Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 34,256
- 44,597
Na. M. M. Mwanakijiji
Mashtaka ya tuhuma za Uhaini dhidi ya Tundu Antipas Lissu hadi yalipofikia sasa hivi yanatuelekeza kuwa mashahidi wa viti vya mbele vya mashtaka ya Tundu Lissu dhidi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano. Japo kesi hii imeletwa na watawala katika jitihada za kumnyamazisha Tundu Lissu na kufifisha harakati za kudai mabadiliko ukweli ni kuwa kwa kuendelea na kesi hii kibano kitageuzwa kwao.
Uamuzi wa TAL kuendelea kujitetea yeye mwenyewe bila kutegemea mawakili wake au yule aliyepewa na serikali ni uamuzi wa kimkakati (a strategic maneuver), wa kuchokoza (provocative), na wenye makusudi (intentional). Ni uamuzi wa kimkakati wa kuifanya kesi hii kuwa ni kulazimisha serikali iseme kweli kabisa kuwa ina lengo la kumnyonga Lissu kwa kosa la uhaini, ni wa kiuchokozi kwa sababu unajaribu kuigusa Mahakama Kuu ya Tanzania kuona kama kweli kwa uzoefu wake inaweza kumkuta kweli na hatia ya uhaini kwa ushahidi utakaoletwa mahakamani na wa makusudi kwa sababu mwisho wa siku mfumo wetu wa kisheria unawekwa kizimbani.
Bahati nzuri historia imejaa mifano lukuki ya serikali ambazo zimejaribu kuzima harakati za mabadiliko kwa kutumia nyundo ya mahakama. Mfano bora zaidi ni kesi ya Rivonia kule Afrika ya Kusini ambapo iliishia kwa kumhukumu Nelson Mandela na wenzake hukumu ya kifungo cha miaka 27 jela kwa kosa ambalo lilitishia hukumu ya kifo. Ni katika kesi hiyo Nelson Mandela alitoa hotuba ambayo inatajwa kuwa miongoni mwa hotuba bora zaidi kutolewa katika karne ya 20. Hotuba ya "Niko Tayari Kufa" ilianisha sababu ya kwanini Nelson Mandela na wenzake walikuwa tayari kutumia nguvu kupinga utawala wa kikaburu.
Tundu Lissu amejenga hoja zake toka Kisutu. Utetezi na hoja alizozitoa hadi hivi sasa hazijajibiwa. Pendekezo langu kwake ni kuwa awaache serikali waendeshe mashtaka dhidi yake bila kusimama kujitetea. Asiwape uhalali (legitimacy) ya kujitetea mbele ya Mahakama Kuu. Kama wao wana ushahidi wa kutosha awaache waendeshe kesi yao. Walete mashtaka yake na awalazimishe wamkute na hatia. Asubiri tu kutoa 'closing argument". Lakini awaache waendeshe mashtaka yao wao wenyewe....
Awe mfungwa wa kisiasa per excellence.