Wazo Gomvi: Kabla ya Kujitoa CHADEMA Ingeeleza Hili Kwanza...

Nonsense
 
Hivi CCM waleenguliwa wangapi ? vilena kama wote wamepita inaingia akilini?. Mi nijuavyo mazingira waliko wagombea yanafanana mfn elimu waliyopata , vijiji, vitongoji na mitaa e
walipo iweje CCM wao wawe smart 100%?.
 
 
mzee unanongwa kwelikwe
ukumbuke hata ma
shida yako unajifanyaga una akili nyingii. nakukumbusha tu kwamba hata MAKABURU walijenga madaraja na mabarabara, hospitali mpaka umeme wa neuclear lakini walipingwa kwasababu walibinya uhuru wa watu kamma MAGUFULI.
Mwaka jana nilikuwa kwenye jimbo moja la uchaguzi huko mkoani pwani. nikiwa pale madiwani wawili walipewa ml 5 kila mmoja ili watangaze kuunga mkono juhudi.
kwenye uchukuaji fomu DED na OCD walikwenda kujificha mahali na kunywa pombe tangu asubuhi na DED alimwambia mhasibu wa mapato asifike kabisa ofisini ili wakirudisha fomu wasipate pa kulipia mhasibu akaondoka na kuzima simu
 
Mikutano ya siasa ni marufuku, Polisi wanasimamia vema na wapo watu mahabusu! Hujui hilo?
Tuelewane mkuu tusije tukakwazana bure.

Yote hayo ya kunyimwa nafasi za kufanya shughuli a kisiasa na mizengwe yote inayofanywa na serikali hii naielewa na ninaipinga kwa nguvu zote.

CCM na Magufuli hawana hati miliki ya nchi hii, na kwa maana hiyo ndio sababu wanastahili kupingwa kwa njia zozote na watu wote wasiopenda hali hiyo. Na kwa hivyo basi, hatuwezi kukaa chini na kusema kwa kuwa tunanyimwa haki yetu, basi tumwachie Mungu. Ni wajibu wetu kuitafuta haki yetu kwa kila njia inayowezekana. Haki mara zote ikinyimwa, ni lazima itafutwe hata kwa njia zisizo za staha.

Kwa hiyo hapa unaponijibu ni kana kwamba kwa kuwa CHADEMA wamekatazwa mikutano, basi ndio iwe mwisho wao wa kufaya liwezekanalo lolote kuwafikia wananchi huko vijijini?

Huko mitaani CHADEMA haina viongozi wanaowasiliana na viongozi wenzao wa ngazi za juu hadi Makao makuuKama njia hizo zipo, kwa nini mikakati isifanyike siasa zikaendeshwa huko mitaani hata bila mikutano ya hadhara?

Tusing'ang'anie hapa hili wazo la kukatazwa kufanya mikutano ndio iwe sababu ya kutofanya siasa. Hili mimi sikubaliani nalo na lisiwe ndio sababu kuu ya kuhalalisha udhaifu wa hivi vyama vya upinzani.

Unaponyimwa haki huwezi kukaa chini na kutulia. Utatafuta njia mbadala ya kuirudisha haki yako.
 
Miongoni mwa maswali mazuri sana haya; maana upande wa swali hilo ni kuwa inawezekana vipi wale wa CCM "waonekane" wamejaza fomu zao kwa usahihi yaani hata mmoja asienguliwe?
Haya yote tunayojiuliza hayaondoi wajibu wa vyama katika kusimamia maandalizi ya wagombea wao. Mimi bado ningependa kujua 'support' wanayotoa kwa wagombea wao katika harakati kama hizi, na hasa tukifahamu vizingiti vinavyowakabili.

CHADEMA na wenzao ACT-Wazalendo watakuwa wamejiimarisha sana wakiwa na nguvu huko mashinani. Huko ndiko kunakotakiwa kufanyiwa kazi kubwa.
 
Mimi sikubaliani kabisa na huo "ujuha na ulaghai" wa wapuuzi kama Polepole.

Bila kujali CCM wamefanya nini, ni wajibu wa Vyama vya upinzani kushirikiana na wagombea wao kwa njia mbalimbali na panapohitajika, kutoa msaada kwa hao washiriki. Je hivi vyama vimefanya hivyo? Hili ndilo mimi ningependa kujua.
 

