Wazungu wanasema Tanzania rushwa imepungua Sana wakati wa Rais Samia kuliko ule wa Magufuli. Watanzania wanasema rushwa inaongezeka. Je, ipi ni ipi?

Kafulila yuko vizuri Sana
 
Umeshaambiwa kwamba chanzo ni Transparency international ndio maana mnafeli sana mitihani
Usiwe mkurupukaji jamaa.
Niliyemnukuu unajua aliandika nini!!??
Kwenye hiyo habari umeona chanzo hicho cha TI kilichoandika hayo au umemsikia tu D. Kafulila!!???
Unajua maana ya kuweka chanzo cha tafiti cha kuaminika!!???
Mkuu bagamoyo njoo ufundishe vilaza namna ya kuweka habari na vyanzo vyake vya kuaminika tafadhali.
 
Ungeenda Ku-google
 
Angalia Sasa hivi kupata kazi katika sehemu mbalimbali hata Sensa ni rushwa tupu yaani ni konection Tu.
 
Nimetoa angalizo sijaunga mkono rushwa. WENYE WAJIBU WA KUpambana na rushwa wapo wafanye majukumu yao
Mkuu nakusalimu kwa jina JMT,
TUENDELEE KUMWOMBEA KAFULILA NI MTU GENUNE SANA NA ANAUWEZO MKUBWA WA KUMSAIDIA MAMA
 
Kuna uwalakini...na wasifu wao, kuhusu TANZANIA na RUSHWA
Huwa hawakupambi bure bure tu.

...hatahivyo

Jitihada mahsusi za kungamiza '"Mbinu" na "Ujeuri" za wapiganaji wa "Vita vya uchumi" wapinga rushwa na wapinga ukoloni mamboleo Afrika, zinaendelezwa.
 
Hakuna kama Rais Samia
 
wazungu ni wapuuzi tena wapuuzi sana.afrika tuungane tufanye biashara zetu.tuachane na wazungu.ukiona mzungu anasifia jambo ujue tumeanza kuibiwa rasilimali zetu.kwa nn afrika tusiungane tukaacha kupeleka watoto wetu kusoma huko,tukafanya biashara sisi kwa kuliko kuing"ang"ania hii mibeberu?
 
Wazungu hawakwepeki mzee
 
Kwa ivo mtoa maada akili yako inaongozwa na kushikiliwa na mzungu? Akikwambia wewe ni nchi maskini hata kama una rasilimali utakubali? Akikwambia wewe ni tajiri ila unaishi kwa mlo mmoja ni sawa tu?
 
Kwa ivo mtoa maada akili yako inaongozwa na kushikiliwa na mzungu? Akikwambia wewe ni nchi maskini hata kama una rasilimali utakubali? Akikwambia wewe ni tajiri ila unaishi kwa mlo mmoja ni sawa tu?
Mzungu ndio mwenye taarifa zako zote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…