DOKEZO Wenye Hospitali binafsi wakataa kuwahudumia wateja wa NHIF kutokana na vifurushi vipya

DOKEZO Wenye Hospitali binafsi wakataa kuwahudumia wateja wa NHIF kutokana na vifurushi vipya

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Hii ndio maana ya mfuko kujiendesha kitathmini na tafiti ,kuongeza pale inapohitajika ,sio kila kitu kinapanda bei kadri siku zinavyokwenda vingine bei inashuka kutokana na upatikanaji wake ,inawezekana upatikanaji wa amoxilin umeongezeka kuliko ilivyokuwa awali hakuna haya ya kuongeza bei na hii ni lengo zuri la kupunguzia mzigo wanachama wake , lakini ni mfuko huuhuu ambao umekuwa ukiwezesha watoa huduma kwa fedha(loan) kuboresha miundombinu pale inapohitajika ili kuviongezea uwezo ,mfuko haugemei upande mmoja unajali wadau wake wote
Mkuu Thibitisha ulichokisema hapo juu!
Bei zote za Dawa hakuna hata moja iliyopanda toka mwaka 2013 huku..bei za dawa Madukani zikiwa juu ila wao wamestick kwemye bei ile ipe ya zamani..
Mazingira kwa watoa huduma Hayajaboreshwa still bado ni Sera ile ile ya mwaka 2013..
Ina maana hakuna vitu vilivyobadilika kwa takribani miaka 10, jibu ni hapana..

Sasa shida ni nini ni kutaka kukomoa watu..

NImezungumzia Amoxyline kama sample tu..
So unamaanisha upatikanaji wa Dawa nchini umeongezeka?

Nahisi haupo.kwenye Kada ya Afya na ndio.maana unapata Hata uwezo wa kuandika ulichoandika ..

Niambie Bima ya Afya (NHIF) Imewahi kumkopesha mtoa huduma Gani kati ya mwaka 2015 mpaka leo?

Tusiingize siasa kwenye mambo ya Kitaifa mambo ya afya ambayo watakaoemda kuumia ni Wananchi na wachangiaji wa Bima wala.sio Sisi wamiliki au hao BIma wenyewe..
 
Nawaunga Mkono Mia fill 100..
Huwezi kuboresha kitita na ukaacha Kuboresha maslahi ya Watoa Huduma pamoja na Bidhaa husika na Baada ya kuambiwa bado unashupaza shingo..

Amoxyline iliyokuwa inalipwa kwa Bima miaka 10 iliyopita sh 80 kwa kidonge still bado baada ya miaka 10 bei ni hiyo.hiyo..Bila kuangalia Soko la Bidhaa la sasa unapanga bei bila huruma ya watu wenye Hospitali ambao wao hawaletewi dawa na MSD..
as one among the interested personel nasema wako sahihi na hatutapokea Mtu mwenye Bima Yoyote. Mpaka pale serikali itakapo thamini Mfumuko wa bei na maslahi ya pande mbili
Urinalysis -1,400/=
😔
 
Kama wanakataa maboresho sijui wafanyiwe nini mana NHIF wamewaita mezani na wakafika wakatoa ya moyoni sasa ninapoona wanageuka unaona kama kabisa wanaleta siasa kwenye wa binadamu wabadilike
Umesoma Barua ilivyoandikwa wamekaa mezani lakini NHIF wamegoma kupokea mabadiliko sasa ulitaka wafanye nini wao wakubali..

Nini maana ya mjadala si nikukubaliana na kila mtu awe benefit nayo sio nikuache wewe ulipata faida halafu mimi nipate hasara
 
Kama wanakataa maboresho sijui wafanyiwe nini mana NHIF wamewaita mezani na wakafika wakatoa ya moyoni sasa ninapoona wanageuka unaona kama kabisa wanaleta siasa kwenye wa binadamu wabadilike
Wewe umesoma kweli? Yani watu wafanye kazi ya bure? Hela zenyewe zinachelewa sana kuja kwenye mahospitali halafu unaboresha huduma unawasahau wadau wakubwa kama hawa sekta binafsi?
Kama jambo hili litakwama na serikali ikakaza shingo hapa ni wananchi tutakao umia……wengi tunazitegemea hizo hospitali binafsi!
 
Kama wanakataa maboresho sijui wafanyiwe nini mana NHIF wamewaita mezani na wakafika wakatoa ya moyoni sasa ninapoona wanageuka unaona kama kabisa wanaleta siasa kwenye wa binadamu wabadilike
Aaaah mkuu,
Kwani kutoa ya moyoni ndo kukubali?
Baada ya kutoa ya moyoni nini kilifanyika ili kufikia muafaka..
Wenyewe wameweka wazi kwamba muafaka haukifikiwa. Hawajakataa kukutana na wewe ninyi.
Watuambia habari Gani hapa...
 
Hivi wakuu kikatiba ili uwe waziri ni lazima uwe mbunge!! Na ili uwe mbunge lazima ujue kusoma na kuandika + kubwabwaja uongo na ukweli...

Uwaziri ungekua unapatikana kitaaluma kama mameneja wa mabenki nk labda kuna mambo yangebadilika, hawa wanasiasa wengi wao ni wajivuni mno.
 
