Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,611
Precision na fastjet wamekufa au wanakufa kwa sababu zao binafsi pasipo kuingiliwa na mkono wa serikali. Ukosefu wa weledi wa sekta ya anga, umeua fastjet.Hata kama ndege ni lazima, si lazima ndege ziwe za serikali.
Marekani hawana shirika la ndege la serikali linalofanya biashara ya usafiri wa ndege, na nchi yao inakwenda vizuri tu. Na hawa ndio waliogundua usafiri wa ndege, ndio wanaotengeneza ndege kubwa za Boeing.
Biashara ya ndege ina risk kubwa sana, na watu wa serikali kikawaida hawajui kujiendesha kwa ufanisi kibiashara, na pale wanapojua, serikali ina michakato yenye ukiritimba mwingi ambao haufai kwenye biashara. Serikali ingeweka mazingira mazuri kwa mashirika binafsi kufanya biashara. Mashirika binafsi yafanye biashara. Tulishaanza hili vizuri.
Lakini kwetu sisi, serikali ndiyo imeshiriki kuua mashirika ya ndege ya binafsi kama Precision Air na FastJet.
Na hata hilo shirika la ndege la serikali haliachwi lijiendeshe kwa uhuru kibiashara, linaingiliwa sana kisiasa na serikali.
No wonder linatengeneza hasara year in, year out.
Soma zaidi kwa nini Africa mashirika yake mengi ya ndege yanapata hasara.
Weiterleitungshinweis
www.google.com
Kuna wataalam wa masoko na masuala ya anga wanaoendesha shirika kwa sasa, kwa ufupi lipo katika mikono salama sana kulinganisha na miaka ile ya awamu ya kwanza na ya pili.