Ahsantee sana Mercy.
MOTP me kukulaumu sitoacha hata ukamilifu wa dahari. You know you are a married man, respect your commitment period. Tumesamehewa dhambi na sio majaribu, so majaribu lazima yaje coz hakuna kitu ambacho shetani anakipiga vita kama a happy marriage. Sasa wewe shetani akigonga tu hodi huyooo ushamfungulia hadi chumbani khaa. Wewe kila siku ni bahati mbaya tu, unayaentertain majaribu wee; Zinaa haikemewi, inakimbiwa. We can't blame michepuko, yenyewe haina commitment na mkeo
Afu wanaume wa humu mnisikilize kwa makini, najua wengi wenu mnakutana na opportunity kama za MOTP, unfortunately wengi wenu mawazo yenu yanakuwa ya kupiga match na kusepa, ila wanawake tupo calculated always. Afu unaniudhi unavyowapa treatments kama za mkeo muone kwanza mtcheew, unategemea watakubali kuachana na wewe? Siku zinavyoenda wewe unaona shughuli imeisha ila mwenzako ndo mapenzi yamemnogea and so ataanza kujitahidi kumpindua mkeo ili akumiliki. Ndo unapomuweka mkeo kwenye hatari sasa bila yeye kujua, please waoneeni huruma wake zenu. Naima ameshaamua liwalo na liwe, she had a taste of paradise, there is no way she will let go it. Mara nyingi hakuna mtu anayependa tu kuishia kuwa mchepuko wa a good man, atapigana vita vyote ili akumiliki. You can't guarantee how low she can stoop kuwin hiyo vita yake please. Tena shukuru tu michepuko yako haina akili za kujibebesha mimba, ila soon utaanza kuwa na watoto East Africa yote. Endeleeni kujiendekeza tu, siku hizi mwanaume mpumbavu hujisababishia kifo chake mwenyewe