Wazo: Je, tunaweza kuifuta form six? Yaani Mwanafunzi akianza form one (Non-stop) aende mpaka form five, alafu anajiunga na chuo?

Wazo: Je, tunaweza kuifuta form six? Yaani Mwanafunzi akianza form one (Non-stop) aende mpaka form five, alafu anajiunga na chuo?

Good Afternoon my dear brothers and sisters out there.

Eti wadau, tunaweza kufuta form six?? Mwanafunzi akianza form one, aende mpaka form five (Non stop) alafu chuo??

Yaani tunaua mitihani ya form four pamoja form six. Mtihani wa Secondary unakuwa mmoja tu wa form five.

Karibu kwa mjadala na pia ninakaribisha Ukosoaji wenye tija (Constructive Criticism) pasipo kutumia lugha za matusi wala kejeli.

Ni mimi,

Alex Muuza Maembe.
======
Asante kwa mada yako mdau. Lakini napata ukakasi kuweza kuchangia mada yako, kwa sababu umetoa tu mapendekezo lakini haujasema ni kwanini unataka hayo mabadiliko. Na pia hujasema umeona changamoto gani kwa mfumo wa sasa hata ukakupelekea wewe kuja na mapendekezo hayo. Nikipata hayo mambo nitakuja kuchangia.

Karibu uboreshe mada yako ili ilete maana. Natanguliza shukurani.
 
Mkuu, Alex Muuza Maembe Hujaona hapa.?
 
Asante kwa mada yako mdau. Lakini napata ukakasi kuweza kuchangia mada yako, kwa sababu umetoa tu mapendekezo lakini haujasema ni kwanini unataka hayo mabadiliko. Na pia hujasema umeona changamoto gani kwa mfumo wa sasa hata ukakupelekea wewe kuja na mapendekezo hayo. Nikipata hayo mambo nitakuja kuchangia.

Karibu uboreshe mada yako ili ilete maana. Natanguliza shukurani.
Sawa mkuu. Ngoja nikipata muda nitaifanyia maboresho mada hii kwa manufaa mapana ya mfumo wetu wa elimu..
 
Kidogo huwa inawapa mwanga wakifika Chuo kikuu

Waliosoma hizo Kombi wanajua Advance imewasaidiaje baada ya kufika chuo
Mkuu, sio kila atakachokutana nacho mwanafunzi chuoni basi kina uhusiano na masuala ya A level. Hapana. Kuna baadhi ya mambo chuoni ni mageni mno kwa mwanafunzi aliyetokea secondary..
 
Mkuu, sio kila atakachokutana nacho mwanafunzi chuoni basi kina uhusiano na masuala ya A level. Hapana. Kuna baadhi ya mambo chuoni ni mageni mno kwa mwanafunzi aliyetokea secondary..
Waliwaanzishia QT sababu ndio hizo unapiga 1&2 mwaka mmoja 3&4 mwaka mmoja na 5&6 mwaka mmoja umemaliza yule unaenda chuo chapu miaka 3 tu
 
What is the motive?
Where are objectives?

Au lengo ni kufuta tu, Vitoto vya saiv vnamaliza first degree at 23 wakiwa wadogo, hawaja mature, kimwili wala kiakil leo hii mnataka wamalize na miaka 21 waende wapi?
 
NILISHA SEMA HAPA KUWA A-LEVEL yote ifutwe .. sema tatizo nchi imejaa viongozi mazuzu ...primary miaka 8 secondary miaka 4 kwisha ...kinacho takiwa kwa primary ni kuwa na primary advance yaani darasa la 7 na la 8 liwe sawa na form 2 ya sasa..
Faida ni ngingi kufanya hivi

1)ingeondoa obwe la kisaikoloji linalo wafanya wanafunzi kuchoka shule kwa kuona kuna A level baada ya kumaliza O level...hivyo wanafunzi wangesoma kwa bidii sana wakijua wakimaliza miaka 4 ya secondary ni Chuo moja kwa moja.

2)shule zote za ALevel zingegeuka kuwa O level na kuongeza idadi ya shule.

3)inge ondoa usumbufu wa wanafunzi kutafuta shule za A level maana zitakuwa hakuna.

⁴)walimu wote wa A level wange jiunga pamoja na O level na kuongeza idadi ya walimu

5)ingepunguza gharama za serikali kwenye mambo ya mitihani kwa kuondoa form 6 ...
Faida ni nyingi sana
Mkuu At Calvary umemsoma huyu ndugu yetu hapa??..
 
Inawezekana hata hiyo form v isiwepo kabisa mwisho iwe form iv kama majirani zetu kenya
Kenya wapo sahihi kabisa ...vyuo vyetu wanaingia wa mama na kufanya mambo ya ajabu umri mkubwa wamesha choka shule kutokana na mlolongo mrefu wa elimu...
Primary 8 yrs
Secondary 4 yrs
Chuo....kazi kwisha tatizo ccm ni wapumbavu
 
Back
Top Bottom