Wengi hawayajui haya

Wengi hawayajui haya

8ae87a7cd3d5bc282fc764af5f85a899.jpg
Nimeyala kwa mara ya kwanza Rwanda, yapo mengi sana huko
 
Magogwe kwa wapera matungusha kwa wachagga...hhahah
Hata wasambaa wayaita hivyo, mara nyingi yapikiwa kwenye mlenda, hasa hasa mlenda wa unga, unaweza ukalichemsha au kuchoma kisha ukamenya maganda ukalumangia kwa ugali. Yakikomaa vizuri watoto wanayala bila kupikwa wala kuchomwa.
 
Haya matunda ni mengi sana huko maeneo ya uwemba njombe na hua tunaita matunda damu.

Ina maana haya matunda kuna sehem wanayaweka kwenye mboga?au kuyachoma na kuyatumia kama mboga?nilikua sijui kabisa.

Kwa bibi yangu yanaitwa matungusha, yanatumika kama substitute ya nyanya kupikia. Yanaliwa pia hivyo hivyo na kama niah anavyosema yako very sour but full of vitam C ila tatizo ni kwamba huu mmea unaelekea kuwa extinct, so mshana jr big up kukumbushia but do somemthing kuhusu mbegu yake.

Nyie mtakua mnayaita matunda damu labda kutokana na hiyo vitamin C nyingi ambayo ina-aid absorption ya madini ya chuma mwilini, lakini huwa hayana rangi nyekundu kama yale matunda damu ambayo ni mekundu.
 
hayo ufipani tunayaita matunda damu sababu ndani ni mekundu kama damu
Kweli ufipa yanaitwa matunda damu, nakumbuka enzi hizo unalipasua katika ya tunda unaweka sukari ili kupunguza uchachu wa hilo tunda ndio linaliwa
 
Mbeya umalila yapo mengi sana hayo na yanastawi sana sehemu zinazo pata mvua nyingi huwezi kuyakuta sehemu yenye asili ya jangwa.
 
Hayo makilaume uyakute yapo ndani ya msele.....yaani unaweza ukajikuta unamaliza kilo nzima ya dona peke yako....
 
Back
Top Bottom