..ndugu yangu Kalamu 1, sidhani kama cdm wametulia tu na kuacha kufanya shughuli za kisiasa.

..wamefurukuta, na wamejitahidi, na juhudi zao ndiyo zimepelekea au.zimezaa matokeo haya.

..[hujuma, makatazo, ukatili wa ccm] + [ juhudi, kufurukuta, kujitutumua kwa upinzani] matokeo yake tunayoyashuhudia ktk mchakato wa uchaguzi.

..Now, do we like what we are seeing?

..Does this guarantee a better future for our country?

..Kwa maoni yangu, ni vizuri tukavaa koti la watu wazima wanaoangalia ugomvi wa watoto wawili.

..Kuna wakati watu wazima huwaacha watoto wabamizane, ili wapate kujifunza, lakini hali ikikaribia kuwa mbaya ugomvi huamuliwa na watoto hao husuluhishwa.

..Nadhani kwa hapa tulipofikia ni busara zaidi kusema INATOSHA. Ni vizuri sasa vyama vya siasa vikakaa pamoja na kuazimia kufanya siasa kwa kuzingatia HAKI SAWA kwa vyama vyote.
 
FAIR ENOUGH.

Siwalaumu CHADEMA na ACT-Wazalendo kujitoa kwenye uchafuzi. Ninawaunga mkono kwa hatua hiyo. In fact, hiyo ni sehemu ya mapambano. Na ili mapambano haya yawe na nguvu, ni lazima wananchi wawe karibu na vyama hivi. Waelewe maana ya mapambano haya.
 


TATIZO CCM BADO HAWAJAPATA JIBU LA HAYA MATENDO YAO YA KIGAIDI.

Wanawaona wapinzani ni kama mashoga , sheria wazitunge wao, Tume waweke wao , kesi wabambikiwe wapinzani , huku ni kuhanisiwa na kutiwa vidole.

Ni Lazima ili kupatikana haki watu wajitolee .

Haki katu haiwezi kupatikana kama sahani ya ugali ya mama ntilie
 
.Nadhani kwa hapa tulipofikia ni busara zaidi kusema INATOSHA. Ni vizuri sasa vyama vya siasa vikakaa pamoja na kuazimia kufanya siasa kwa kuzingatia HAKI SAWA kwa vyama vyote.
Hili silioni likitokea chini ya CCM hii na Mweyekiti wake. Tuwe wakweli tu.
 

Kukaa nasoma uzi wa jitu nafiki kama hili ni blasphemy!
 
Hili silioni likitokea chini ya CCM hii na Mweyekiti wake. Tuwe wakweli tu.

..Why not?

..kama ni jambo jema na litakaloleta heri na amani kwa nchi yetu kwanini lisifanyike?

..Je, tunatoa wapi uhalali wa kujiita WAZALENDO?
 

..Uhuru tuliupata bila kumwaga damu.

..sidhani kama Mwalimu Nyerere aliwahi kusumbuliwa na kudhalilishwa na wakoloni kama wanavyofanyiwa viongozi wa upinzani ktk awamu hii.

..ccm wasilazimishe waTz kumwaga damu.
 
..OK.

..but do we have a guarantee that the situation will get better, or at least remain as it is?

..huu uhasama, uadui, na chuki, inayopandikizwa na ccm, watoto wetu watakuja kuishi namna gani?
It can only get worse under the current leadership. Let's hope I'm wrong!
 
Mkuu Kalamu1 naomba nikiri ukweli nilioushuhudia kwa macho yangu kwenye maeneo kadhaa.

Kwanza nikweli kwamba kwa sehemu upo uzembe flani kwa Wapinzani hususani CHADEMA kufanya usaidizi madhubuti kwa wanachama wao juu ya namna sahihi ya ujazaji wa fomu hizo ili wasitoe loopholes/mianya ya kukatwa majina.


Lakini pamoja na Ukweli huo kwa macho yangu kuna maeneo kadhaa nimeshuhudia baadhi ya Wagombea wamejaza kwa usahihi Sana chini ya usaidizi wa viongozi wao lakini yet wameenguliwa kwamba hawajajaza "kwa usahihi" fomu zao while wa chama tawala wao hakuna hata mmoja aliyeenguliwa kwa sababu sawa na hizo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…