Weka siasa pembeni, tafakari "credibility" ya Mamlaka za Serikali katika sakata la CHADEMA

So wewe unadhani Lissu angekuwa Rais. Unajua Kwanini alikuwa na go and return ticket. Ukiwa mpumbavu jaribu kukaa kimya
Hebu tueleze wewe unayejua, ni kwa nini alikuwa na go and returt ticket ? Au alikatiwa na mabeberu kama mnavyowaita ?
 
Yani watu waliofoji uchaguzi ndio washindwe kufoji mihuri na signature kweli?
Kwahiyo Unataka Kusema Vyeti Fake Watumishi Walifutwa Kazi Haraka Sana. Na Hii Nayo Ifutwe Turudie
Tanzania Ujanjaujanja Tu, Mambo Mengine Yanatia Kinyaa 😏😏😐😂
 
Daah nikweli kabisa sasahivi sidhani Kama kunaraia anaweza kusaidiana na askari iwapo kamakutatokea .Uhalifu kamazamani ccm pamoja naserikali ndio imetufikisha hapo
 
Uzuri kila kukicha vilaza tunazidi kujulikana, tunazidi kulizwa kwa kujifanya wajuaji. Sawa mwenye akili kubwa, sisi wacha tuendelee kulishwa mifupa, wenye akili huko naona mnalishwa minofu. Endeleeni kufaidi minofu, kwani unazidi kuletwa. Stay tuned!
 
Ukweli ni kwamba Yote haya yameanzia kwenye siasa za majintaka Sasa hivi siasa hizi za.majibtaka zinaathiri taswira ya nchi yetu. Haiingii akilini kuona mihimili ya nchi Bunge, Mahakama na Serikali kupitia NEC na Vyombo Mbalimbali vya Dola vikiingiza Nchi yetu katika Kashfa nzito za kimaadili na utovu wa nidhamu.

Inawezekanaje Spika mwenye washauri na Watendaji wa Kila Aina kujiingiza katika mchezo huu wa kihuni? Hivi kweli Tanzania ya Mwl. Nyerere imefikia mahala pa kuwa na Spika anayefanya mambo kihuni na bila kuheshimu Taratibu, Sheria na Katiba kiasi hiki?

Haiingii Akilini kwa Mhimili wa Mahakama kujiingiza katika Kashfa ya Kimaadili Kama hii. Hivi wananchi waiamini taasisi ipo nyingine Kupata Haki zao Kama chombo cha kutoa haki nacho kinaminya haki?

Wapo wapi wazee wa taifa hili?? Tunahitaji Sana busara na Ushauri wenu. Pamoja na ukweli kwamba mnaona Bora mkae kimya ili muishi vzr, lakini heshima yenu ni muhimu zaidi. Mambo haya kutokea mbele yenu na mkawa kimya, yanafikirisha Sana watu waliowaamini ndani na nje ya nchi yetu.
 

Taifa likikosa mashauri litaangamia.
Hao wazee wanaogopa wasiojulikana wamepewa uhakika wa shibe na familia zao kuumizwa kwako au maadili yanawahusu nn
 
Hii ni aibu kubwa sana kwa mfumi wetu wa utawala!Hii inaonesha wazi kuwa watawala wako juu ya sheria na wanaweza kuingilia mambo ya ndani ya vyama wakijisikia!
Kesho Msajili anaweza kuamka na kusema amepata taarifa za kuwa Mwenyekiti wa CDM ni Halima mdee na katibu mkuu ni Bulaya!Na ikawa hivyo!
 
nimekuwa nikiuliza humu lakini sijajibiwa, Nec haiwezi kufikishwa mahakamani kwa kughushi nyaraka za chama na kufanya uteuzi wa ulaghai?
 
Waambieni upuuzi wanaofanya umechosha,watumishi wanahitaji stahiki zao.Na si fedha zitumike kuwanunua wakina Mdee.
 
Mnatia sana huruma


mbowe kateua katibu mkuu mpya au naibu katibu mkuu kasawazisha, bila mnyika kujua

Kafuata taratibu zote wabunge wale pale

Mnyika, Lissu automatically wako against Mbowe kwenye hili


Mkiambiwa chama kina wenyewe uelewe
Umejuaje kuwa kuna huo mpasuko kati ya viongozi hao wa CHADEMA?
 
Wewe ni Great Thinker..hichi ndicho kinatengenezwa katika nchi. Kwa ufupi vyombo vya usalama viko kuinstall madhalimu uliyoyataja hapa. Kukaa kimya kwao ni hatar sana kwa mstakabar wa umoja wetu. Vyombo vyote vnaonekana vimekua biased juu ya sheria na kanuni zilizowekwa kuismamia nchi na Tasisi zake!!
Tunakoelekea rushwa halitakuwa kosa la jinai why KwasabAbu waliochin wataona waiishi kama vile wakubwa wanavyooishi yaani "mbona wao wanaiba/rushwa na sisi lazma tuibe/tule rushwa ".Uongozi nyanga'nyi utatengeneza mfumo nyanga'nyi hapo ndy penyewe patakapotutesa kama Taifa. Huu ni ugonjwa utakaotutafuna sana. Je Vyombo vyetu kwann viko kimya??

Sent from my SM-G920F using JamiiForums mobile app
 
Hiyo ni opportunity ya kuendelea kupaza sauti zao, kwa sababu mkiitwa mtaani amuendi na mtu kama wewe unakiri kabisa kura wala upigi. Hila unataka waendelee kuumia tu kwa ajili yako.

Kwa ivyo tusiwaamulie pia kwenye maamuzi yao.
Sauti zilizopazwa kabla zimeleta impact gani?
 
Hata hivyo ukweli ni kwamba hayo yote hayawezi kuurejesha mwili wake katika hali aliyokuwa nayo mwanzo.Hapo ndipo ninapopata sababu ya kumshukuru Mungu kwa kutuumbia kitu kinachoitwa "huruma" katika nafsi zetu.Aliona mbali sana.
 
Labda wameamua kuihujumu serikali kijanja.U never know.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…