Waziri ya Afya, Kwa Sasa mama mjamzito kadi ya clinic anauziwa 10,000. Akijifungua mtoto wa kike 15,000 wakiume 30,000

Waziri ya Afya, Kwa Sasa mama mjamzito kadi ya clinic anauziwa 10,000. Akijifungua mtoto wa kike 15,000 wakiume 30,000

Sio huko tu mkuu.
Hospitali nyingi wanauza kadi za clinic.
Nilishuhudia hii Chanika hospitali ya nguvu kazi. Wanaambiwa kadi zimeisha na kuelekezwa sehemu ya kwenda kununua, nje ya jengo la hospitali.
Hiyo inayonunuliwa imeandikwa "Haiuzwi'
Hii nchi kwa sasa ina ujinga mwingi wakutojali.
Tunahitaji waziri na wizara yake ya Afya watuambie kwann kadi iandikwe haiuzwi na Bado inauzwa!?
 
Wewe Kwa nini ulitoa buku 10 badala ya kumripoti huyo mtumishi asiyekuwa mwaminifu?

Pia Nape atueleze inakuaje vocha imeandikwa 500 then inauzwa 600 Kwa maelezo ya kinyemela?

Mwisho kama gharama zinapanda taarifa itolewe,binafsi huwa sitoa kama ninajua hiyo gharama sio ya kulipia unless nihakikishiwe kwamba zimeisha na huwezi subiria Serikali Hadi ilete ndio wanapitia humo humo maana hapo utakuata karibu wateja wote wameuziwa huwezi kubisha.
Mkuu soma vizuri aliesababisha nikajua ni muhanga mwingine sio Mimi na nikauliza watu kadhaa ndo wakaniambia na hiyo tofauti ya bei ya kuzaa mtoto wa kiume na wakike.
 
Hatu
No ujinga Kwa Watanzania kuendelea kulalamika kana kwamba hamjui Ofisi za Viongozi au TAKUKURU.

Watumishi wasio waaminifu wako Kila sehemu ingawa kweli zinaweza kuwa zimeisha na Huduma lazima ziendelee hapo no way out maana mnazaana hovyo na Kwa Kasi sana kiasi kwamba mahitaji yanaongezeka Kwa Kasi kubwa
Hatukatai kununua wao waandike tu kadi hii inauzwa Tsh10,000/=

Pili watuambie utofauti wa gharama kati ya kuzalisha mtoto wa kike na wakiume. Tofauti hiyo inatoka wapi?
 
watanzania wengi wanshindwa kuzijua haki zao
watanzania hatuna umoja kwenye kuitaka haki utalia mwenyewe likikukuta tumejawa tamaa na uwoga

mimi apo kwenye bei tofauti ndokumenimaliza nikama viingilio regular na vip😃
Inasikitisha sana
 
Mimba sio dharula, ni maandalizi na unakaa na ujauzito miezi 9, changia huduma kwa maendeleo yako na afya ya mtoto wako, Watanzania tubadilike maana hakuna kitu cha Bure.
Sasa kwanini serikali ijifiche kwenye kuwatangazia watu kuwa huduma ni bure mtu akiwa anajua ni bure aende na pesa kidogo. Isifiche na wakati mwingine waziri kutoka huko aendelee kusisitiza kuwa kitu fulani ni bure, waseme wazi kuwa huduma zinalipiwa basi watu wajue. Mbona huduma ambazo wananchi wanajua zinalipiwa mfano maji au luku hakuna anaye zidemand bure. Serikali kusema uongo ndipo shida ilipo waseme wazi wazi kuwa huduma kwa wajawazito zinalipiwa, waseme kuwa elimu si bure. Waache kudanganya kwa ajli ya manufaa ya kisiasa.
 
Back
Top Bottom