ras jeff kapita
JF-Expert Member
- Jan 4, 2015
- 22,152
- 33,899
Umeomba ruksa kwa sheikh lkn?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Naunga hoja kwa mikono yote miwili 100%Mheshimiwa Hussein Bashe, natumai na Rais wetu mama Samia Suluhu Hasan na washauri wake wengine utawafikia ujumbe huu.
Zao la bangi za aina tofauti (different varieties of hemp) linastawi vizuri sana Tanzania. Ni wakati muafaka, tena tumechelewa sana, kuanzisha zao la bangi kwa faida. Zao la bangi linaweza kututowa kwenye umasikini kwa haraka sana.
Baadhi ya faida zinazotokana na zao la bangi ni pamoja na:
Dawa aina mbali mbali, zinazotumika hivi sasa mahpspitalini na dawa mbadala.
Pia bangi inawe kutengeza karatasi, inaweza kutengeza mbao, inaweza kutengeza, "vigae" vya kuezekea, inaweza kutengeza bodi za gari ambazo ni bora kuliko za mabati.
Licha ya hayo, inaweza kutengeneza virutubisho mbali mbali vya aya ya binadam, wanyama na mimea. Pamoja na madawa ya kuzuia wadudu wa mimea.
Pia bangi inaweza kutengeza mafuta ya kutumika kwenye magari ambayo ni bora kuliko ethano na methanol.
Kinachotakiwa kufanywa ni kuanza na aina moja au mbili ya bidhaa muhimu na kufunguliwa kituo maalum cha utafito na kuzalisha mbegu bpora kwa biashara.
hatuna haja ya kutegemea mataifa ya nje kwenye hili, tunaweza kuzalisha mali ghafi zetu wenyewe na kuwauzia nje bidhaa zinazotokana na bangi. Ni kujipanga tu.
Nafahamu Bashe utaweza hili kwa ufanisi mkubwa ukilivalia njuga. Weka legacy kijana kupitia bangi.
Nafahamu wengi wakisikia "bangi" akili zao zinakwenda katika kilevi cha bangi. Kilevi cha bangi ni matumizi duni ya bangi, ingawa na yenyewe inaweza kufanyiwa tafiti ika[atikana mbegu isiyo na madhara na ikauzwa kihalali kuliko hivi sasa tunaletewa mbegu za kutia watu wazimu, mpaka skanka limejaa sasa hivi linaumiza vijana.
Tuondokane na ujinga na kufata watu, tumepata elimu ili ituukomboe siyo tuendelee kuwa wajinga wa kuburuzwa kama misukule, wanachotaka mabwana wakuba ndiyo tukifate, ni wakati Tanzania tukajifanyia yetu wenyewe na hao wakubwa tuwaimbishe nyimbo tunazotaka sisi. Rasilimali tunazo, kwanini watuendeshe na mali zetu?
Uchumi tuna tunaukalaia kwa kudanganywa na nchi za magharibi ili tuendelee kuwa watumwa wao daima.
Naamini ndani ya miaka ya kuruhusu zao la bangi na tafiti zake za kina, hatutako[pa tena nje, sisi tutakuwa wakopeshaji.
Nawasilisha.
. Kinachotakiwa kuboreshwa ni:-
Wacha we,,Faiza mi 5 tenaMheshimiwa Hussein Bashe, natumai na Rais wetu mama Samia Suluhu Hasan na washauri wake wengine utawafikia ujumbe huu.
Zao la bangi za aina tofauti tofauti (different varieties of hemp) linastawi vizuri sana Tanzania. Ni wakati muafaka, tena tumechelewa sana, kuanzisha zao la bangi kwa faida. Zao la bangi linaweza kututowa kwenye umasikini kwa haraka sana.
Baadhi ya faida zinazotokana na zao la bangi ni pamoja na:
Dawa aina mbali mbali, zinazotumika hivi sasa mahospitalini na dawa mbadala.
Pia bangi inaweza kutengeza karatasi, inaweza kutengeza mbao, inaweza kutengeza, "vigae" vya kuezekea, "boards" mbali mbali za kujengea na kuundia fanicha, inaweza kutengeza bodi za magari ambazo ni bora kuliko za mabati.
Licha ya hayo, inaweza kutengeneza virutubisho mbali mbali vya kutumika na binadam, wanyama na mimea. Pamoja na madawa ya kuzuia wadudu wa mimea.
Pia bangi inaweza kutengeneza mafuta ya kutumika kwenye magari ambayo ni bora kuliko ethanol na methanol.
Kinachotakiwa kufanywa ni kuanza na aina moja au mbili ya bidhaa muhimu na kufunguliwa kituo maalum cha utafiti na kuzalisha mbegu bora kwa biashara.
hatuna haja ya kutegemea mataifa ya nje kwenye hili, tunaweza kuzalisha mali ghafi zetu wenyewe na kuwauzia nje bidhaa zinazotokana na bangi. Ni kujipanga tu.
