Wema Sepetu, Mr. Blue, TID, Recho wahusishwa na Dawa za Kulevya. Watakiwa kuripoti kituo cha Polisi

Wema Sepetu, Mr. Blue, TID, Recho wahusishwa na Dawa za Kulevya. Watakiwa kuripoti kituo cha Polisi

View attachment 466457



Akitoa taarifa katika kipindi cha infomer cha clouds FM kufuatia msako wa kukamata wahusika wa madawa ya kulevya alichofanya mkuu wa mkoa Paul makonda.

Askari 9 wamekamatwa wakishirikia na wauza madawa ya kulevya Huku wasanii watumiaji wa madawa hayo wakitajwa na kutakiwa kuripoti polisi wenyewe mapema ,

wasanii waliotajwa na kutakiwa kuripoti polisi ni
1. Wema sepetu
2. Petiman wakuache
3. TID
4. Mr. Blue
5. Recho(kizunguzungu)

SOURCE; Clouds FM (Informer)

NB: Suala la Dawa za Kulevya limikuwa likizungumziwa na kupewa kipaombele kwa muda mrefu hapa JamiiForums. Kwa taarifa zaidi tembelea mada hii, kupata orodha ya mada nyingine nyingi zinazojadili suala hili - Madawa ya Kulevya na aibu ya Tanzania - Yatosha sasa!

Hawa ni nyoka wadogo sana. Hawa hawawezi kupita Mwalimu Nyerere International Airport na KIA bila kukamatwa.
Makonda wataje wale ambao huwa wanapitisha mzigo Airports zetu bila kukamatwa.
 
Huwa hawataji wahusika,sijui wanakula viapo vya aina gani..!!
Katika kupambana na madawa ya kulevya ukatili hauepukiki!

Unafikiri ukiwauliza huko mtaani watasema??
 
Unaweza kuta child Benz hamjui mkuu wa mzigo , unakuta yeye ananunua kwa MTU wa 3 au 4
Kamaanisha aanze na chid aje uyo mtu wa tatu wa pili atimaye wa kwanza nadhani pia kafanya hivyo ndo mana kawapata hao wakuu kupitia watumiaji wa mwisho
 
Huo ndio mnyororo tunataka, hata akiwa anapata kwa mtu wa nne, akionyeshwa kazi huyo mtu wa nne atataja mtu wa tatu, akionyeshwa kazi mtu wa tatu atataja mtu wa pili kwa vyovyote vile.. Katika hili lazima ukatili wa hali ya juu utumike kama itakavyohitajika!
Kwa sheria utamfunga huyo mtu aliyetajwa?? Na kwa uthibitisho upi pasina shaka?? Hakuna kesi hapo.. kuna siasa tu
 
HIVI JAMANI NAJIIPELEKAJE POLIS KWA JINA LA TID KWA MFANO? SIUNGI MKONO MUUZAJI WALA MTUMIAJI ILA WELEDI UTUMIKE
 
Watanzania wengi watasherehekea habari kama hii,lakini kwa ukweli dhana ni kitu kibaya sana,kama mtu hajakamtwa na ushahidi wa kufanya hayo mambo ya madawa ya kulevya basi ni kosa kumtaja jina lake ,huu ni udhalilishaji wa haki ya mtu..

Nafikiri nchi yetu ina vyombo vinavyohusika na makosa kama haya,kwanini mkuu wa mkoa haachii hizo mamlaka zikafanya kazi yake...,Tanzania yunakwenda wapi,kama polisi wanaushahidi kwanini hawawakamati hao wahusika na kuwapeleka mahakamni...

Nawewe inabidi ukamatwe,,tunahisi ni mmojawapo,, NGOJEA tuwaambie tusk force wakuje kukudaka😀
 
Hawa akina akasha na Vicky goswami ukiwafuatilia vizuri kunanuhusiano na yule Rummy shoo alivyoshikwa Kenya. Na toka kina akasha wapate kukamatwa na kuwa under radar. Rummy nae akaanza kufulia kwa kasi sana.
Hawa wadosi walikuwa wafanyabiashara hapa bongo.
Hawa Akasha grup ni wa zamani sana, wameuwa sana askari wa kenya hawa ndiyo walio kuwa wanafanya biashara na ikulu ya kenya enzi za Mwai Kibaki hawa jamaa walikuwa mafia sana
 
mkuu biashara ya unga sio sawa na ile ya kuuza na kununua pipi....kwamba ukiulizwa tu unamtaja mangi fasta....no biashara ya madawa ni hatar na very serious kiasi hawaoni ajabu kumpoteza yeyote atakae zuia njia zao...!!!!!

Kiukweli hao waliotajwa kama kweli wanajihusisha na mizigo basi maisha yao ni hatar zaid mikononi mwa madrug dealers kuliko hata mikononi mwa serikali. wale jamaa hawanamchezo and they have strong support behind.
 
Back
Top Bottom