Weka urafiki na wanajeshi (bakabaka) hutojutia

bas ujapata kujua wajeda wanatendaga nini kwa vituo vya mapongo especially case iwe ni base less watu wanatolewaga lockup na makwenzi wanapigwa
Acha siasa za uongo wewe kima mara ngapi hao wanajeshi wanakamatwa na polisi wakiingia lock up wanalia tu mara ooh mtanifukuzisha kazi mara nini sijui..Wenzao wakija huja kwa upole na kuomba waondoke naye ili waende wakamchukulie hatua za kijeshi huko kambini(hapa huzingatiwa uzito wa kosa/jinai ndogo ndogo) makosa makubwa makubwa yote ya jinai yakifanywa na mwanajeshi hakuna kiongozi wa jeshi anaweza kuja kumuombea kituoni.


Huo ujinga wenu wa kudanganyana wafanyieni watoto wadogo,mwanajeshi ni mtu na polisi pia ni mtu(wote wana uzani sawa).

Hakuna pimbi yoyote anayeweza kutoa mtu kibabe akiwa lock up isipokuwa kwa mjibu wa sheria tu.

Mtu atakayeweza kuthubutu kufanya hivyo akiwa ni mtumishi basi anaweza hata kufutwa kazi au kukoma kupanda vyeo baada ya kushitakiwa.
 

Umezunguka ila umerudi palepale. Urafiki na watu wa vyombo vya ulinzi na usalama sio suluhisho. Taabu iko palepale. Naamini katika Haki na Sheria kuliko urafiki (kujipendekeza)
 

Waeleze ukweli.
 
Kuna uzi humu unachekesha balaa,

mmoja alikuwa anaenda kumtembelea bro wake kambini kila j,mosi, sasa j,mosi moja kaenda hajamkuta kawakuta wajeda wenzie[emoji3]

Wakamuuliza we hauna kazi??

maana kila weekend unakuja hapa, wakamwambia ahamishe tofali,,,,,,,kafika bro wake anashangaa dogo anabebavtofali na anakohamishia sipo[emoji3][emoji3][emoji3]

Dogo alivyomuona bro akajua atamwambia ache,


Bro akamwamhia dogo rudisha tofali ulikotoa[emoji3][emoji3]
 
Nikushauri kitu kijana,

Dark ages ilikuwa hata Ulaya toka zamani,hata
Ulaya kulikuwa na uchawi na mpka Serikali zilikuwa Zina sheria juu ya uchawi,Ulaya kulikuwa na ubabe wa watawala kupitiliza, People evolve, making changes,

Hivyo sisi Bado miaka ya 1800; ni wajibu wa jamii kuamka kuleta madiliko,fikra chanya Kwa jamii #Inawezekana

America mtu mweusi alisimama kumpisha mzungu akae kwenye siti,

Revolution is not like an apple when it's ripe will fall- Lazima mentality, attitude za watz zibadilike tusiwe watu wakuona hiki hakiwezekani,changes Start by you.
 
Kwa mujibu wa maelezo yake hakuna simu iliyopigwa kokote hao wanajeshi walienda kumtoa kwa fujo hapo lockup kitu ambacho hakiwezekani
 
SUBIRI UGONGEWE.

utarudi tena hapa.
 
Kwa mujibu wa maelezo yake hakuna simu iliyopigwa kokote hao wanajeshi walienda kumtoa kwa fujo hapo lockup kitu ambacho hakiwezekani

Hivi mbona mnaongea mambo kirahisi sana, hao polisi wenyewe ukijifanya kuzijua sheria na haki zako wanakuambia "okay wewe si unajifanya mjuaji sasa utaozea humu", sasa unafikiri hapo kama huna nguvu ya ziada kama pesa au connection unafanyaje
Acha uoga dogo kwenye vitu vya msingi; utakuja lipia hadi barabara upite, drop that mentality,Kila mtu akiwa kama wewe hii nchi itazidi kuingia shimoni
 
Till then, what we are saying now is the reality, thanks
 
Naomba link nikacheke
Hao watu wanapenda kukomoa ukiwaingia vibaya.
 
