Ukiwaambia Watanzania tatizo letu linaanzia kwenye malezi ya watoto, turekebishe kuanzia huko, sio kumuangalia rais wa leo tu, utapata watu wachache sana watakaokubali hilo na kulifanyia kazi.Shida kubwa kwetu Watanzania ni kutoa lawama kwa jambo fulani,bila kufanya tafiti ya kina juu ya chanzo chake ni kipi?
Kuna rafiki yangu mmoja aliwahi niambia "utafanyaje siku ukigundua kwamba wewe ndo chanzo Cha tatizo"Watanzania tujitafakari,haya tuonayo kwa viongozi wetu ni zao letu wenyewe.
Mungu anakataza kuua, kufadhili wauaji.Tofauti na yule, huyu mcha Mungu
Hadithi za Kizimkazi hizo, kwanini asiwapeleke Mahakamani?Twtizo la kupikwa na wasioitakia mema Tanzania. Waliokaa kikao ngulelo kupanga uhaini, usaliti na ugaidi ndio tatizo.
MUNGU gani huyo??Tofauti na yule, huyu mcha Mungu
Ni uchumi upi huo unaongea? Lete data. Ukitaka kuengelea inflation imezidi, unemployment ni zaidi ya 40%, ukiongelea wawekezaji sioni mwekezaji gani huyo wa maana toa reference. Impact ya economic growth ya sasa hivi na kukua kwa GDP kama kutatokea ni kutokana na infrastructure investment zile za Bwawa ambalo litatoa impact kubwa, meli zilinunuliwa, ndege zilinunuliwa na viwanja vya ndege vilijengwa, SGR, Makao makuu nk. Huyu kaleta nini kipya? Kukodisha Bandari kwa DP world na kuwandoa wamasai mbugani ndiyo investment kubwa?Nilikuwa wa kwanza kusema Mama arudishe siasa za kuwashughulikia Wapinzani bila kuingiza mambo hayo kwenye uchumi.
Mifano Iko Mingi sana kuanzia Uganda,Rwanda,Egypt,China nk.
Bwana wako yule alikuwa haelewi yeye akaleta chuki zake Hadi kwenye Uchumi,Hali ikawa mbaya wawekezaji wakakimbia, account zikaanza kufungwa ,watu kubambikiwa Kodi Kwa sababu pesa imepungua na Biashara kukaba kiasi kwamba vilio vya vyuma kukaza vilitamalaki.
Rais awashughulikie Wanasiasa uchwara na vibaraka wote ila silete siasa za ujamaa hapa.
Mwisho kama unaembeba habebeki unategemea uendelee kumbeba? Una mdamp tuu unasonga mbele mwenyewe.
Well SaidBora bwana yule alifariji wananchi, wakampenda na kumuona ni mkombozi wao, huyu wa sasa hata upande wa " wanyonge hayupo"
Nchi hii kipindi cha bwana yule ilikuwa ina muelekeo chanya hasa ile falsafa ya kazi kazi.
Mama mtu amepwaya hasa kwa wananchi wengi hawampendi,anapendwa na chawa wake tu.
Nafikiri Kumfananisha Nchimbi na Rais wa Nchi ni kosa kimkakati.Mama mbona wasiwasi wake tu?
Alikuwa nayo nafasi ya kusimama katika haki na akaungwa mkono na walio wengi.
Nchimbi mbona anaongea lugha nzuri na anaeleweka?Kwani angeongea kama Nchimbi shida ilikuwa wapi?
Asingekubaliana na teka teka nani angekuwa na taabu naye?
Tatizo lake kulewa madaraka akisikia katiba mpya anaona urais wake 2025 unakuja kwenda na maji.
Laiti angejikita kwenye kujenga legacy yake kuliko 2025 mbona alikuwa na yote ya kupata?
Alipo sasa na ajiangalie asije akaanguka.
Kwani yaliisha je na yule mwamba aliyeambiwa mgombea shuruti awe mwanamke?
Huyu yupo upande wa majangili ya mali za ummaBora bwana yule alifariji wananchi, wakampenda na kumuona ni mkombozi wao, huyu wa sasa hata upande wa " wanyonge hayupo"
Nchi hii kipindi cha bwana yule ilikuwa ina muelekeo chanya hasa ile falsafa ya kazi kazi.
Mama mtu amepwaya hasa kwa wananchi wengi hawampendi,anapendwa na chawa wake tu.
