Waziri wa ulinzi Yoav Gallant asema baada ya kuipiga Iran dunia itaelewa mchakato wa maandalizi na mafunzo namna ulivofanywa na IDF

Waziri wa ulinzi Yoav Gallant asema baada ya kuipiga Iran dunia itaelewa mchakato wa maandalizi na mafunzo namna ulivofanywa na IDF

Sio biashara yangu kujua anapoishi.
Mbona umekwepa kutaja kwamba anaishi mafichoni? Kumbuka chimbuko la hoja lipo hapo post #97 na ni Hali ya Taharuki ya Kitisho na Hofu ya kuuwawa na Israel kutokana na tukio la tar. 1 Oktoba 2024 lililofanywa na Iran dhidi ya Israel.
 
— 🇮🇱/🇮🇷 NEW: Iranian officials, including two members of the IRGC, said that if Israel inflicted major harm, the responses under consideration include a barrage of up to 1,000 ballistic missiles, escalated attacks by Iranian-backed resistance groups in the region, and disrupting the flow of global energy supplies and shipping moving through the Persian Gulf and the Strait of Hormuz – New York Times

@Middle_East_Spectator
 
Mbona umekwepa kutaja kwamba anaishi mafichoni? Kumbuka chimbuko la hoja lipo hapo post #97 na ni Hali ya Taharuki ya Kitisho na Hofu ya kuuwawa na Israel kutokana na tukio la tar. 1 Oktoba 2024 lililofanywa na Iran dhidi ya Israel.
Unaongea upuuzi tu!
Kwa hoja yako hii ya kipuuzi ina maana Netanyahu naye anaishi mafichoni kwasasa, maana siku kadhaa zilizopita watu wametuma drone nyumbani kwake.
 
Iran sio Gaza.
Iran ni special case.
Kama shambulio la Iran la may US,UK na France kwa pamoja ziliisaidia Israel kudungua makombora na saba yakapita, jiulize Israel ingebaki peke yake ingekuaje!?
Iran ni taifa lenye nguvu kijeshi nguvu ambayo Israel hawezi kuimudu hata kidogo.
Hilo shambulio hakutumia Hypersonic angetumia Hypersonic wasinge angusha hata Missile moja.
 
Asante Yesu kristo mwana wa Mungu aliye hai ,,,mavaa kobazi yapigwe yachakae

Katika Injili za Mathayo, Marko na Luka, Yesu ameitwa mara 22 kwa jina la "Mwana wa Mungu", lakini hata mara moja yeye mwenyewe hakujiita kwa jina hilo.

Katika Mathayo 27.43 yanatajwa maneno ya wakuu wa makuhani wa Kiyahudi pamoja na waandishi na wazee waliokuwa wakimdhihaki, si maneno yake yeye Yesu.

Hao walikuwa wakimzulia kuwa anadai uwana wa Mungu, na anadai kuwa ni Mfalme wa Israeli.

Mara nyingi waliokuwa wakimwita Mwana wa Mungu walikuwa ama wendawazimu, wenye pepo wachafu, au askari wa Kirumi ambao tokea hapo wao ni washirikina, mapagani.

Mwenyewe Yesu alikuwa daima akipendelea kujiita mwana wa Adamu kwa Kiebrania, lugha yake, Bin Adam, yaani ni binaadamu, mtu tu.

Katika Injili jina hili la Yesu kuitwa mwana wa Adamu limetajwa yapata mara 80.

Mahasimu zake wa Kiyahudi walimzulia kuwa alidai kuwa ni Mfalme wa Mayahudi ili kumchongea kwa watawala wa Kirumi, na kuwa alidai kuwa ni Mwana wa Mungu ili apate kuchusha kwa Mayahudi.
 
Huyu mzee atajifia tu mwenyewe bila hata ya risasi au drone kutumika. Ni katika Hofu kuu umauti utamkuta. RIP in advance.
Netanyahu hata akiwa na majeshi yake anavaa bullet proof 10 utafikiri ni kiboko , Hivi anaogopa kitu gani na yeye kwanza ni Mteule wa Mungu , pili ni Mteule wa Marekani na silaha zote unazozijua alizonazo Mmarekani kapewa , Hofu ya kitu gani ??
 
