Waziri ya Afya, Kwa Sasa mama mjamzito kadi ya clinic anauziwa 10,000. Akijifungua mtoto wa kike 15,000 wakiume 30,000

Tunahitaji waziri na wizara yake ya Afya watuambie kwann kadi iandikwe haiuzwi na Bado inauzwa!?
 
Mkuu soma vizuri aliesababisha nikajua ni muhanga mwingine sio Mimi na nikauliza watu kadhaa ndo wakaniambia na hiyo tofauti ya bei ya kuzaa mtoto wa kiume na wakike.
 
Hatu
Hatukatai kununua wao waandike tu kadi hii inauzwa Tsh10,000/=

Pili watuambie utofauti wa gharama kati ya kuzalisha mtoto wa kike na wakiume. Tofauti hiyo inatoka wapi?
 
watanzania wengi wanshindwa kuzijua haki zao
watanzania hatuna umoja kwenye kuitaka haki utalia mwenyewe likikukuta tumejawa tamaa na uwoga

mimi apo kwenye bei tofauti ndokumenimaliza nikama viingilio regular na vip😃
Inasikitisha sana
 
Mimba sio dharula, ni maandalizi na unakaa na ujauzito miezi 9, changia huduma kwa maendeleo yako na afya ya mtoto wako, Watanzania tubadilike maana hakuna kitu cha Bure.
Sasa kwanini serikali ijifiche kwenye kuwatangazia watu kuwa huduma ni bure mtu akiwa anajua ni bure aende na pesa kidogo. Isifiche na wakati mwingine waziri kutoka huko aendelee kusisitiza kuwa kitu fulani ni bure, waseme wazi kuwa huduma zinalipiwa basi watu wajue. Mbona huduma ambazo wananchi wanajua zinalipiwa mfano maji au luku hakuna anaye zidemand bure. Serikali kusema uongo ndipo shida ilipo waseme wazi wazi kuwa huduma kwa wajawazito zinalipiwa, waseme kuwa elimu si bure. Waache kudanganya kwa ajli ya manufaa ya kisiasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…