Kutumia siyo kulikuza zao la bangi kibiashara, ni kuharibu thamani yake.Mkuu; waTz Raia walishaamka kitambo ila Serikali yao bado inakoroma usingizini. Nadhani Dozi ya mkoloni (Brainwash) ilizidishwa kipimo kwa Serikali na mamlaka zake. e.g. Waliopo humo serikali na vyombo vyake kwa kificho ni watumiaji mno wa zao hilo; ila wakija huku kwetu hadharani wanatukazia ss macho.
Ni kweli kabisa - kuanzia madawa, mafuta ya aina zote, chanzo cha Nishati(Fuel), kamba za kujengea n.k. n.k. Lakini faida zooote hizo Serikali na Wizara zake Mambo ya ndani, Kilimo na Mifugo, Ofisi ya PM na nyinginezo wamezifumbia macho na wameshupalia eti ni zao Haramu.Bangi ni zao muhimu sana, ni malighafi kwa karibia kila kitu cha matumizi ya binadam.
Hayo 👆 👆 ni kweli, ila lazima hatua za kuchukua (mchakato)ziwepo. Na hatua ya kwanza kabisa kabisa ni kulitambua zao hilo na kuondoa Marufuku ya Kisheria dhidi ya zao hilo yaani kulihalalisha. Watu wawe huru kuwa na zao hilo na sio kama ilivyo sasa linazalishwa kwa kificho na kutumika kwa kificho. i.e. Haliwezi kuwa ni biashara Halali. Kibiashara (black mkt.)lipo ila ni kwa kificho. Kwa mantiki hiyo, wafanyabiashara halali i.e. wenye leseni (Wanunuzi/wateja wahitaji) watakutana na Wakulima/Wazalishaji kwa uwazi na Serikali (Wizara husika) itafanya kazi yake ya kusimamia na kudhibiti ubora wa viwango. Ifike mahali zao la bangi liweze kuchangia ukuaji wa viwanda vya hapa nchini esp. viwanda vya madawa.Kutumia siyo kulikuza zao la bangi kibiashara, ni kuharibu thamani yake.
Inapaswa bangi iwe mali ghafi ya bidhaa nyingi muhimu.
Kuvuta haifiki hata asilimia moja ya umuhimu wake.
Duh! Umekuja kivingine.BWAAANA AKAEE NANYIIIII
AKAAAE NA ROHOOOO ZENUU
TUMHIMIDIII BWANAAA
TUMSHUKURUUY MUNGUUUU
MTAKIANE AMANI YA BWANA
Upo sawa kabisa. Wataalamu Wana sema gongo Haina kipimo maalumu Cha Ethanol inayotakiwa!!Gongo kama Gongo sio Tatizo. Tatizo ni watumiaji. Mfano, Mtu anakwenda asbh. hajala chochote anamimina chupa nzima. Jioni anarudi hoi analala bila kula chochote. Kwa nini midomo na maini visiungue?
Serikali umejitia upofu kwa kuruhusu Spirits (konyagi, Kijogoo,etc) kuuzwa kihalali eti hao wanalipa kodi - but in the real sense vyote hivyo gongo,konyagi etc ni Ethanol.
Kwa maswali hayo 👆 👆 mbona ni kama unajitoa ufahamu aisee?1.Nchi gani wanatumia bangi kuzalisha mafuta ya kupikia?
2.Aina ipi ya bangi,inazalisha mafuta Kwa wingi?
3.nitajie viwanda viwili vinavozalisha kwa siku lita hata 10 za mafuta yatokanayo na bangi?
Mkuu; Hiyo ni Jargon tuu ya Serikali. Kwani wale waliokuwa wanachakachua k-vant na nyinginezo hazikunyweka? Hii Serikali ingesimamia ili kuweka kipimo maalum cha ethanol ngazi ya mzalishaji mdogo. Tunashindwa wapi?? Mbona tunaweza kutambua ubora wa maziwa ngazi ya mkulima mdogo kwa vipimo ambavyo ni portable unajibebea kipimo mfukoni?? Serikali inashindwaje kuzipima Gongo na kuweza kudhibiti ubora na kiwango cha Ethanol? Hata hivyo ubora wa Ethanol ngazi ya mzalishaji mdogo (kwa kienyeji) hupimwa kwa kuiwasha moto. Ikiwaka ni nzuri (safi) isipowaka imechakachuliwa. Serikali ijiongeze zaidi isijekuwa imepitwa na wazalishaji ngazi ya chini kabisa huko maporini inakozalishwa kwa kificho.Upo sawa kabisa. Wataalamu Wana sema gongo Haina kipimo maalumu Cha Ethanol inayotakiwa!!
Hapo ndio na kukubali dadake, sijui kwanin mama akuvuti ktk serikali kama alivyo fanya kwa kina zuhura😁😁🙏Siamini kwenye "bodi" naamini kwenye vituo vya tafiti.
Kituo cha tafiti kinaweza kuzofanya kazi za bodi na zaidi, kitaalam kabisa.
Tena namshauri Bashe, wachana na mambo ya bodi, anzisha vituo vya utafiti vitavyokuwa direct facilitators zinazosimamiwa na wizara zako.
Tuwe na "Research and development" za uhakika, badala ya bodi za wapigaji.
Hata mm sijui ila ni hizo kelele kila siku za Serikali kwamba tunataka tuwe na maendeleo endelevu. Kwa hiyo tunadhani wanaweza kuwa serious safari hii. Vinginevyo kweli bado tutakuwa tunatwanga maji kwenye kinu.Hivi kitu gani kinachowafanya muamini kuwa Tanzania ipo serious kwenye suala la maendeleo ya nchi?
Hatujawahi kuwa serious kwenye suala la maendeleo, sasa sijui ni kwa vp tutakuwa na uthubutu wa kuanzisha kilimo cha bangi.
Wanachojali ni kuongeza idadi ya magari mapya kila uchao. Hawezi kupitia uzi huu kujifunzaTuna tatizo kubwa la waziri w fedha na sera zake za mikopo.
Wazungu wanakukopesha ili wakugtawale na wao ndiyo wanatushinikiza viwango vya kodi ili waendelee kututawala.
Waziri wa fedha anatakiwa awe na maamuzi magumu kwa sasa.
Kwanza namshauri apige marufuku dhahabu yote kuuzwa nje ya Tanzania, tuinunuwe wenyewe, siyo gtu kwa wazalishaji wadogo, na anaetaka dhahabu atainunuwa dhahabu yetu kupitia soko rasmi la dhahabu.
Sasa hivi tunavituo vya madini, lakini cha kustajaabisha vipo kukusanya kodi tu, havipo kwa kununua hayo madini ili yaratibiwe na kuuzwa rasmi na pesa zote za kigeni zipitie BoT.
Subira yavuta kheri. Jambo jema halihitaji haraka.Hapo ndio na kukubali dadake, sijui kwanin mama akuvuti ktk serikali kama alivyo fanya kwa kina zuhura😁😁🙏
Kweli kabisa.Machozi ya samaki yameenda na maji. Wamesahau magari hayo mapya wanayanunua ni kutokana na fedha ambazo ni kodi zetu.Wanachojali ni kuongeza idadi ya magari mapya kila uchao. Hawezi kupitia uzi huu kujifunza
Mtaalam wa oil purification au refining niko hapa ukipata gap nistueMpaka mafuta ya kupikia chakula ya bangi ni bora kuliko mafuta yoyote tunayoagiza kutoka nje, na kuna aina fulani ya bangfi inaweza kuzalisha mafuta kwa wingi sana.
Msidhani yanalewesha, hayaleweshi yakifanyiwa "purification".