Kwa uovu mwingi alioufanya, hata asipotengewa siku ya kukumbuka uovu wake, atakumbukwa tu.
Miaka mingapi imepita tangu Adolf Hitler atoweke lakini anaendelea kukumbukwa na Ujerumani, Wayahudi na watu wa Dunia nzima? Waovu huwa hawasahauliki, hivyo hawana sababu ya kutengewa siku maalum.
Kwa kawaida baya moja hukumbukwa kuliko 10 mema. Mkapa alifanya mazuri mengi maradufu ya Magufuli, lakini Mkapa, huenda miaka 50 ijayo, watakapjaliwa kuwepo hawatamkumbuka tena. Lakini Magufuli ataendelea kutajwa.
Hakuna mkristo asiyemfahamu Yuda Iskariote, lakini ni wachache sana wanaoweza kuwataja angalao mitume 7 wa Yesu Kristo.