Well done Jakaya Kikwete

Well done Jakaya Kikwete

Huyo Kikwete si yeye aliyejitapa kawaletea chuma, mzigo mzito mpe Mnyamwezi?

Leo unataka kumfanya kama si sehemu ya mfumo uliomuweka Magufuli?
Kile kilikuwa chuma kina matatizo makubwa.
 
Samia na kikwete ni ndugu mtoto wa mjomba mtoto wa shangazi...lao ni moja hao hiyo ya kusema "Samia na JPM ni kitu kimoja" ni kuwalaghai mazuzu.
Mataga huwa wakisikia hiyo kauli wanafurahi sana
IMG-20210430-WA0126.jpg
 
CCM ni principles na imani ya misingi yake.
Majadiliano tuliyoyaona ndiyo CCM tunayoifahamu.
CCM FAKE ile ya kuchagua wapinzani kuiendesha, visasi, na kufanyiziana tumeona ukomo wake.
Aaaah, ninakuelewa vizuri sana mkuu 'Masopa'; hakika CCM ya miaka mitano iliyopita, hiyo ilikuwa ni CCM ya aina yake kabisa, sitarajii kuwa itatokea tena katika miaka ya hivi karibuni. Hiyo ilikuwa ni CCM "iliyotekwa" na mtu mmoja mwenye mabavu mengi.

Lakini, hata hivyo, hii "CCM ya majadiliano" unayosema tumeiona, hii kweli ndiyo CCM itakayodumu chini ya mama?

Kuna watu humo walishaonja nyama za watu, miaka mitano iliyopita, hawa nao je, mtawafanyaje?

Phew, hivi "principles na imani ya misingi ya CCM ya siku hizi (nina maana ile ya Kikwete, na hii tunayoikaribisha kwa furaha, ya mama) ni ipi vile? unaweza kutukumbusha mkuu Masopakyindi?

Hivi pacha wako 'Jidu' kapotelea wapi, maana yapo mengi ambayo angekuwa ameyachangamkia sana wiki hizi chache zilizopita.
 
Niliweka kambi jukwaa la wakubwa kiongozi. Yule kiongozi wa malaika alikuwa ananichefua na uongozi wake wa kizwazwa...

Namshukuru Mungu kwa kutufanyia wepesi...
🤣🤣majina makubwa kama wewe nilijiuliza umepotelea wapi. Ashukuriwe Mungu ametuondolea mikosi.
 
Ukiwa kiongozi muungwana,mstaarabu na mtu wa watu unazeeka vizuri sana cheki Mwinyi,cheki Kikwete na watoto wao wanafanya siasa safi!!
Wababe hawazeeki vizuri nahata watoto hatuwaoni wakiwaiga wazazi wao yaani hawawi mfano/mentor kwa watoto wao
 
Mkuu unyenyekevu una thamani yake.
Sasawatu ndio tumeona "wasiojulikana " walitoka wapi, walioanzishiwa kesi hewa za kuhujumu uchumi nani alikuwa nyuma yake, kuibiwa wafanyabiashra kupitia TRA aliyeasisi mambo hayo.

Kwa kweli Tumpe mama Samia support yote hali ya utulivu na kawaida katika mustakabali wa nchi urudi tena, na watu waishi kwa amani.
Mtaishi kwa amani siku ccm ikifa rasmi
 
Aaaah, ninakuelewa vizuri sana mkuu 'Masopa'; hakika CCM ya miaka mitano iliyopita, hiyo ilikuwa ni CCM ya aina yake kabisa, sitarajii kuwa itatokea tena katika miaka ya hivi karibuni. Hiyo ilikuwa ni CCM "iliyotekwa" na mtu mmoja mwenye mabavu mengi.

Lakini, hata hivyo, hii "CCM ya majadiliano" unayosema tumeiona, hii kweli ndiyo CCM itakayodumu chini ya mama?

