Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,390
- 152,301
WAZIRI wa Nchi, Ofi si ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mohamed Mchengerwa, amesema serikali haitomvumilia mkuu wa idara katika taasisi ya umma atakayesababisha mtumishi akose stahili yake au mwananchi kukosa huduma bora.
Mchengerwa amesema hayo Dodoma wakati akifungua Kikao Kazi cha Mwaka cha Wakuu wa Idara za Utawala na Rasilimaliwatu Katika Utumishi wa Umma.
Aliwataka wakuu hao kutekeleza majukumu yao kikamilifu ili kutekeleza agizo la Rais Samia Suluhu ambaye ameelekeza viongozi katika taasisi za umma kutenda haki kwa watumishi walio chini yao na wote kutoa huduma bora kwa wananchi.
Mchengerwa alisema atakapofanya ziara katika maeneo yao, hategemei kukuta foleni ya wananchi wakisubiri huduma.
“Mimi, Naibu Waziri wangu na watendaji wa ofisi yangu tukifanya ziara katika taasisi yako, hatutegemei kukuta foleni ya wanananchi wakisubiri huduma pasipo na matumaini,” alisema.
Mchengerwa alisema ameanzisha mfumo wa kielektroniki unaoitwa ‘Sema na Waziri wa Utumishi’ unaotarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni ili kutoa fursa kwa watumishi na wananchi kuwasilisha malalamiko.
“Kupitia mfumo huu, nitakuwa na uwezo wa kuona malalamiko yanayowasilishwa popote nitakapokuwa na kufanya ufuatiliaji wa namna yalivyofanyiwa kazi na ofisi yangu,” alisema.
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Festo Dugange, alisema Rais Samia amekuwa akisisitiza mara kwa mara matokeo chanya katika utekelezaji wa majukumu ya watumishi kwenye maeneo yao ya kazi.
Alisema ili matokeo hayo yaonekane, wakuu wa idara za utawala na rasilimaliwatu wanapaswa kusimamia utekelezaji wa majukumu ya watumishi wa umma kwa ufanisi.