Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
Ukiwaambia Watanzania tatizo letu linaanzia kwenye malezi ya watoto, turekebishe kuanzia huko, sio kumuangalia rais wa leo tu, utapata watu wachache sana watakaokubali hilo na kulifanyia kazi.Shida kubwa kwetu Watanzania ni kutoa lawama kwa jambo fulani,bila kufanya tafiti ya kina juu ya chanzo chake ni kipi?
Kuna rafiki yangu mmoja aliwahi niambia "utafanyaje siku ukigundua kwamba wewe ndo chanzo Cha tatizo"Watanzania tujitafakari,haya tuonayo kwa viongozi wetu ni zao letu wenyewe.
Na tusipobadili hilo, mengine yote ni kazi bure tu.