Waziri wa Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa arejesha safari za ndege za Air Tanzania Dar kwenda Iringa. Nauli kuanzia Tsh 199,000 kwenda na Kurudi

Waziri wa Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa arejesha safari za ndege za Air Tanzania Dar kwenda Iringa. Nauli kuanzia Tsh 199,000 kwenda na Kurudi

Pfizer

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2021
Posts
590
Reaction score
807
Waziri wa Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa amezindua rasmi safari za ndege kupitia Air Tanzania kutoka Dar Es laam kwenda mkoani Iringa na kutoka Iringa kwenda Dar es laam huku akiitaka Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) kujiimarisha zaidi ili kuweza kuwa na ushindani.
IMG-20250222-WA0048.jpg

Prof. Mbarawa amezindua safari hizo leo mkoani Iringa katika hafla fupi iliyohudhuriwa na viongozi wa serikali, wataalamu kutoka ATCL na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Pamoja na wadau mbalimbali wa usafiri wa anga.

" Air Tanzania endeleeni kuchapa kazi hadi kampuni yetu iweze kushindana siyo tu kwa usafirishaji wa abiria bali pia kwa usafirishaji wa mizigo," Amesema Mbarawa.

Prof. Mbarawa ameiagiza menejimenti ya ATCL kusimamia weledi na uwazi katika utendaji kazi ili shirika liwe na matokeo mazuri katika nchi yetu huku akisisitiza huduma bora kwa wateja ikiwa ni pamoja na kushughulikia kwa haraka malalamiko yanayoletwa na wateja.

Pia Waziri Mbarawa ameiagiza TAA kutunza miundombinu ya uwanja ili uwanja uweze kudumu kwa muda mrefu kwani gharama iliyotumika katika ujenzi huo ni kubwa hivyo ni vema kuutunza.
IMG-20250222-WA0049(1).jpg

Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu William Lukuvi amesema kuwa kufanikiwa kwa ujenzi wa uwanja huo na ndege na kuanza safari ni mafanikio makubwa kwa uchumi wa Iringa pamoja na shughuli za utalii.
IMG-20250222-WA0017.jpg

Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL Mhandisi Peter Ulanga amesema safari za Iringa - Dar es salaam zitakuwa zikifanyika mara tatu kwa wiki yaani Jumatatu, Jumatano na Ijumaa ambapo nauli ya kwenda na kurudi inaanza shilingi laki moja na elfu tisini na tisa (199,000).

Pia Ulanga amesem pamoja na jitihada za mheshimwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kufanikiwa kwa kuanza safari hizo kumechagizwa na msukumo mkubwa kutoka kwa Waziri Mbarawa, Waziri Lukuvi, Naibu Waziri Kihenzile pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Peter Selukamba ambao kila mara walilifuatilia jambo hilo kuona linatokea.
IMG-20250222-WA0021(1).jpg
IMG-20250222-WA0019.jpg
IMG-20250222-WA0020.jpg
IMG-20250222-WA0017.jpg
IMG-20250222-WA0016.jpg
 
Wahehe nao wanapandaga ndege

Bas tu zimewashinda wanadandia maroli dar iringa ndo waje waanze kupanda ndege?
 
Back
Top Bottom