Wazungu wanafanyaje mpaka Watoto wadogo chini ya miaka 13 wanahitimu degree kwenye vyuo vikuu majuu

Ni ngumu sana mkuu kama kuna mwanangu mmoja hata simultaneous exuation hawez kujibu wakati majibu yanaonekana wazi kabisa na ana 30+ iwe integral kwa mtoto wa 4 years.. Mkuu ni ngumu sanaaaa
Sawa mkuu maana naona huu Uzi umejaa chai tu , eti mtoto wa miama 8 kapata degree au sijui wa miaka 3 anasolve integrals. Kuna zile integrals kila ukifanya zinajirudia mpaka urudishe kule sehemu ya pili ya equation ukachanganye Na swali halafu simple tu anakuja mtu anasema mtoto wa miaka 3 ulaya anafanya yote hayo.. Hii ni kashfa kwetu tuliyajua hayo tukiwa Na miaka 20
 
Kwa ufahamu wangu mdogo watu wa aina hii wanakuaga maginiasi (akili kupitiliza) hivyo hua wanarushwa madarasa. .kila darasa unalompeleka anakua wa kwanza amefeli sn anakua wa pili...normal process wanamaliza wakiwa na miaka 18 ndio anakua amemaliza degree
 
Tatizo ya elimu yetu ni mpaka uwe na mavyeti yote ili uendelee level nyingine...
 
Umejaribu kuangalia iq za hao uliwaowataja? Wote hao nina uhakika ni wale 1% ambao iq zao ni very exceptional hata kwa wazungu wenzao .

Umri wa majority kumaliza degree kwa nchi za nje ni 19-20 mtu akiwa na 23 tayari wengi wana masters 25-27 wana phd kabisa .
 
Kusoma degree tz Ni lazima utoke form 6 au uwe na diploma ulioipata pale ume feli form four au kufeli form 6 Kisha ukafate diploma sehemu ndo uanze degree no short cut for that here
Kusoma degree si lazima usome form six na kwenda diploma si lazima ufeli form 4 mfano vyuo vingi sana vya technical vina sponsor form four waliochagua diploma badala ya advance secondary na hao wanaokwenda diploma kwa kuchagua ni vichwa haswa wana division 1 na 2 wengi wao .

Hapo watasoma diploma na wakimaliza level 6 wanakuwa elligible kujiunga na degree level kama wakifikia GPA inayotakiwa zamani ilikuwa 3.5 ila kwa sasa ni 3.0 nadhani, na mkopo wanapata kama wenzao na kama wataunga bila kufanya kazi kwanza basi watakutana na wale wenzao walioenda form six moja kwa moja wao wakiwa wanaingia mwaka wa pili yaani level 7 one bila ya kupita kwanza level 6 kama wenzao wa direct.
 
Hao ni broiler tofauti na sisi wakienyeji..
 
Nanukuu: "Sikujuaga aliishia wapi."
Kama ulivyobainisha ni kweli wapo.Lakini wahusika wa Ufuatiliaji wa watoto hao kimaendeleo ikiwa ni pamoja na Serikali kukubali kuchukua dhamana ndo imekufanya useme" Sikujuaga aliishia wapi."
Vikwazo ni vingi, ni vingi mno. Baadhi ya vikwazo:-
1. Wazazi wanaweza kumkatalia mtoto asiende huko.....Eti ni mdogo mno au hawampi hamasa (encourage and motivate) na hivyo mtoto anaona haina maana naye anapuuzia.
2. Waalimu wake pale anapoanza shule Chekechea, kwa makusudi au bila kujua wanaua au kuzuia kipaji cha mtoto kisijitokeze kwa kutojali au kupuuzia au kumnyima mtoto nafasi/fursa ya kuonesha kipaji chake.
3. Jamii inayomzunguka mtoto wa namna hiyo mwenye kipaji fulani huweka vikwazo vya kisaikolojia (humjengea mtoto na wazazi wake Hofu)- ikiwemo mambo ya kishirikina n.k.
 
Well ni admit kuwa huo umri naweza kuwa nime exaggerate lakini kuna child prodigies.

Mfano huyu dogo hebu mtafute Balamurali Ambati.
Licha ya KUFANYA makubwa darasani ila alifanya blunders sana in real prectice, inaonekana KWENYE research papers ni nondo huyu jamaa ila kwingine huku kama surgery alizingua.
 

Attachments

  • Screenshot_20230425-230801.png
    68.2 KB · Views: 9
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…