Weka hapa msanii alieweza kupata umaarufu nchini akiwa bado yupo mkoani

Weka hapa msanii alieweza kupata umaarufu nchini akiwa bado yupo mkoani

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264
Wasanii wengi wanaofanya kazi zao mikoani huwa wanaishia kutamba hukohuko mikoani lakini wapo wachache ambao walivuka boda na kupata umaarufu nchi nzima.

Uzi huu tuwataje wasanii waliofanya kazi zao mikoani lakini zikahit na kuwatambulisha nchini.

Marlaw - Iringa
1697394632785.png


Marlaw baada ya kumaliza form four alifaulu kwenda kidato cha 5 Mafinga, Alikuwa anaenda Iringa mjini Kurekodi Studio za Iringa Records wakati huo Producer ni Tuddy Thomas ambae kwa sasa kaajiriwa na Diamond, Ngoma iliyohit angali akiwa bado mkoani inaitwa Bembeleza

Belle 9 - Morogoro

1697402095259.png


Belle 9 akiwa Morogoro aliiachia "Sumu ya Penzi" aliyoirekodi studio za 'Rocker tz records' Producer akiwa ni 'Tris', Hii ngoma ilimtambulisha kwa kishindo kizito sana, ilisumbua mno vituo vya redio na Tv,
 
Hawa wengine nao ni comedians wa Mbeya, waliweza kutrend sana kwa kazi walizofanya wakiwa Mbeya i

Mc Mboneke Irudiwe - Mbeya
1697395531345.png

alipata umaarufu mkubwa kwa video yake ya "Irudiwe irudiwa", yani nakumbuka ni kama wiki nzima hivi nikiingia status naona karibu kila mtu kaiweka.

Kashili Muuza Mayai
1697395706061.png


Kuna komedi ilitrend sana mitandaoni mwanzoni watu walizani ni video ya fumanizi la muuza mayai kukamatwa na mke wa mtu kumbe ni Comedy tu.
 
Kuna wasanii waliweza kujuzolea umaarufu nchini wakiwa bado mikoani tofauti na tulivyozoea kwamba msanii lazima apate umaarufu akiwa Dar.

Marlow - Iringa
View attachment 2783137

Marlaw baada ya kumaliza form four alifaulu kwenda kidato cha 5 Mafinga, Alikuwa anaenda Iringa mjini Kurekodi Studio za Iringa Records wakati huo Producer ni Tuddy Thomas ambae kwa sasa kaajiriwa Diamond, Ngoma za Marlaw zilozohit angali akiwa bado mkoani Iiringa ni Bembeleza na Ritha,
Budagala wa Meatu shy town
 
Mpaka nikumbuke ngoma
Joh makini katobolea Dsm

Jo makini kaanza kupata umaarufu Dsm pale alipoibuka na kazi yake ya 'Hao' aliyokuwa ameitoa mwaka 2005,chini ya utayairishaji wake 'producer Ludigo

2006 alitoa chochote popote chini ya utayarishaji wake producer 'Ambrose Dunga.

Baada ya hapo alitoa hit nyingine "Zamu Yangu" akiwa Dsm.
 
Joh makini katobolea Dsm

Jo makini kaanza kupata umaarufu nje ya Arusha pale alipoibuka na kazi yake ya 'Hao' aliyokuwa ameitoa mwaka 2005,chini ya utayairishaji wake 'producer Ludigo

2006 alitoa chochote popote chini ya utayarishaji wake producer 'Ambrose Dunga.

Baada ya hapo alitoa hit nyingine "Zamu Yangu" akiwa Dsm.
Kweli una historia nzuri sana.
 
Kweli una historia nzuri sana.
Hivi kwann wasanii wa Arusha wanatiaga ugumu kwenda Dsm kurekodi kazi zao ?

Naona bado hawajastuka kufikiri nje ya box kwamba Muziki inabidi ufanywe kwa malengo kuzidi ego yao ya kutaka kufanyia kila kitu Arusha ?
 
Hivi kwann wasanii wa Arusha wanatiaga ugumu kwenda Dsm kurekodi kazi zao ?

Naona bado hawajastuka kufikiri nje ya box kwamba Muziki inabidi ufanywe kwa malengo kuzidi ego yao ya kutaka kufanyia kila kitu Arusha ?
Mazoea tu, na wanaamini arusha kumejitosheleza kila kitu....zone ya arusha huwa sio wasanii tu bali na wengine hawaamini katika dar, wao wanaona dar ni extra kwa mambo yao.
 
Back
Top Bottom