ufanyeje!!
1. Kama wewe ni mkulima jitahidi kabla ya kuuza mazao yako yote weka akiba ndani, ya kukutosheleza angalau kwa kipindi kisichopungua mwaka mzima!!
2. Kama wewe siyo mkulima, jitahidi kununua akiba na kuhifadhi wakati mazao yakiwa chini kwa ajili ya familia yako kwa kipindi kichopungua mwaka mmoja!!
3. Kila mtu ajitahidi kulima angalau sehemu anayojua ataweza kuvuna mazao ya kutosheleza familia yake, watu waache uvivu, lima mahindi, mpunga, maharagwe, mihogo, alzeti n.k. n.k
4 Anayeweza kulima large scale asiache kufanya hivyo, Tanzania ina utajiri mkubwa sana wa ardhi yenye rutuba
Waacheni wakulima wafaidi jasho lao kwa kuwa na masoko ya uhakika!! Heko Mama Samia!! Heko kwa waziri wa Kilimo!!