Kabisa yaani. Inakufanya ujihisi mungu mtu ukiwa hai.Ile nafasi lazima ikupe ego matata sana.
Kwa kipimo kipi umetumia kutofautisha ucha Mungu wao?Tofauti na yule, huyu mcha Mungu
Tanzania tabu tunayoNa. M. M. Mwanakijiji
Rais Samia alitaka kupendwa. Rais Samia alitaka kukubalika. Rais Samia alitaka kuoenakana yeye siyo kama yule. Baada ya kuapishwa kufuatia maombolezo ya kifo cha Bw. Yule mara moja watu walianza kusema sasa "wanashusha pumzi". Wapo watu walisherehekea na wakajua kuwa sasa angalau wanaweza kuhema. Hali ya kuwa roho juu kisa bwana yule asiyelala na mwenye kukesha na mafaili hadi chumbani ikashuka. Watu wakaanza kutembea na kuchekeana bila kuogopana.
Upinzani ulishukuru zaidi kwana Bw. Yule aliwabana kweli kweli. Lakini upinzani dhidi yake ulikuwa wazi kabisa na kamili; mgogoro wake na upinzani na dhana ya demokrasia watu waliijua kabla hajaingia madarakani. Hakuwahi kuwa na ahadi za kidemokrasia hata kama aliziimba kidogo. Watu walijua kuwa yeye alichotaka ni "kazi" watu wakakutane kwenye kampeni. Hakutaka kuendekeza siasa za kushindana; walipojaribu kujitutumua vyombo vya dola vya nchi hii vikaingia kumfanya Bw. Yule atawale bila kuzingwazingwa.
Wale wajomba zetu walipojaribu kusema hakuwapepesea macho; na aliwaonesha kweli yeye hawajali kivile pale alipokataa kabisa kwenda kubeba tenga lake kulipeleka huko waliko kuwaomba. Kama aliwaomba aliwataka wao waje kwake ndio awaombe. Tena waje na matenga yao kwanza! Alikataa sana ile hali ya "kujidhalilisha". Sasa Rais Samia alipoingia madarakani siyo tu alitaka kupendwa na watendaji serikali ambao walikuwa roho juu hata kwenda Dubai ilikuwa Mbinde bali alitaka kupendwa na wajomba zetu huko nchi za Magharibi. Rais Samia katika kupendwa huko akaamua kujitenga kimaono na kiutendaji na Bw. Yule.
Bw. Yule alikuwa anafokafoka; mama hakasema yeye hafoki. Huku kijijini Mama akaanza kujulikana kwa "Mama Nahaya Mkayaangilie". Mama hakutaka watu waondoke wamenuna; alijua kuwabembeleza na hata akiwatimua kazi hakutaka wajue ni yeye amechukizwa. Mama akakwepa kabisa kutimua watendaji wabovu papo kwa papo japo anafanya hivyo kimya kimya. Niliandika mahali kuwa Rais Samia ni Simba Mwendapole.
Sasa haya ya juzi ndio yamefunua kuwa jani halitui mbali ya mti na kuwa atapikaye hutapika mbele yake. Mama alijaribu kuwapendeza wapinzani, amejaribu kuwatetea watu wabovu na kwa namna alibariki ulaji wa "urefu wa kamba zao" kumbe wajanja wakala na kamba zenyewe! Mama ambaye alisifiwa kuwa yeye hafokei watu juzi kwenye sherehe za Miaka 60 ya Jeshi la Polisi Mama akajikuta amegeuka kama Bw. Yule.
Yaani, kama hotuba ile ingetolewa kwa sauti ya Bw. Yule kuna watu wangebeba mashada ya maua na kumwambia mama kumbe umerudi! Sasa alivyojitenga vyote vile, na juhudi zote za 4R zimekuwa sasa ni juhudi za 4K - Kugeukana, Kukimbizana, Kutoleana Macho na Kupigana Mikwara! Alijaribu kujitenga na habari za Bw. Yule; lakini sasa karudi tena karudi na naona na tenga analipiga mkwara. Tunakoelekea jina la Bw. Yule litaanza kuimbwa mbele zake kama alama za kumuunga mkono.
Hivi ukivimbiwa kujamba si inakuwa ndio kupumua na kukoroma kwenyewe?Ukisha kula ukavimbiwa unasahau kuna kunawa mikono na mara unapitiwa na usingizi mzito nakukoroma....