Israel nyie bado mnamini atagusa Iran ikiwa Lebanon kisha badilisha tune anataka maongezi wakati mwanzo alisema bila Hezbullah kuondoa majeshi yake yarudi 10km kutoka mto Letan basi hasimamishi vita. Leo anatoa kali eti target yake ilikuwa kumuwa Nasurlah 😄

Alipo anza vita lazima Hezbullah iwe disarmed au mimi taingia kumaliza kazi hio. Alipo ingia vita bila kurudisha wananchi wake North hasimamishi vita. Niliwambia mkisha muona Blinken na Amos Hochstein yule top advisor wa US President Biden wapo middle-east, ujuwe wanakuja muokoa mtoto wao kashindwa vita.
 
S
Ingekuwa Syria au Gaza imeishambulia Israel mara mbili mfululizo bado wangekuwa na vikao kama vya send off kila siku?
Acha kushikiwa akili fungua ubongo wako kwamba Iran ni mkubwa mno kwa Israel ndio maana unaona kila siku Israel anakuja na mipasho bila vitendo.

Hivi dunia ya leo bado mtu unaamini katika propaganda? Yaani mtu atwangwe mara mbili kipigo kitakatifu halafu asirudishe majibu bado unaaminishwa propaganda dhidi ya ukweli?

Ama kweli maajabu kamwe hayawezi kwisha duniani. Israel na mabwana zake wanaujua moto wa Iran ndio maana wanajadiliana hawafikii mwafaka kwasababu inaweza kuwa zahma kubwa kwa Israel akijaribu kujibu.
Sasa mkuu siku wakijibu utasemaje!?...maana hata Irani aliposema atalipiza kisasi dhidi ya Israeli wapanda Israeli walisema kama unavyosema wewe sasa.Swali ni je,unadhani hata wairani wana ona kama hizo ni propaganda tuu!? Au wanahaha!?au unadhani kilicho mpata yule kiongozi wao kwenye helkopta!?wana kichuliaje na je walikitarajia!?
 
Israel inajitahidi kuionyesha dunia haikubali kudhalilika na kuonekana mnyonge mbele ya Tehran lakini ukweli ni kwamba Israel ni wadogo kivita kwa Iran.

Tatizo ni kwamba Iran ilivumilia uchokozi wa Israel kwa muda mwingi na Israel ikadhani inaogopwa ikaendelea na uchokozi na mauaji lakini sasa Iran imeona njia bora ni kulipiza kisasi kwa kila uchokozi anaofanya Israel.
Israel ndo inayo fadhili HAMAS,HOUTH,HEZBOLAR na vikundi vingine vya kigaid?
 
Binafsi nimejiwekea kukipa muda kila kitu; kuweka akiba ya maneno wakati mwingine ni muhimu sana. As far as I know; Israel and Iran they know each other. Iran haiidharau Israel kama sisi tunavyo fanya hapa wala Israel haiidharau Iran kama baadhi yetu tulivo humu ndani; nina sababu ya kusema hivo; unadhani why Iran inamuhamisha hamisha Ayatollah maeneo ya kuishi kila siku? Why wamemuhoji sana CDF wao and like kapumzishwa kazi yake ya ukuu wa majeshi? Again unadhani why Iran anaendelea kuitumia Lebanon kama shield na haendi mwenyewe front? Ni makosa sana kudhani kwamba Israel anaiogopa hivo Iran wakati ameua watu wake muhimu sana kwenye ardhi yake tena jijini Tehran, zipo habari kwamba hata their former president wao Israel ndio wamemuua kwa kutumia zile simu za analogy, kaua wana sayansi wake wa nuclear pale pale Tehran; unawezaje kumdharau huyu mtu? Again, nipo kinyume sana na wanao idharau Iran kwa Israel, Iran karusha makombora kadhaa jijini Tel avivu (zamani Yafa ) na Israel hajachukua hatua kwa haraka; narudia, Iran na Israel wanajuana in and out. Tujipe muda; huenda bei ya mafuta ikapanda tena yaani
Mkuu unaonekana una utulivu na ukomavu mkubwa wa akili.
 
hawana ubavu huo, Hamas mpaka leo wameishindwa, mwaka unakatika. Hawajaweza kuokoa mateka wao.


