Ningependa mabadiliko ndani ya CDM hasa tukizingatia Mbowe kakaa pale muda mrefu sana.
That's good and it's true...
Ninachoogopa ni kufanya mabadiliko ambayo yaweza kuja kukiyumbisha chama siku za usoni.
How? Humwamini Tundu Lissu huyu ambaye ni adui wa CCM na serikali wapinzani wenu..? Unataka kiongozi wa CHADEMA mwenye ushirika na CCM? Really?
Lissu ni kiongozi mzuri lakini anapapara sana na hii inaweza kuja kukigharimu chama.
Papara gani hizo? Unaweza kuthibitisha..?
Humjui na humtazami Tundu Lissu kwa usahihi..!
Sifa ya Tundu Lissu ni kuwa yuko very straightforward, si mtu wa kumung'unya maneno, mpenda haki, mpenda uwazi na ukweli, anaichukia rushwa kwa maneno na kwa vitendo na hata ukimtazama anapoongea unamjua bila shaka yoyote kuwa anamaanisha asemalo, jasiri na mtu anayethubutu, si mwoga...
Kama sifa hizi ni "papara" kwako, basi una shida ktk ufahamu wako...
Nilianza kupata shaka shaka juu yake alipoanza kukikandanya chama chake wake yeye ni sehemu ya uongozi.
Amedanganya kuhusu nini..?
Mwenyekiti Freeman Mbowe alisema hivi juzi pale nyumbani japo hakumtaja Lissu kwa jina lakini obvious alikuwa anamlenga huyu bwana...
Tunachotaka mseme, ni kuthibitisha uongo wake kwa kila anachosema kuhusu chama chenu..
Semeni hivi: Kasema 1, 2, 3, 4 nk ya uongo. Ukweli ni 1, 2, 3, 4 nk..
Lakini kutoa tu sweeping statement za jumlajumla kuwa "ni mwongo" halafu hamthibitishi uongo wake, then hamna hoja...
##By the way, nilikuuliza kuwa, ukiachilia mbali Freeman Mbowe ambaye muda wake kiuongozi haupo upande wake tena, ni nani anayeweza kum - surpass Tundu Lissu ndani ya CHADEMA hii ya sasa kukalia kiti hicho kwa majira na nyakati za siasa za leo, ngumu na za kibabe kama sio Tundu Lissu..??
Be honest, jibu swali hili...