Kuna watu humo walishaonja nyama za watu, miaka mitano iliyopita, hawa nao je, mtawafanyaje?

Phew, hivi "principles na imani ya misingi ya CCM ya siku hizi (nina maana ile ya Kikwete, na hii tunayoikaribisha kwa furaha, ya mama) ni ipi vile? unaweza kutukumbusha mkuu Masopakyindi?

Hivi pacha wako 'Jidu' kapotelea wapi, maana yapo mengi ambayo angekuwa ameyachangamkia sana wiki hizi chache zilizopita.

IMANI YA CCM

  • Binadamu wote ni Sawa
  • Kila mtu anastahili heshima ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake
  • Ujamaa na kujitegemea ndiyo njia pekee ya kujenga jamii ya watu walio sawa na huru

AHADI ZA WANACHAMA WA CHAMA CHA MAPINDUZI

(1) Binadamu wote ni ndugu zangu na Afrika ni moja

(2) Nitaitumikia nchi yangu na watu wake wote

(3) Nitajitolera nafsi yangu kuondosha umaskini, ujinga, magonjwa na dhuluma.

(4) Rushwa ni adui wa haki, sitapokea wala kutoa rushwa.

(5) Cheo ni dhamana, sitatumia cheo changu wala cha mtu mwingine kwa faida yangu.

(6) Nitajielimisha kwa kadri ya uwezo wangu na kuitumia elimu yangu kwa faida ya wote.

(7) Nitashjirikiana na wenzangu wote kujenga nchi yetu.

(8) Nitasema kweli daima, fitina kwangu mwiko.

(9) Nitakuwa mwanachama mwaminifu wa CCM na raia mwema wa Tanzania na Afrika.

Mkuu nimekuwekea Imani na misingi ya ya CCM , misingi ambayo imetumika miaka yote kukiendesha chama.
Haijalishi nani yupo katika uongozi wa juu, lakini misingi hiyo na uendeshaji wake ndiyo roho ya chama.

Mama Samia alipopata tu Urais aliweka mbele misingi hiyo, hasa kwenye haki za mtu binafsi, kutoonewa na kuondoa dhulma(wasiojulikana), kuwa na uhuru wa habari, kutoa mawazo yako kwa uhuru, kujitegemea na kutobugudhiwa isivyo halali katika kipato na serikali(TRA).

Kimsingi kwa kusema tu hayo, Mama Samia alirudisha imani kubwa ya wanachama kwa CCM.

Na hapo ndio wazoefu kama JM Kikwete wamafanya kazi kubwa kumsaidia Mama kuweka imani hiyo kwa vitendo na kwa uzoefu wao.

Mtu yoyote akienda kinyume na imani hizo na principles zake, hana chama.

Kuhusu Jidu, mtafute , yumo mtandaoni namwona , ingawaje anaikwepa mada.
Si ajabu naye yuko kwenye lile genge la kanda, na linamsuta.
 
Tutaanza kutembeza vibaba tena, hayo ndio waliyoyataka baada ya kuwekwa kapuni na chinga pamoja na jiwe,sasa wote hawapo kila mtu anatoka shimoni, tunakoenda siko.
Una uhuru wa kutokwenda mkuu.

Hamia nchi nyengine tuache Sisi Watanzania tumuunge mkono mama
 
Kikwete mitandaoni anatazamwa kwa mitazamo mibaya lakini kwa waliowahi kufanya nae kazi wanafahamu uwezo wake kikazi na ushirikiano alio tayari kuutoa kwa mtu.

Mama hawezi kugeuka wala kupindua, kakamatwa vizuri tu ukizingatia Mzee wa Chalinze ndiye aliyempa cheo huku bara.
 