Nafahamu Bashe utaweza hili kwa ufanisi mkubwa ukilivalia njuga. Weka legacy kijana kupitia bangi.
Nafahamu wengi wakisikia "bangi" akili zao zinakwenda katika kilevi cha bangi. Kilevi cha bangi ni matumizi duni ya bangi, ingawa na yenyewe inaweza kufanyiwa tafiti ikapatikana mbegu isiyo na madhara na ikauzwa kihalali kuliko hivi sasa tunaletewa mbegu za kutia watu wazimu. Mpaka skanka limejaa sasa hivi linaumiza vijana.
Tuondokane na ujinga na kufata watu wa magharibi. Tumepata elimu ili itukombowe siyo tuendelee kuwa wajinga wa kuburuzwa kama misukule, wanachotaka mabwana wakubwa ndiyo tukifate, ni wakati Tanzania tukajifanyia yetu wenyewe na hao wakubwa tuwaimbishe nyimbo tunazotaka sisi. Rasilimali tunazo, kwanini watuendeshe na mali zetu?
Uchumi tunao lakini tunaukalia, Nyerere. Kwa kudanganywa tu na nchi za magharibi tutaendelee kuwa watumwa wao daima.
Naamini ndani ya miaka mitatu ya kuruhusu zao la bangi na tafiti zake za kina, hatutakopa tena nje, sisi tutakuwa wakopeshaji.
Nawasilisha.
Siasa tu hizo,,,,mbona pombe pia kuna baadhi ya watu hawaiwezi ila ipo inauzwa na athari zake zote za kiafya , bangi pia ingeruhusiwa kama pombe tu wanao iweza waendelee na wasio iweza waendelee na mengineBANGI! UTAZIBITI VP UVUTAJI WAKE? C VIJANA WOTE WATAKUWA MATAHIRA
Pombe na sigara zinapatika kila mahali kila mtu anakunywa na kuvuta sigara?BANGI! UTAZIBITI VP UVUTAJI WAKE? C VIJANA WOTE WATAKUWA MATAHIRA
Ni kweli. Tatizo kubwa ni kwa viongozi na Wataalam (Tekanalojia na Maadili) kutokutambua na kukubali au kuzichunguza kwa undani baadhi ya Sheria kuona kama zimepitwa na wakati au ziliwekwa kimkakati enzi hizo kwa malengo ya kudhibiti ukuaji wa kiuchumi (ni vita)wa maendeleo ya Taifa na Watu wake na kuzifanyia marekebisho.Ni kubadili tu mtazamo. Bangi na Gongo ni bidhaa ambazo zikihalalishwa zinaweza kuchangia pato la Taifa. Tazama, tangu zimepigwa vita mbona ndiyo zinashamiri..!!!
Gongo imesomesha mtoto wa shangazi saivi ni askari Huwa anaulizwa akija nyumbani vipi Huwa unawakamata ? Anakubali Huwa tunakamata muda huo walevi wa gongo wamejikojolea wapo hapo hapo nyumbaniNi kubadili tu mtazamo. Bangi na Gongo ni bidhaa ambazo zikihalalishwa zinaweza kuchangia pato la Taifa. Tazama, tangu zimepigwa vita mbona ndiyo zinashamiri..!!!
BANGI! UTAZIBITI VP UVUTAJI WAKE? C VIJANA WOTE WATAKUWA MATAHIRA
Mi nakumbuka mzee mmoja alifungwa gerezani kwa kesi ya gongo. Siku ameachiliwa nikamuuliza, "Utakwenda kufanya kazi ya gongo tena?". Alinijibu kwa ujasiri kuwa hawezi kuacha kazi hiyo kwa sababu imemuwezesha kusomesha watoto wake, amefungua bucha mbili za nyama na ana nyumba za kupangisha. Alijinasibu kuwa biashara ya gongo kwake ni zaidi ya mgodi (madini), maana kule ni pata potea. Hiyo ilikuwa mwaka 1999 jijini Arusha.Gongo imesomesha mtoto wa shangazi saivi ni askari Huwa anaulizwa akija nyumbani vipi Huwa unawakamata ? Anakubali Huwa tunakamata muda walevi wa gongo wamejikojolea wapo hapo hapo nyumbani
Naomba hapa Hasahasa ilimwe kwa ajili ya Export tu parekebishwe kuwa kwa matumizi sahihi kwani hata ss waTz tunahitaji kuwa na vi wanda vyetu wenyewe vya kuichakata bangi kupata madawa yaliyomo ndani yake badala ya kuyaagiza madawa yatokanaya na bangi huko tulikoiuza tena kwa bei poa halafu bei ya madawa yatokanayo na bangi yetu wanatuuzia kwa bei mbaya.Ingependeza ungetupa Somo, kwa nchi zilizoruhusu zimeongeza kiasi gani kwenye pato la taifa?
Hata bungeni kuna wabunge walizungumzia, Hivyo uko sahihi. Hasahasa ilimwe kwa ajili ya Export tu