Wazungu wanafanyaje mpaka Watoto wadogo chini ya miaka 13 wanahitimu degree kwenye vyuo vikuu majuu

Wazungu wanafanyaje mpaka Watoto wadogo chini ya miaka 13 wanahitimu degree kwenye vyuo vikuu majuu

Ni ngumu sana mkuu kama kuna mwanangu mmoja hata simultaneous exuation hawez kujibu wakati majibu yanaonekana wazi kabisa na ana 30+ iwe integral kwa mtoto wa 4 years.. Mkuu ni ngumu sanaaaa
Sawa mkuu maana naona huu Uzi umejaa chai tu , eti mtoto wa miama 8 kapata degree au sijui wa miaka 3 anasolve integrals. Kuna zile integrals kila ukifanya zinajirudia mpaka urudishe kule sehemu ya pili ya equation ukachanganye Na swali halafu simple tu anakuja mtu anasema mtoto wa miaka 3 ulaya anafanya yote hayo.. Hii ni kashfa kwetu tuliyajua hayo tukiwa Na miaka 20
 
Kwa ufahamu wangu mdogo watu wa aina hii wanakuaga maginiasi (akili kupitiliza) hivyo hua wanarushwa madarasa. .kila darasa unalompeleka anakua wa kwanza amefeli sn anakua wa pili...normal process wanamaliza wakiwa na miaka 18 ndio anakua amemaliza degree
 
Tatizo ya elimu yetu ni mpaka uwe na mavyeti yote ili uendelee level nyingine...
 
Habari wadau.

Sio kitu cha ajabu kukuta mtoto wa miaka 10 anasoma chuo kikuu majuu.

Tena degree za kibabe kama Engineering , Medicine, Mathematics etc.

Wazungu wanatumia mbinu gani kuwapa admission kwenye vyuo vikuu vyao hawa watoto.

Je Tanzania hatuna watoto wenye akili wa miaka 10 mpaka miaka 13 ambao wanaweza kusoma degree kwenye vyuo vikuu vyetu kama udsm, mzumbe , udom ama Muhas

Tunakosea wapi ama tuna gundu hatuwezi kuzaa watoto ma Genious Darasani wa kusoma degree bila kupitia mfumo wa sekondari unaochukua miaka mingi kufika chuo kikuu

Mfano wa wahitimu wa vyuo vikuu ni

1. Balamurali Ambati alimaliza degree ya udaktari akiwa na miaka 16 na kufikia miaka 17 akawa daktari tayari anatibu watu.

2. Michael Kearney alihitimu degree ya Geology akiwa na miaka 8 tu.

3. Ruth Lawrence alimaliza degree yake ya Physics Oxford university akiwa na miaka 11 na akaunganisha degree zingine hapo hapo Oxford kufikia miaka 17 akahitimu PHD ya Mathematics hapo hapo Oxford University

4. Sho Yano alihitimu degree yake ya udaktari akiwa na umri wa miaka 12 tu

5 - Juliet Beni. At just 15 years old, she obtained her bachelor’s degree at the University of California, ( chuo kikuu alichosoma proffessor Mkandala wa udsm kinampa nafasi mtoto mdogo asome degree yake mapema )
Umejaribu kuangalia iq za hao uliwaowataja? Wote hao nina uhakika ni wale 1% ambao iq zao ni very exceptional hata kwa wazungu wenzao .

Umri wa majority kumaliza degree kwa nchi za nje ni 19-20 mtu akiwa na 23 tayari wengi wana masters 25-27 wana phd kabisa .
 
Kusoma degree tz Ni lazima utoke form 6 au uwe na diploma ulioipata pale ume feli form four au kufeli form 6 Kisha ukafate diploma sehemu ndo uanze degree no short cut for that here
Kusoma degree si lazima usome form six na kwenda diploma si lazima ufeli form 4 mfano vyuo vingi sana vya technical vina sponsor form four waliochagua diploma badala ya advance secondary na hao wanaokwenda diploma kwa kuchagua ni vichwa haswa wana division 1 na 2 wengi wao .