IMANI YA CCM

  • Binadamu wote ni Sawa
  • Kila mtu anastahili heshima ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake
  • Ujamaa na kujitegemea ndiyo njia pekee ya kujenga jamii ya watu walio sawa na huru

AHADI ZA WANACHAMA WA CHAMA CHA MAPINDUZI

(1) Binadamu wote ni ndugu zangu na Afrika ni moja

(2) Nitaitumikia nchi yangu na watu wake wote

(3) Nitajitolera nafsi yangu kuondosha umaskini, ujinga, magonjwa na dhuluma.

(4) Rushwa ni adui wa haki, sitapokea wala kutoa rushwa.

(5) Cheo ni dhamana, sitatumia cheo changu wala cha mtu mwingine kwa faida yangu.

(6) Nitajielimisha kwa kadri ya uwezo wangu na kuitumia elimu yangu kwa faida ya wote.

(7) Nitashjirikiana na wenzangu wote kujenga nchi yetu.

(8) Nitasema kweli daima, fitina kwangu mwiko.

(9) Nitakuwa mwanachama mwaminifu wa CCM na raia mwema wa Tanzania na Afrika.

Mkuu nimekuwekea Imani na misingi ya ya CCM , misingi ambayo imetumika miaka yote kukiendesha chama.
Haijalishi nani yupo katika uongozi wa juu, lakini misingi hiyo na uendeshaji wake ndiyo roho ya chama.

Mama Samia alipopata tu Urais aliweka mbele misingi hiyo, hasa kwenye haki za mtu binafsi, kutoonewa na kuondoa dhulma(wasiojulikana), kuwa na uhuru wa habari, kutoa mawazo yako kwa uhuru, kujitegemea na kutobugudhiwa isivyo halali katika kipato na serikali(TRA).

Kimsingi kwa kusema tu hayo, Mama Samia alirudisha imani kubwa ya wanachama kwa CCM.

Na hapo ndio wazoefu kama JM Kikwete wamafanya kazi kubwa kumsaidia Mama kuweka imani hiyo kwa vitendo na kwa uzoefu wao.

Mtu yoyote akienda kinyume na imani hizo na principles zake, hana chama.

Kuhusu Jidu, mtafute , yumo mtandaoni namwona , ingawaje anaikwepa mada.
Si ajabu naye yuko kwenye lile genge la kanda, na linamsuta.
OOOooh My!

Mkuu Masopakyindi; 'seriously' sikutegemea ungefanya hivi - lakini maadam umefanya, naamini kabisa hiyo kadi yako ilikuwa ni halali kabisa; na inawezekana sana ulikuwa kati ya walioiva barabara!

Sasa hii ni leo na kwa hali iliyopo. Mengi ya hizo "'Principles"', na unayoiita "misingi" kwa wengi ndani ya chama hicho ni kama historia mbaya.

Hebu, angaliakwa mfano hizo "AHADI". Si nyingi ya hizo wakati huu ni kama takataka?

Anyway, wengi wetu kwa ujumla wetu sote, tunaitakia mema mengi nchi yetu pamoja na watu wake wote. Sina shaka hata chembe kabisa, kwamba Kikwete ni MZALENDO wa kweli wa nchi hii, hilo sina shaka naye kabisa.

Yeye kakulia ndani ya chama kabisaaaaa; na hizo AHADI na makorokoro yote yale anayjua sana, na bila shaka alikuwa akiyaimba kama msahafu huko TANU Youth League.

Alipochukua hatamu ya uongozi, labda yeye aliamini njia zake mpya ndio zitalisukuma taifa kwa haraka na watu wote (na wanyonge wa Magufuli) wakiwemo, kuinua maisha yao kupitia kwenye njia zake hizo mpya, ambazo naona nawe ni muumini wake mkubwa juu yake.

Huenda siku moja utapata nafasi utatueleza, kama ulivyonistua hapa leo na hayo uliyoyaweka kuhusu CCM ya 1977..., haya mapya ya CCM ya Kikwete, na pengine sasa itakuwa ya 'Hasan'.
 
Back
Top Bottom