TANZIA Waziri wa TAMISEMI Mohammedi Mchengerwa Amefiwa na Baba Yake Mzazi Akiwa Ibadani Makka Na Atazikwa hukohuko Makka

TANZIA Waziri wa TAMISEMI Mohammedi Mchengerwa Amefiwa na Baba Yake Mzazi Akiwa Ibadani Makka Na Atazikwa hukohuko Makka

Kweli kabisa ! Kufa katika ibada tukufu tena katika mji mtukufu ni alama ya mwisho mwema japo hatusemi ni kwenda peponi kwa 100%.
Kuna baadhi ya mambo hukumu yake ipo kwa Allaah anayejua mioyo ya waja wake inaamini na kufikiria nini!
Sisi tunahukumu yale tunayoyaona na yaliyomo kwenye mioyo tunamuachia Allaah mwenye uwezo wa kuchunguza mambo yenye kutendwa kwa siri na Yale yaliyomo kwenye mioyo ya waja.
Pamoja na hayo kama Kuna jambo la kionewa wivu mimi huyu marehemu namuonea wivu kwani na mimi natamani nifienkatika mji aliofia yeye nikifanya ibada aliyokuwa akiifanya yeye na hatimaye nizikwe katika mji huo mtakatifu.
Hakuna kitu kama hicho ww
 
ila Qur'an kuna namna huwa inafikirisha, hao mabikra wanaopewa maana yake itataka wafanye nao ngono,,hivi kweli ndugu zangu wavaa kobaz mtaka kutuaminisha mbinguni mahali patakatifu itakuwa ni uwanja wa kugegedana tu tena kila mtu na mabikra wake 72?
Halafu Watu weusi hawapewi bikra 72 ni waarabu tu
 
Baba yake Wazir wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mohamed Mchengerwa, Alhaj Omary Mchengerwa amefariki leo Alfajiri akiwa kwenye Ibada ya Umrah huko Makkah.

Kwa mujibu wa taarifa ya Familia ya Mchengerwa, Mzee Omary atazikwa leo huko huko Makka.

Ifuatayo ni Ratiba ya Ibada ya Visomo vitakavyoongozwa na Mufti wa Tanzania Dkt Zuberi Bin Ali wa Mbwana nyumbani kwa Waziri Mchengerwa, Masaki Dar es Salaam.

LEO: TAREHE 24 FEBRUARI 2025

Dua ya Kisomo itafanyika nyumbani kwa Mhe. Mohamed Mchengerwa Masaki saa 10 Alasiri

KESHO TAREHE: 25 FEBRUARI 2025

Dua ya kisomo itafanyika Jimboni Rufiji

KESHO KUTWA TAREHE: 26 FEBRUARI 2025

Dua itafanyika nyumbani kwake Marehemu Alhaj Omary Mchengerwa Yombo.
Apumzike kwa Amani mzee Mchengerwa.
 
Kwa sababu amefia makka atazikwa hukohuko ila angefia kwengine angesafirishwa!! Duu hii ni hatari
 
Hili Jina Mchengerwa nilikuwa nalifaham la bwana mmoja Omary Mchengerwa. Na tulikuwa tunasalimiana mara kwa mara kwa sms, kuna kipindi akija Zanzibar alikuwa anakuja ofisini kwangu. Ila ni muda mrefu sikuwa tena na mawasiliano nae...
Hii habari ya huu msiba sikuweza kuunganisha kama ndio yeye. Nilijua majina tu yanafanana
Kumbe ndie.
Allah Amjaalie pumziko jema. Inna lillah wainna ilayh rajiuun
 

Attachments

  • Screenshot_20250301_185555_Chrome.jpg
    Screenshot_20250301_185555_Chrome.jpg
    121.8 KB · Views: 2
Makka ni Mji Mtakatifu kwa Waislamu wote na kila mmoja anatamani kuzikwa katika mji Ule.
Sasa kwann labda angekufa dar es salaam angepelekwa rufiji kuzikwa? Hoja ni kwamba hakuna utaratibu wowote katika dini ya kiislam wa kumsafirisha maiti isipokuwa ni waendeleza "uzushi" wa kuwa "akazikiwe nyumbani kwao" sasa mbona imekuja issue ya makka wamemzikia hukohuko? Sasa hujaona hapo bwn mwashambwa kuwa ni mila tu isiyo na tija yoyote zaidi ya upuuzi katika dini?
 
Back
Top Bottom