Hapo watasoma diploma na wakimaliza level 6 wanakuwa elligible kujiunga na degree level kama wakifikia GPA inayotakiwa zamani ilikuwa 3.5 ila kwa sasa ni 3.0 nadhani, na mkopo wanapata kama wenzao na kama wataunga bila kufanya kazi kwanza basi watakutana na wale wenzao walioenda form six moja kwa moja wao wakiwa wanaingia mwaka wa pili yaani level 7 one bila ya kupita kwanza level 6 kama wenzao wa direct.
 
Habari wadau.

Sio kitu cha ajabu kukuta mtoto wa miaka 10 anasoma chuo kikuu majuu.

Tena degree za kibabe kama Engineering , Medicine, Mathematics etc.

Wazungu wanatumia mbinu gani kuwapa admission kwenye vyuo vikuu vyao hawa watoto.

Je Tanzania hatuna watoto wenye akili wa miaka 10 mpaka miaka 13 ambao wanaweza kusoma degree kwenye vyuo vikuu vyetu kama udsm, mzumbe , udom ama Muhas

Tunakosea wapi ama tuna gundu hatuwezi kuzaa watoto ma Genious Darasani wa kusoma degree bila kupitia mfumo wa sekondari unaochukua miaka mingi kufika chuo kikuu

Mfano wa wahitimu wa vyuo vikuu ni

1. Balamurali Ambati alimaliza degree ya udaktari akiwa na miaka 16 na kufikia miaka 17 akawa daktari tayari anatibu watu.

2. Michael Kearney alihitimu degree ya Geology akiwa na miaka 8 tu.

3. Ruth Lawrence alimaliza degree yake ya Physics Oxford university akiwa na miaka 11 na akaunganisha degree zingine hapo hapo Oxford kufikia miaka 17 akahitimu PHD ya Mathematics hapo hapo Oxford University

4. Sho Yano alihitimu degree yake ya udaktari akiwa na umri wa miaka 12 tu

5 - Juliet Beni. At just 15 years old, she obtained her bachelor’s degree at the University of California, ( chuo kikuu alichosoma proffessor Mkandala wa udsm kinampa nafasi mtoto mdogo asome degree yake mapema )
Hao ni broiler tofauti na sisi wakienyeji..
 
Inawezekana wapo lakini mazingira yetu haya support mambo kama hayo. Sisi tulishakariri lazima mtoto asome chekecea, msingi, sekondari ndio aende chuo.

Ila mimi kuna dogo mmoja alikuwa anaitwa Bryan nakumbuka alikuwa darasa la nne ila alifanya mtihani wa la saba akafaulu na kuenda sekondari akiwa mdogo kabisa. Sikujuaga aliishia wapi.

Huku kwetu wapo hao watoto shida ni mifumo yetu iliyodumaa na kukariri maisha.
Nanukuu: "Sikujuaga aliishia wapi."
Kama ulivyobainisha ni kweli wapo.Lakini wahusika wa Ufuatiliaji wa watoto hao kimaendeleo ikiwa ni pamoja na Serikali kukubali kuchukua dhamana ndo imekufanya useme" Sikujuaga aliishia wapi."
Vikwazo ni vingi, ni vingi mno. Baadhi ya vikwazo:-
1. Wazazi wanaweza kumkatalia mtoto asiende huko.....Eti ni mdogo mno au hawampi hamasa (encourage and motivate) na hivyo mtoto anaona haina maana naye anapuuzia.
2. Waalimu wake pale anapoanza shule Chekechea, kwa makusudi au bila kujua wanaua au kuzuia kipaji cha mtoto kisijitokeze kwa kutojali au kupuuzia au kumnyima mtoto nafasi/fursa ya kuonesha kipaji chake.
3. Jamii inayomzunguka mtoto wa namna hiyo mwenye kipaji fulani huweka vikwazo vya kisaikolojia (humjengea mtoto na wazazi wake Hofu)- ikiwemo mambo ya kishirikina n.k.
 
Well ni admit kuwa huo umri naweza kuwa nime exaggerate lakini kuna child prodigies.

Mfano huyu dogo hebu mtafute Balamurali Ambati.
Licha ya KUFANYA makubwa darasani ila alifanya blunders sana in real prectice, inaonekana KWENYE research papers ni nondo huyu jamaa ila kwingine huku kama surgery alizingua.
 
Attachments

  • Screenshot_20230425-230801.png
    Screenshot_20230425-230801.png
    68.2 KB · Views: 9
Back
Top Bottom