SAGAI GALGANO
JF-Expert Member
- Nov 13, 2009
- 47,706
- 69,281
Si tulishakubaliana nyie vibwengo wake mkazikwe naye sasa hizi tantalila zenu za nini tena huku? Mfuateni mkamsaidie mateso anayopata huko jehanamKila tarehe 17 ya mwezi wa tatu ni siku ya maumivu makali kwa Watanzania. Kila ikifika tarehe hiyo ni kama donda lililopona linatoneshwa tena na maumivu kuanza upya, watu wanamkumbuka Hayati Magufuli.
Kwa kuwa alikuwa ni shujaa kwenye maisha ya wengi hivyo anastahili kuenziwa kishujaa kwa kutengwa siku maalumu ya kumkumbuka na iwe ni mapumziko.
Hii itasaidia maumivu na mateso ya watu kuwa furaha. Pia, kwa kuwa tutahitaji kuwaenzi na Marais wengine waliotangulia na watakaotangulia mbele za haki, basi tarehe 17 ya mwezi wa tatu iwe ni mahususi kufanya hivyo ukiachana na Hayati baba wa Taifa ambaye ana siku maalumu ya kumbukumbu yake.
Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app