Hii ndiyo hoja ya uwongo. Eti Israel haina bjeti ya vita!! Huo ni uzushi. Marekani inaweza kuisaidia Israel wakati wa vita lakini haimanishi Israel haina bajeti.
Dah mkuu unajitahidi kuipambania Israeli kweli Kweli ila sijui kwa faida gani!
Inafikia kipindi mpaka unajaribu kulazimisha nyekundu iwe njano, lkn inashindikana kwa sababu uongo hauwezi kuwa ukweli, na ukweli hauwezi kuwa uongo.
Kama upo sawasawa kabisa, jibu yafuatayo:
1. Mwaka 1978 wakati Tanzania inapigana na Uganda tulisaidiwa na Cuba, je, hatukuwa na bajeti?
Tofautisha kusaidiwa na kupewa.
2. Urusi na vita yake na Ukraine, inasaidiwa na North Korea, Iran na wapiganaji toka mataifa ya Mashariki ya kati, je, Urusi haina bajeti?
3. Iran wakati wa vita yake na Iraq, ilikuwa ikisaidiwa na Israel, je, Iran haikuwa na bajeti?
5. Sasa hivi Ukraine inasaidiwa na Ujerumani, Ufaransa na Uingereza, je, Ukraine haina bajeti?
6. UAE imekuwa ikisaidiwa na Israel wakati wa mashambulizi ya Iran , je, UAE haina bajeti?
Kwanza hayo mataifa mawili, Marekani na Israel yana mikataba mingi ya ushirikiano kwenye ulinzi na tekinolojia za vifaa vya kivita, ambapo kwenye mikataba hiyo kila upande una haki ya kutumia silaha zilizopatikana kupitia hiyo miradi ya utafiti kwa kulipia gharama za utengenezaji.
Si rahisi sana Israel kutengana na Marekani. Trump na Netanyahu wanaweza kutoelewana, lakini hiyo haimaanishi ushirikiano kati ya Israel na Marekani, umeisha.
Hata Biden hakuelewana na Netanyahu, kiasi cha Marekani kugoma kuwauzia silaha Israel , lakini alipokuja Trump, mambo yakawa tofauti. Kwanza silaha nyingi toka Marekani kwenda Israel, hazitolewi bur
Habari ya uwongo hii. Yawezekana pia inasababishwa na uwezo mdogo wa mlrmeta mada kwenye lugha za kigeni.
Huyo waziri hajanyimwa visa, bali ni yeye amefuta trip ya familia yake kwenda USA baada ya familia yake kuambiwa kuwa ni lazima yeye aende akachukuliwe alama za vidole. Akachukulia kuwa huo ni udhalilishwaji na usumbufu, akaamuru familia yake iachane na mpango wa kwenda USA.
Itamar Ben-Gvir was not formally denied a visa, but he canceled his planned family trip to the United States after the U.S. Embassy made the unusual demand that he appear in person to provide his biometric fingerprints.
Hapa hakuna swali la msingi hata moja