Wazoefu nipeni ABC Niko pekeangu na wife anakaribia kujifungua

Inategemea na neighbourhood. Kuna sehemu mwanamke akielekea ama akitoka kujifungua. Si nzuri kushikwashikwa au kuhudumiwa na watu wengi maana kila mtu huwa na nia na lengo lake.

Ni vizuri awe ndugu ama mtu wa kuheshimiana nae sana ndio akuhudumie katika uzazi maana hakuna kipindi mwanamke anakuwa vurnalable kiakili, kihisia, kiroho, kiusafi na kwenye chakula kama kipindi cha uzazi.

Nimesema tu kwa nilioyaona. So sio lazma experiences zifanane. All the best
 
Ni kweli lakin pia haikuwa ujauzito kwetu haitakiwi kabisa ujauzito wa kwanza ni lazima uwe na mzazi au ndugu wa karibu km huwez kurudi lazima wao waje had ujifungue na uoge arobaini ndo wanaondoka
 
Mkuu....
Mimi mke wangu hajawahi kujifungua kwao.
Hakuna rocket science mkuu, tafuta na jiandae kwa mahitaji ya mama kujifungua kisha subiri mkeo ajifungue na hata kumkanda utafanya mwenyewe
Inaonekana ni baba bora sana mkuu. Maana kupitia comments zako nilizoziona ni kama kila kitu huwa ni rahisi kwako hususani kimalezi na kifamilia.

Kama unakuwa involved kwenye maisha ya mke na watoto wako kiasi hicho, hongera sana 👏🏾👏🏾
 
Nimekupata vizuri sana kiongozi, shukrani sana nimepata kitu
 
Pole Sana mkuu, maumivu yako ni mazito
 
kwa uzofu wangu mdogo , katika hali ya kawaida utapata usumbufu wa hapa na pale lakini yoote yatapita salama.

Muhimu la kujiandaa ni wakati ule wa kujifungua hospitalini, uwe na vifaa elekezi, uwe na uhakika wa usafiri muda wowote .

Akirudi nyumbani hakikisha vyakula vyake vinakuwa vyepesi kama uji, mtori nk.

Kufua kutakuwa ni kwingi , kwa hio vifaa vya kufulia kama maji sabuni na mazingira rafiki ya kuanika nguo.


Mama ili maziwa ya mtoto yasiwe ya shida zingatia vyakula vinavyo saidia maziwa kuzalishwa kwa wingi .

Siku za mwanzo kutakua na usumbufu mtoto kulia, lakini sio muda mrefu itakuwa kawaida.

Kama itakuwa amejifungua kwa upasuaji kuna ongezeko vitu na tahadhari .
Nakuombea heri na baraka na mafanikio, na hongera pia.
 
Ni kweli lakin pia haikuwa ujauzito kwetu haitakiwi kabisa ujauzito wa kwanza ni lazima uwe na mzazi au ndugu wa karibu km huwez kurudi lazima wao waje had ujifungue na uoge arobaini ndo wanaondoka
Yeah ni tamaduni zetu hizi ili kulinda stara ya watu. Ni sawa na mtu akifariki, ndugu mara nyingi wanahusika ili kulinda utupu wa ndugu yao. Maana wengine wakiona wanaweza hata kutangaza

Ila kwenye uzazi haswa wa kwanza, Ni vizuri kuwa na ndugu wenye experience maana wanasaidia kujua.

Imagine mtu hujui kuhusu uzazi, utamnyonyesha mtoto bila kumbeulisha mwishowe umuuee

Au mtoto analia na mzazi ndio unatakiwa kujua huyo mtoto analilia nini. Aidha ni joto, hashibi kutokana na wepesi wa maziwa, au anawashwa na mkojo, au umemlaza vibaya na muda mwingine labda alilala kupitiliza so usiku anataka mcheze badala ya kulala 😁

Kuna vingi, na kama imeshindikana bhasi baba wa mtoto awe involved kwa asilimia nyingi na aheshimu mabadiliko ya mkewe kimwili na kihisia. Maana wengine mtoto akilia sana na yeye anaanza kulia
 
Haujakosea mkuu....
Ukifuatilia sana comments zangu, kuna jambo utakuja kubaini kuhusu mimi na familia yangu mazeeee.... we are all good and humble
 
Kuna vingi, na kama imeshindikana bhasi baba wa mtoto awe involved kwa asilimia nyingi na aheshimu mabadiliko ya mkewe kimwili na kihisia. Maana wengine mtoto akilia sana na yeye anaanza kulia
Ni sahihi kabisa mkuu uangakuz ni muhimu sana
 
Mkuu kama una noti unatuma tu ndugu upande wa mke anakuja mlipo ndo anashughurika na ndugu yake wewe ni pesa tu unatoa hakuna wasi mambo haya ni madogo sana kama Haina noti ndo kimbembe mtafutano😁
 
Mkuu kama una noti unatuma tu ndugu upande wa mke anakuja mlipo ndo anashughurika na ndugu yake wewe ni pesa tu unatoa hakuna wasi mambo haya ni madogo sana kama Haina noti ndo kimbembe mtafutano😁
Wauguzi hawana dogo 😃ela muhimu
 
Asante kwa kunitag mai 💕

CAMANGA Nimejifungulia nyumbani kwangu mara mbili nikiwa na mume wangu ambaye ana tabia kama za mzee mwenzangu Ushimen na msaidizi wa kazi tu.

Muhimu:
Msikilize mkeo, usiwe mvivu na usiwe mbinafsi. Hichi ni kipindi mwanamke anakua vulnerable sana kwa sababu ya maumivu ya uzazi na mabadiliko mengi ya homoni.

Hakikisha ana vyakula na mahitaji ya msingi yake pamoja na mtoto.

Msaidie kwenye mambo kama kumkanda (if anataka) na kumuosha huko chini hasa kama atakua ameshonwa. Akiwa ameshonwa (either kwa sababu ya cesarian au kuongezewa njia) kila kitu kinampa maumivu, kuanzia kupiga miayo, chafya, kukaa, kusimama, kutembea, kukojoa na kujisaidia haja kubwa, msaidie anapohitaji.

Msaidie mambo madogo madogo ya mtoto kama kumbadilisha diaper pale unapokuwa nyumbani na hakikisha mkeo naye anapata muda wa kupumzika, hasa kama mtoto anasumbua.

Kuwa sensitive na mambo ya maumivu, kama inabidi kumyanyua, kumsaidia kwenda chooni na kadhalika. Anaweza kua na aibu au kujisikia fedheha kukuomba kila kitu, jiongeze. Siku za mwanzo huwa zinakua na changamoto ila baada ya wiki hivi ataanza kukaa sawa na kuweza mwenyewe.

Cha msingi mjali na kila ukijisikia wewe umechoka, fikiria yeye ambaye anafanya mengi zaidi yako ikiwemo kunyonyesha mchana na usiku, anachokaje.

Hichi kipindi kitawaleta karibu sana kama utaweza kuwa sapoti anayoihitaji na siyo mzigo.

Pole, haitakua rahisi ila mtaweza.
 
Kama mtoto wa pili , mkeo atakuelekeza nini Cha kufanya Kila la kheri...
Ila omba asiongezewe njia au Op nje ya hapo anatoboa tu peke yake...
Hv kuongezewa njia ndio anachanwa K na kiwembe?
 
Una ela? Tafuta nesi awe anamsaidia home simple
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…