Waziri wa Mambo ya Ndani, Eng. Masauni fuatilia pesa za makusanyo ya Wiki ya Nenda kwa Usalama. Zimepigwa?

HR anakutana na mahabusu wapi mkuu? nasemea nyie mnaokamata watu hovyo hovyo na kuwaweka mahabusu bila sababu za msingi
Rushwa ni ngumu kuisha nchi hii kwani hata aliyekamatwa kihalali anashawishi kwa rushwa aachiwe mkuu.
Rushwa ni suala mtambuka mkuu.

Leo hii ukikamatwa na traffic na una makosa ya wazi utabembeleza uachiwe huku ukimpatia chochote.
Hivyo mla rushwa wa kwanza ni mwananchi mtoa rushwa
 
WAZIRI ENG. MASAUNI

Naomba nikurudishe nyuma kidogo, miaka miwili nyuma ukiwa naibu waziri wa mambo ya ndani, ukiwa kama mwenyeketi wa usalama barabarani uliagiza kila mkoa ukusanye fedha za WIKI YA NENDA KWA USALAMA ambazo hutozwa kuanzia tsh 3,000 hadi 5,000
kwa kulingana na ukubwa wa gari husika.

Baada ya makusanyo hayo ulielekeza kila Mkoa ununue magari kwa ajili ya kusaidia utendaji wa kazi katika ofisi za ma RTO wa mikoa.

Katika maagizo yako hayo karibu mikoa yote ilijitahidi kukusanya kwa uaminifu na kutekeleza agizo lako kuwa walinunua magari kulingana na makusanyo ambapo mikoa iliyokusanya kidogo ilijitahidi kunua hata Noah.

Pamoja na mikoa mingine kutii agizo lako hilo. lakini Mikoa ya kipolisi ya Kinondoni, Ilala na Temeke haikutekeleza agizo lako hilo matokeo yake kuna tetesi kuwa Ofisi ya Kanda ilikusanya pesa zote na zikaishia mikononi mwa wajanja wachache.

Hivyo lengo la agizo lako halikutimizwa. Ili kuupata ukweli wa hili ni kazi rahisi tu ni kuwaita hao ma RTO watakueleza walipoelekeza hizo pesa.

Katika hili unayo nafasi nzuri ya kulifuatilia hili kwani sasa wewe ni Waziri kamili na hili lilikuwa agizo lako mwemyewe.

Mikoa hiyo ya kipolisi kwa ujumla haikosi kuwa na magari yasiyopungua 500,000 na ukizidisha kwa bei ya wastani ya 3,000x500,000=1,500,000,000. Hii ni pesa nyingi zingeweza kulisaidia jeshi la polisi. Naomba nisiwataje wahusika bali jaribu kufuatilia mwenyewe ndani ya muda mfupi utakua na majibu.

Mungu abariki utendaji wako.

Kwani urefu wa kamba zao unaishia wapi?
 
Hapo hapo mkuu.
Zile zilikua enzi za pesa za kubrashi viatu baba

IMG_20220404_113346_582.jpg
 
Rushwa ni ngumu kuisha nchi hii kwani hata aliyekamatwa kihalali anashawishi kwa rushwa aachiwe mkuu.
Rushwa ni suala mtambuka mkuu.

Leo hii ukikamatwa na traffic na una makosa ya wazi utabembeleza uachiwe huku ukimpatia chochote.
Hivyo mla rushwa wa kwanza ni mwananchi mtoa rushwa
gari za traffic zinakaguliwa na nani mkuu? mtu ana kamatwa kosa linadhaminika lakini ananyimwa kwanini asitoe rushwa? itengemezwe application online watu wajaze kuomba dhamana online bila kuonana na mtoa dhamana live vigezo system i-verify yenyewe kama umekizi unaprint chap stationary mtu anatoka, tatizo mnatengeneza mazingira ya rushwa sn, mfano unanikamata eti siti zako chafu, kuna husiana vipi na barabara kama siti zimechanika na wakati siyo gari ya abiria? mambo ya hovyo sn
 
Yule mwamba aliyeomba u IGP Angeles hili jeshi tumfanyie tathmini anaweza kutuvusha
 
Hiyo nayo ni kazi ya waziri wa mambo ya ndani?
 
Zinapigwaje wakati mtoaji ni mmoja, sidhani kama wapigaji ni polisi labda wakipiga walizoletewa kwa ajiri ya shughuli flan lkn sio makusanyo.
Tuwe tunalipa kwa control number hao mchwa wakose kwa kula
 
WAZIRI ENG. MASAUNI

Naomba nikurudishe nyuma kidogo, miaka miwili nyuma ukiwa naibu waziri wa mambo ya ndani, ukiwa kama mwenyeketi wa usalama barabarani uliagiza kila mkoa ukusanye fedha za WIKI YA NENDA KWA USALAMA ambazo hutozwa kuanzia tsh 3,000 hadi 5,000
kwa kulingana na ukubwa wa gari husika.

Baada ya makusanyo hayo ulielekeza kila Mkoa ununue magari kwa ajili ya kusaidia utendaji wa kazi katika ofisi za ma RTO wa mikoa.

Katika maagizo yako hayo karibu mikoa yote ilijitahidi kukusanya kwa uaminifu na kutekeleza agizo lako kuwa walinunua magari kulingana na makusanyo ambapo mikoa iliyokusanya kidogo ilijitahidi kunua hata Noah.

Pamoja na mikoa mingine kutii agizo lako hilo. lakini Mikoa ya kipolisi ya Kinondoni, Ilala na Temeke haikutekeleza agizo lako hilo matokeo yake kuna tetesi kuwa Ofisi ya Kanda ilikusanya pesa zote na zikaishia mikononi mwa wajanja wachache.

Hivyo lengo la agizo lako halikutimizwa. Ili kuupata ukweli wa hili ni kazi rahisi tu ni kuwaita hao ma RTO watakueleza walipoelekeza hizo pesa.

Katika hili unayo nafasi nzuri ya kulifuatilia hili kwani sasa wewe ni Waziri kamili na hili lilikuwa agizo lako mwemyewe.

Mikoa hiyo ya kipolisi kwa ujumla haikosi kuwa na magari yasiyopungua 500,000 na ukizidisha kwa bei ya wastani ya 3,000x500,000=1,500,000,000. Hii ni pesa nyingi zingeweza kulisaidia jeshi la polisi. Naomba nisiwataje wahusika bali jaribu kufuatilia mwenyewe ndani ya muda mfupi utakua na majibu.

Mungu abariki utendaji wako.

ASANTE KIJANA SAWA NITALIFANYIA KAZI SWALA LAKO[emoji1319]
 
Back
Top Bottom