Ok, so hizi iPhones mpya, kuanzia 14 mpaka 16, zina uwezo wa kuwa na lines mbili.
Nina namba ya Marekani na nina namba ya bongo kupitia Vodacom.
Both numbers are active.
Nikiwa Marekani, namba yangu ya Vodacom inafanya kazi. Napokea simu, texts, n.k. Access ya M-Pesa inafanya kazi vizuri tu. Naweza kumtumia mtu hela, kupokea hela, kulipia Luku, na mengineyo.
Nikiwa Tanzania vivyo hivyo, namba ya T-Mobile inafanya kazi kama kawaida.
Nikiwa Marekani, primary line na secondary line zinatumia network ya T-Mobile. Na simu inakuonyesha juu mkono wa kushoto network inayotumika.
Nikiwa Tanzania, network inabadilika inakuwa inakuwa ya Vodacom.
Jana tu nimepokea ujumbe toka Vodacom. Huwa napokea jumbe kama hizi karibu kila siku. Nadhani system yao inapo detect kuwa eSIM yao ipo nje ya Tanzania, automatically inatuma ujumbe kama huu.
View attachment 3120466