Wenje: Lissu alimsingizia Mbowe kahongwa magari mawili

Kumuamini mbowe kwataka moyo, Yaani mlungula wa Abdul inaonekana umetembea Sana kwa wenje na kundi lake
 
Nakipenda hiki Chama wakikuchoka wanatoa siri zako zote mlizokuwa mnapanga wote mtuhumiwa anakasirika anatoka Chama, akishatoka na mtoa Siri muda ukifika naye anatumiwa njia hiyo hiyo, wanacheza na mtoto wa katikati ya jiji [emoji2][emoji2][emoji2]
 
Ukinunua gari ubalozini wanakupa namba za ubalozi pia?
 
Ukinunua gari ubalozini wanakupa namba za ubalozi pia?
Nakujibu ingawa hili swali ni la mtoto wa form 2B.

Yah lakini utatakiwa kwenda TRA kuzibadilsha na kulipa kodi stahiki.
 
Yaan huo Mnada, Ubalozi walimstua Mbowe tu, ukawa ni Mnada wa Siri kiasi kwamba LISSU hakukua kabisaaa Wala hamna mwanachama mwengine alojua.


Sehem ya wanasiasa ambao akiongea ,usimtilie mashaka ni LISSU, na MPINA.
Mbowe aliipa taarifa sekretariati kuwa kuna mnada na akawashauri nao wanunue magari. Na minada ya ubalozi inatangazwa kwenye magazeti na kwenye mitandao. Aidha, lile ni suala lake binafsi na hawajibiki kukitaarifu chama chake.

Mbowe ni mfanyabiashara ndio maana anafuatilia. Lissu sio mfanyabiashara ndio maana hafuatilii. Ndio maana alipoambiwa kuwa Mbowe amehongwa magari akaamini. Inaelekea ni mwepesi sana kuamini majungu.

Amandla...
 
Hivi ukihongwa gari nyaraka hupewi?πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Usiwe mjinga kasema kahongwa gari na serekali.

Kumbe Mbowe kanunua gari mtumba katika mnada wa hadhara.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…