Waziri wa Kilimo Hussein Bashe zuieni uuzwaji wa chakula nje ya nchi, mfumuko wa bei unatisha!

Waziri wa Kilimo Hussein Bashe zuieni uuzwaji wa chakula nje ya nchi, mfumuko wa bei unatisha!

Mkuu

Bei ya debe la mahindi kwenye baadhi ya vijiji nchini ni 25000/= hadi sasa, watu wameshaanza kula kwa kununua unga kwa kilo sh.1700 hadi sasa na hii ni Oktoba hatujui January hali itakuwaje!

Fungeni mipaka hali sio nzuri kabisa, watu wasije kufa njaa, mfuko wa sembe ushafika sh.37000/= tena vijijini kabisa hali sio nzuri!

Kufunga mipaka walau hata KWA muda mfupi itasaidia price regulatory mechanism Ili bei ya chakula isije ikapaa Sana Hadi hapo January,mkiacha hivi hivi watakao KUWA na uwezo wa kukinunua ni wachache Sana na hao wakulima wanafurahia bei kubwa watashindwa kuja kukinunua chakula na watalia njaa tena wengi Sana tu na kuilaumu serikali bei zimepanda,ukiongeza na anguko la uchumi wa Dunia kutokana na vita pia ongezeko la bei la bidhaa nyingine litafanya Maisha ya huyo mkulima maskini kuwa magumu mno!!

Ikumbukwe njaa huangusha wafalme tunapaswa kuheshimu na kuchukua tahadhari zote.

Mungu ibariki Tanzania

Naamini utasoma na hatua zitachukuliwa!
Tumelima kwa gharama zetu halafu mtupangie wapi pa kuuza mazao yetu...mnatumia nini kufikiri nyie watu...[emoji51]
 
Tumelima kwa gharama zetu halafu mtupangie wapi pa kuuza mazao yetu...mnatumia nini kufikiri nyie watu...[emoji51]
Utanielewa tu!mbona Mwakani sio mbali!

Niambie mwaka ujao kutakuwa na mvua ya kutosha kilimo cha mahindi nchini!?

Utabiri wa Hali ya hewa unasemaje!?

Subirini!
 
Hapo ndipo unapoambiwa unahitaji kutumia Akili zaidi ya Ushabiki ok mkulima anauza mazao kwa soko la nje then njaa inaingia then huyo huyo na jamii yake wananunua bidhaa zitokanazo na mazao waliyouza kwa bei ya juu
Huyo Mkulima , ameambiwa auze mavuno yake yote? Je kama nitabia yake kuuza bila kujiweka akiba ,so Bado atauza hata kama nisoko landani?
 
Hakumsaidii yeye binafsi kama mkulima,bali kunasaidia Watanzania wote kwani bei ya mazao ya chakula haitakuwa juu kutokana na kupatikana kwa urahisi.
Huo urahisi ndio unao sababisha kupanda kwa gharama za vyakura kwa kupaa.
 
Utanielewa tu!mbona Mwakani sio mbali!

Niambie mwaka ujao kutakuwa na mvua ya kutosha kilimo cha mahindi nchini!?

Utabiri wa Hali ya hewa unasemaje!?

Subirini!
Mwl Athumani Ramadhani, tatizo la njaa kama linakuja, hilo litakuwa ni janga la nchi husika na viongozi waliopo walioshindwa kuona tatizo na kuchukuwa tahadhari lawama itawaangukia.

Nijuavyo mimi, hakuna nchi yoyote duniani ambayo serikali yake huacha tu biashara yoyote ifanyike bila taratibu na tahadhari ya kulinda maslahi ya wananchi wake, siyo wakulima tu, bali wananchi wote.
Sasa kama serikali yetu itaona ni vyema wakulima wafaidike zaidi kutokana na uhaba wa mazao kwa hasara ya raia wengine wote nchini, hilo litakuwa ni jambo la kushuhudia. Lakini binafsi siamini kwamba hapa ni mkulima ndiye anayenufaika, bali kuna kundi la watu wasiolima ndio watakaonufaika kwa mgongo wa mkulima.

Lakini kabla sijaondoka, naona nikuachie wazo ambalo sijaona likitajwa popote katika mada yako hii. Kama bei zimepanda bei kwa sababu ya mazao kuuzwa nje, hivi wewe unaonaje tukihimiza serikali iruhusu wenye uwezo wa kuingiza mazao hayo toka kokote duniani kwa bei nafuu ili pawepo na ushindani? Wakulima watafaidika kwa bei kubwa wanayouza nje, na walaji nao watafaidika kwa kuwepo na bidhaa yenye bei nafuu kutokana na kupatikana sehemu nyingine duniani.
Kwa nini tung'ang'anie mazao ya hapa hapa nchini ndiyo yauzwe kwa bei za chini kama tunaweza kupata mazao hayo hayo kutoka sehemu zingine duniani? Hii si ndiyo itakuwa biashara huria tunayoiimba kila siku?

Hebu lipe fikra zako jambo hilo.
 
Mkuu

Bei ya debe la mahindi kwenye baadhi ya vijiji nchini ni 25000/= hadi sasa, watu wameshaanza kula kwa kununua unga kwa kilo sh.1700 hadi sasa na hii ni Oktoba hatujui January hali itakuwaje!

Fungeni mipaka hali sio nzuri kabisa, watu wasije kufa njaa, mfuko wa sembe ushafika sh.37000/= tena vijijini kabisa hali sio nzuri!

Kufunga mipaka walau hata KWA muda mfupi itasaidia price regulatory mechanism Ili bei ya chakula isije ikapaa Sana Hadi hapo January,mkiacha hivi hivi watakao KUWA na uwezo wa kukinunua ni wachache Sana na hao wakulima wanafurahia bei kubwa watashindwa kuja kukinunua chakula na watalia njaa tena wengi Sana tu na kuilaumu serikali bei zimepanda,ukiongeza na anguko la uchumi wa Dunia kutokana na vita pia ongezeko la bei la bidhaa nyingine litafanya Maisha ya huyo mkulima maskini kuwa magumu mno!!

Ikumbukwe njaa huangusha wafalme tunapaswa kuheshimu na kuchukua tahadhari zote.

Mungu ibariki Tanzania

Naamini utasoma na hatua zitachukuliwa!

Hakuna Kitu Kinachoshinda Uvumilivu kwa wananchi Kama Kupanda Kwa Bei ya Vyakula.
Unaweza Sema Oooh Ongezeni Uzalishaji.
Ok sawa Huo Uzalishaji Uongezwe Kwanza Ndio Ziada Iuzwe Nje!
Sio Huna Ziada halafu Unauza Nje Alooo[emoji30][emoji2955]
 
Mamlaka ya Hali ya hewa imeshatangaza Rasmi chini ya wastani wa mvua KWA mikoa 14 nchini!!

Mavuno yatakuwa kidogo MWAKA ujao!!

Wizara ya kilimo makinikeni sasa!!
 
Back
Top Bottom