A
Anonymous
Guest
Naomba kupaza sauti kuhusu suala linalotukabili baadhi ya wachimbaji walioshiriki katika mchakato wa safari ya Canada kupitia Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Wadogo wa Madini Tanzania (FEMATA) kwa lengo la kwenda kujifunza, wamekula fedha zetu na hawataki kuzirejesha.
Washiriki tulitoa fedha kwa ajili ya safari hiyo, ilikuwa ifanyike Februari 2026, kutokana na sababu kadhaa wakaenda wachache wakiongozana na Waziri, wengine wakaambiwa wataenda Aprili na wengine Juni 2026, lakini wale ambao hawakufanikiwa kwenda kwa maana ya kukosa VISA au sababu nyingine tukaahidiwa kurejeshewa fedha.
Katika hizo safari wakaenda wachache, wachimbaji zaidi ya 20 tukakwama, wakasema watarejesha fedha zetu, wapo waliochanga Sh Milioni 8, wengine 9 wengine 10.
Tangu wakati huo hadi leo Oktoba 2026, FEMATA haijaturejeshe fedha zetu, tumekuwa tukiahidiwa bila kutimiziwa, wapo waliokopa benki, wanadaiwa wakati safari hawakwenda, hatutendewi haki.
Hili si suala la Kisiasa wala kutafuta ugomvi na mtu, tunachohitaji ni uwajibikaji, uwazi na fedha zetu tulizotoa kwa ajili ya safari ambayo haikufanyika. Wale wanaogusia suala hilo kwenye magroup ya WhatsApp wanaondolewa, tukiwatafuta viongozi hawapokei simu akiwemo aliyeongoza msafara mwanzo kabisa wa safari.
Ujumbe huu ufike kwa Waziri wa Madini, kwa kuwa yeye analifahamu suala hili na alishiriki kwenda na Wadau mwanzoni kabisa, atusaidie kwani inadaiwa fedha zimeliwa na hawana mpango wa kuturudishia.
Pia soma
~ Rais wa FEMATA, John Bina: Tutawashtaki Waliohusika Kula Hela za Wachimbaji Waliolipia Safari ya Canada
~ 𝐅𝐞𝐦𝐚𝐭𝐚: Wachimbaji Madini waliokwama kwenda Canada watajeshewa fedha zao Oktoba 23, 2026