Lebanon ndiyo wamingia cha kike. Wakiigusa Iran safari hii, Itran wameshatangaza, ndiyo itakuwa mwisho wa mazayuni duniani.
Kuhusu mwisho huo mpango walishawahi kuwa nao mataifa mengi hasimu ya Israeli lakini walishindwa tena kwa vitendo.Nikweli kwamba tunaichukia saana either Israeli au Irani lakini uhalisia utaamua hizi kaulihisia tunazo ziita na kuaminii kwamba ndio UKWELI.
 
Sio kwamba Iran ni kubwa kuliko Israel bali wanaoima implication. Tatizo la Mashariki ya kati ni Iran na Marekani. Marekani imeacha wajibu wake wa kuwa Kiranja kama zamani pengine kutokana na kuwa na viongozi dhaifu. Hali hii imempa nguvu muajemi kuwekeza sana kwenye silaha. Kama Marekani ingekuwa bent na Israel hii vita ingeshaisha. Lakini Marekani imekuwa kikwazo kwa Israel. Ndio maana katika siku za karibuni Israel iliamua kuchukuwa hatua yenyewe bila kuijulisha Marekani. Mathalan kuingiza jeshi eneo la Rafa Marekani hakutaka lakini Israel ikaamua na ikafanikiwa. Kuwaua viongozi wa Hamas ni maamuzi ya Israel yenyewe bila kuijulisha Marekani.
Sasa hili la kulipa kisasi kwa Iran lilikuwa limepangwa na Marekani kujulishwa. Matekani ikalikisha taarifa kwa Iran. Kwa hiyo kwa sasa Israelbhawezi kushambulia hadi kwanza ifanye kazi ya ziada na kutoijulisha Marekani wala mtu mwingine. Shambulizi litafanywa ghafla na hayo mataifa yatajua kuwa Israel hana mchezo pale watu wake wanapouwawa au maslahi yake kuharibiwa. Hivyo, tulieni tu mtakuja kuona!
Acha uongo, Israeli hana ubavu wa kuishambulia Iran bila msaada wa marekani. Israel hawezi hata kuwashinda Hezbollah bila ya msaada wa magharibi
 
Israeli hawana kitu, hata mipango ya Israel kuishambulia iran inafanyika marekani. TUMELISHWA MATANGO POLI MENGI SANA KUHUSU ISRAEL
 
Netanyahu hata akiwa na majeshi yake anavaa bullet proof 10 utafikiri ni kiboko , Hivi anaogopa kitu gani na yeye kwanza ni Mteule wa Mungu , pili ni Mteule wa Marekani na silaha zote unazozijua alizonazo Mmarekani kapewa , Hofu ya kitu gani ??
Hakuna asiyeogopa kifo. Hata Yahya Sinwar alichukua tahadhari dhidi ya kifo ila basi tu Umauti ulimfika.
 
Mbona umekwepa kutaja kwamba anaishi mafichoni? Kumbuka chimbuko la hoja lipo hapo post #97 na ni Hali ya Taharuki ya Kitisho na Hofu ya kuuwawa na Israel kutokana na tukio la tar. 1 Oktoba 2024 lililofanywa na Iran dhidi ya Israel.
na benjamini nae anaishi wapi?mbon juzi tu hap nyumba yake ilipigwa na yeye hakuwepo au alienda dukani kwa mangi kununua kiberiti...hata benjamini nae anaishi kimitego chini ya ardhi coz anajua silaha za Iran zinaweza kupiga popote ndani ya Israeli
 
na benjamini nae anaishi wapi?mbon juzi tu hap nyumba yake ilipigwa na yeye hakuwepo au alienda dukani kwa mangi kununua kiberiti...hata benjamini nae anaishi kimitego chini ya ardhi coz anajua silaha za Iran zinaweza kupiga popote ndani ya Israeli
Wote ni mwendo wa "leopard crawl"
 
Back
Top Bottom