Serikali inazalisha na kufundisha Wanasiasa na Raia kuwa sio wazalendo. Taifa letu la kesho halitakua na viongozi wazalendo.
Serikali inavyotengeneza sinema za kununua (Kwa rushwa) wapinzani na kwa vitisho, inafundisha na kutuaminisha kwamba siasa ni kujali tumbo lako pia vita dhidi ya Rushwa haishindikani.
Vyombo vya dola (hasa vya usalama) vime lawitiwa na viongozi wachache baada ya kujitoa kwenye mfumo wa vyombo vya Usalama na kua vyombo vya siasa, credibility imekufa, division of power/delegated legislation hakuna, havina hadhi tena kama vyombo vya usalama, na hakuna raia anaeviamini kwasasa hivi.
Imefikia hatua raia wanashindwa kutofautisha kati ya kuwa Askari polisi na vibaraka wa CCM raia wanaona askari ni kibaraka na sio mtu wa kumwamini. Kwasababu jeshi la polisi limekubali kutumika kisiasa.
NB tumeshudia OCD wakiimba mapambio ya CCM. Na hakuna hatua za kinidhamu walichukuliwa.
Hii, tunajenga uadui ndani ya Taifa. na hakuna vita mbaya kama kujenga uadui wa ndani (Katika familia, ni rahisi kupambana na adui wa nje ya familia, kuliko kupigana na adui wa ndani ya familia).
Uadui wa ndani ya taifa ni njia rahisi ya kuruhusu maadui wa nje ya taifa.
Serikali isilalamike kama inavyopenda kulalamika "Kuna baadhi ya watu sio Wazalendo wa Nchi yetu" Yenyewe ndio inazalisha hao watu, yenyewe ndio inaharibu uzalendo kwa raia, yenyewe ndio inajenga chuki na kuvunja uaminifu kwa raia.
Yaliofanyika jana ni kashfa kubwa kitaifa na duniani. TISS, Polisi, TAKUKURU wanatakiwa watoe majibu ya kuridhisha kwa Wanancu na Dunia"Kukaa kimya, raia na dunia tutaamini wamehusika katika uvunjifu wa Sheria na Katiba ya Nchi.
Cha kujiuliza:
Uchafu huu wote pamoja na kuliangamiza taifa, unafanyika kwasababu gani?
Jibu, kwaajili ya viongozi wachache wa CCM (Wasiojali wala kuogopa amani ya nchi kuvunjika, raia kufa, taifa kuangamia) wenye tamaa ya kushika madaraka kwa miaka 5 ijayo.