Sina urafiki na
1. Polisi
2. TISS
3. TRA
4. TAKUKURU

Hata kama tutajua ni ile ya kusalimiana juu Kwa juu ila SITAKI URAFIKI NAO KABISAAAA

#YNWA
 
makamanda hawanaga kwere ila hawa raia wakakamavu anaweza akawa mwanao akukuuza kwa mapimbi wenzie wakupige maokoto
Polis (Hasa Afisa upelelezi) mkoa Simiyu sitowasahau kwa uhuni/ wizi/ unyang'anyi/ ukatili wao.
Niliona ujambazi wa polisi, Simiyu jamani. Wameunda umojawa wizi wakishirikiana na ofisi ya mwendesha mashtaka, mahakama na baadhi ya mawakili. Nilishuhudia watuhumiwa wakifichwa wakubwa zao wanapokuja kuwakagua....
Jeshi la polisi liundiwe chombo cha kulitazama....
 
Hata chinga hayupo tayari kaka dunia uwanja wa fujo?
 
Hakuna njia yoyote ya kibabe kwa kutumia nguvu unayoweza kwenda kumtoa mtu kituo cha polisi labda uvamie na bunduki uwauwe askari ufungue lockup uondoke na mtu wako na siyo vinginevyo, ni kweli hata polisi hawatendi haki lakini hakuna namna unaweza kwenda kumtoa mtu kibabe , njia rahisi ni kufanya mazungumzo au kufata hatua za kisheria ili huyo mtu apate haki yake na siyo kwenda kupiga mkwara hutoboi
 
Dah! Nidhamu ya kutishia polisi? Nidhamu ya kuvunja protokali? Subiri wakati ukifika ndio utajua hujui. Urafiki na wanausalama ndio ila uwe wa kimkakati sana.
 
Umenikumbusha tukio moja la zamani kidogo enzi za jk, mdogo wake na rafiki yangu aliwekwa lock up kimakosa jamaa kwenda kumdhamini/kumtoa askari akaomba rushwa ya laki 2 na nusu, jamaa akaomba apunguziwe atoe 150k, askari akagomea kwenye 200k, jamaa akaondoka. Baadaye rafiki yake akamuunganisha na mkuu wa kituo.
Jamaa alipo obama na mkuu wa kituo na kumweleza akapiga simu dogo akatolewa. Mshikaji akampa mkuu wa kituo sh. 50,000/- tu.
 
Na nikwambie kitu,Wanajeshi wa sahivi wana Akili very Smart sana na wanafundishwa nidhamu ya hali ya juu,Mimi na washikaji kibao huko sasa Fanya Ujinga wako mtaani mwambie atakwambia kabisa fuata sheria umekosea.
Binafsi pia siungi mkono mkosaji. Kila mtu awajibike kwa makosa yake, lkn masada unatakiwa kupewa anaye onewa na polisi. Niseme pia polisi hawaonei mwenye back up, elewa neno back up.
 
Bado hujatoa suluhisho, mfano kijana tu wa mtaani kakamatwa bila kosa na hana pesa wala connection anafanyaje kutoka ndani, pengine anaweza kuwa anazijua sheria na haki zake niambie anazitumiaje hapo ili wamuachie bila kumdhuru
Nacho jua dhamana ni bure, ukikamatwa kawaida bila influence or interest ya Viongozi,kusota kituo Cha polisi ni Uzembe
Binafsi pia siungi mkono mkosaji. Kila mtu awajibike kwa makosa yake, lkn masada unatakiwa kupewa anaye onewa na polisi. Niseme pia polisi hawaonei mwenye back up, elewa neno back up.
Point yangu si Back Up, Point yangu tunatakiwa kutoka zama za Manyani-(Animal Farm life)

Jamii yakutendeana haki bila kujari nafasi ya mtu kwenye jamii either tajiri au masikini hii ndo culture inayotakiwa kuijijenga Kwa watanzani more civilized society,na hii inawezekana kama Kila mtanzania atajua haki na wajibu na Sheria nakusimama kurinda haki ya jirani yake bila woga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…