Ukiwaambia Watanzania tatizo letu linaanzia kwenye malezi ya watoto, turekebishe kuanzia huko, sio kumuangalia rais wa leo tu, utapata watu wachache sana watakaokubali hilo na kulifanyia kazi.
Na tusipobadili hilo, mengine yote ni kazi bure tu.
Kuweni makini, maana hiyo mtandao aliigusia. Sasa ngoja tuone ya sirini, hii siyo serikali ya samaki.Na. M. M. Mwanakijiji
Rais Samia alitaka kupendwa. Rais Samia alitaka kukubalika. Rais Samia alitaka kuoenakana yeye siyo kama yule. Baada ya kuapishwa kufuatia maombolezo ya kifo cha Bw. Yule mara moja watu walianza kusema sasa "wanashusha pumzi". Wapo watu walisherehekea na wakajua kuwa sasa angalau wanaweza kuhema. Hali ya kuwa roho juu kisa bwana yule asiyelala na mwenye kukesha na mafaili hadi chumbani ikashuka. Watu wakaanza kutembea na kuchekeana bila kuogopana.
Upinzani ulishukuru zaidi kwana Bw. Yule aliwabana kweli kweli. Lakini upinzani dhidi yake ulikuwa wazi kabisa na kamili; mgogoro wake na upinzani na dhana ya demokrasia watu waliijua kabla hajaingia madarakani. Hakuwahi kuwa na ahadi za kidemokrasia hata kama aliziimba kidogo. Watu walijua kuwa yeye alichotaka ni "kazi" watu wakakutane kwenye kampeni. Hakutaka kuendekeza siasa za kushindana; walipojaribu kujitutumua vyombo vya dola vya nchi hii vikaingia kumfanya Bw. Yule atawale bila kuzingwazingwa.
Wale wajomba zetu walipojaribu kusema hakuwapepesea macho; na aliwaonesha kweli yeye hawajali kivile pale alipokataa kabisa kwenda kubeba tenga lake kulipeleka huko waliko kuwaomba. Kama aliwaomba aliwataka wao waje kwake ndio awaombe. Tena waje na matenga yao kwanza! Alikataa sana ile hali ya "kujidhalilisha". Sasa Rais Samia alipoingia madarakani siyo tu alitaka kupendwa na watendaji serikali ambao walikuwa roho juu hata kwenda Dubai ilikuwa Mbinde bali alitaka kupendwa na wajomba zetu huko nchi za Magharibi. Rais Samia katika kupendwa huko akaamua kujitenga kimaono na kiutendaji na Bw. Yule.
Bw. Yule alikuwa anafokafoka; mama hakasema yeye hafoki. Huku kijijini Mama akaanza kujulikana kwa "Mama Nahaya Mkayaangilie". Mama hakutaka watu waondoke wamenuna; alijua kuwabembeleza na hata akiwatimua kazi hakutaka wajue ni yeye amechukizwa. Mama akakwepa kabisa kutimua watendaji wabovu papo kwa papo japo anafanya hivyo kimya kimya. Niliandika mahali kuwa Rais Samia ni Simba Mwendapole.
Sasa haya ya juzi ndio yamefunua kuwa jani halitui mbali ya mti na kuwa atapikaye hutapika mbele yake. Mama alijaribu kuwapendeza wapinzani, amejaribu kuwatetea watu wabovu na kwa namna alibariki ulaji wa "urefu wa kamba zao" kumbe wajanja wakala na kamba zenyewe! Mama ambaye alisifiwa kuwa yeye hafokei watu juzi kwenye sherehe za Miaka 60 ya Jeshi la Polisi Mama akajikuta amegeuka kama Bw. Yule.
Yaani, kama hotuba ile ingetolewa kwa sauti ya Bw. Yule kuna watu wangebeba mashada ya maua na kumwambia mama kumbe umerudi! Sasa alivyojitenga vyote vile, na juhudi zote za 4R zimekuwa sasa ni juhudi za 4K - Kugeukana, Kukimbizana, Kutoleana Macho na Kupigana Mikwara! Alijaribu kujitenga na habari za Bw. Yule; lakini sasa karudi tena karudi na naona na tenga analipiga mkwara. Tunakoelekea jina la Bw. Yule litaanza kuimbwa mbele zake kama alama za kumuunga mkono.
Hana maana kabisaHuyu yupo upande wa majangili ya mali za umma
Bure kabisaHana maana kabisa