Wewe umesoma kweli? Yani watu wafanye kazi ya bure? Hela zenyewe zinachelewa sana kuja kwenye mahospitali halafu unaboresha huduma unawasahau wadau wakubwa kama hawa sekta binafsi?
Kama jambo hili litakwama na serikali ikakaza shingo hapa ni wananchi tutakao umia……wengi tunazitegemea hizo hospitali binafsi!
Mkuu Leak ,
Si TU kwamba maboresho hayajawagusa watoa huduma kama inavyosemwa, bali bei za huduma nyingi zimeshushwa ndo maana hospitali wanahlfia kupata hasara.
Tumepewa mfano wa urinalysis kushushwa toka tzs 2000 Hadi tzs 1400.
Ukifatilia Kwa umakini, kinacholalamikiwa zaidi ni malipo ya huduma kushushwa.
Huduma ya dialysis, anti cancer drugs ni miongoni mwa huduma na dawa zilizoshushwa bei Kwa kiwango kikubwa.
 
Hatari sanq,NHIF kilamara tunasema humu kama hawawezi kutoa huduma bora wajitoe au watangaze kufirisika,haiwezekani kufanya siasa kwenye afya zetu,naumia sana kuona mshahara wangu ukikatwa huku nikiwa sina uwezo wa kupata matibabu bora.

Pili nhif kama wanaona hawapati faida kwa kiasi wanachotukana hasa wstumishi wa umma,ni bora waseme ili kiasi kiongezwe,kiuhalisia haingii akilini mimi kukatwa sh 23 000 kwa mwezi huku pesa hiyo ikilipia/kuhudumia watu 6,ukigawawanya maana yake kila mtu anachangia shilingi takribani 3 800 kwa mwezi huku akipata matibabu ya mamilioni.

Nhif waweke vifurushi ambavyo watumishi wa uma watachagua ili wapate huduma bora,tuache, ujamaa kwenye mfumo wa kibepali,kwa umuhimu wa Bima mimi niko tayri kukatwa mara mbili au hata tatu ya kiasi wanachonikata sasa ili kupata huduma bora

NHIFTZ basi tuueni wateja wenu ili mfaidi makato tunayokatwa,Mungu saidia wazee wetu wanaohudumiwa na hospitali za private wasikufe kwa kukosa huduma
 
Hahaha mchakesha sana unadhani watakao athirika ni kina nani? Hospitali zenyewe za Umma mtu unakwenda hata panado hakuna unafikiri nani ataumia?
Wizara ya Afya Tanzania iache kufanya mzaha kwenye hili
Wewe unafikiri atakayeathirika ni nani,labda nikwambie athari itakayotokea wenye hospitali ndiyo wataathirika zaidi maana wengi wao kilichowasukuma kufungua hizo hospitali ni tamaa ya kupata utajiri wa haraka haraka kupitia NHIF japo wenyewe wanajifanya lengo lao ni kutoa huduma kwa wananchi na kwamba fedha sio kipaumbele chao lakini si kweli na kama wana jeuri wagome angalau kwa miezi sita tu kama hawajafunga hivyo vihospitali uchwara vya mchongo,haiwezekani huduma inayolipiwa kwenye hospitali za umma wao walipishe mara nne zaidi wakati hivyo vihospitali vyenyewe vingi havina maajabu.
Hawa watu ni wezi na inaonekana na wewe ni mmoja wao sasa safari hii muhesabu maumivu chaguo ni lenu ama mtoe huduma kwa bei halisi au mfunge hivyo vihospitali vyenu na kelele hizi zinapigwa sana na vile vihospitali vya uchochoroni siamini kwenye ujinga huu utawakuta hindu mandal,aghakhan au regency wao wanashurutishwa tu na huenda hata kutishiwa na hayo majizi.
 
Hatari sanq,NHIF kilamara tunasema humu kama hawawezi kutoa huduma bora wajitoe au watangaze kufirisika,haiwezekani kufanya siasa kwenye afya zetu,naumia sana kuona mshahara wangu ukikatwa huku nikiwa sina uwezo wa kupata matibabu bora.

Pili nhif kama wanaona hawapati faida kwa kiasi wanachotukana hasa wstumishi wa umma,ni bora waseme ili kiasi kiongezwe,kiuhalisia haingii akilini mimi kukatwa sh 23 000 kwa mwezi huku pesa hiyo ikilipia/kuhudumia watu 6,ukigawawanya maana yake kila mtu anachangia shilingi takribani 3 800 kwa mwezi huku akipata matibabu ya mamilioni.

Nhif waweke vifurushi ambavyo watumishi wa uma watachagua ili wapate huduma bora,tuache, ujamaa kwenye mfumo wa kibepali,kwa umuhimu wa Bima mimi niko tayri kukatwa mara mbili au hata tatu ya kiasi wanachonikata sasa ili kupata huduma bora

NHIFTZ basi tuueni wateja wenu ili mfaidi makato tunayokatwa,Mungu saidia wazee wetu wanaohudumiwa na hospitali za private wasikufe kwa kukosa huduma
NHIF ni wanyama...hakika hili ni Pigo kuu...
 
Back
Top Bottom